Rostam Aziz: Dkt. Slaa alihongwa 2015 kuisaliti CHADEMA, akapewa Ubalozi

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,219
103,804
Mchana wa leo Rostam amefanya mkutano na waandishi wa habari. Pamoja na mambo mengine ametoa tuhuma nzito kwa serikali na mahakama.

Amesema Dr. Slaa alinunuliwa wakati wa uchaguzi na kukisaliti chama chake cha Chadema na kisha kupewa ubalozi. Hizi ni tuhuma nzito za rushwa wakati wa uchaguzi.

Rostam anasema mashtaka ya mkataba wa kimataifa hayawezi kupelekwa kwenye mahakama zetu kwa sababu Mtu wa serikalini anaweza tu kupiga simu kwa hakimu au Jaji na kumpa maelekezo ya hukumu. Mahakama yetu ina majibu wa kujibu tuhuma hizo.

--
Watanzania wakumbuke kuwa, huyu mtu (Dkt. Slaa) alipokuwa CHADEMA mwaka 2015 alikisaliti chama chake wakati kukiwa kinaelekea kwenye uchaguzi, alikisaliti chama chake kwa kuhongwa, alihongwa ndipo akaasi na kukisaliti chama chake (CHADEMA). Alikaa zake pale Serena baada ya pale akapanda ndege kwenda Canada na kisha akapewa ubalozi

Kwa kifupi Dkt. Slaa hana uadilifu wala uaminifu wa kunisema, mtu ambaye hana msimamo, mbinafsi , anayeangalia maslahi yake na hajawahi kuchangia chochote katika uchumi wa nchi yetu kazi yake ni kupiga tu mdomo. Mtu wa namna hii kumjibu ni shida lakini ni lazima wakati mwingine umjibu
 
Mchana wa leo Rostam amefanya mkutano na waandishi wa habari. Pamoja na mambo mengine ametoa tuhuma nzito kwa serikali na mahakama...
Kangaroo Courts haziaminiki mahala popote pale duniani. Aidha, Serikali za Afrika zinazofuata mfumo wa kikomunisti au ujamaa (ambao Waliberali wanauhesabia kama Udikteta) nazo pia haziaminiki.

Mahakama zetu zingekuwa zinaaminika, Migogoro itokanayo na Mikataba ya Kimataifa ambayo Serikali imeingia ingekuwa inatatuliwa hapa hapa nchini.
 
Sidhani kama kuna uongo hapo kwa hayo aliosema. Watanzania tunaendeshwa kwa mihemko na wazimu kichwani.

1) Mikataba Ya Kimataifa (International Contracts) huwa ina tafsiriwa/kuvunjwa/kurekebishwa/kutolewa maelekezo/kudaiwa fidia kwa kutumia Mahakama Ya Kimataifa Ya Biashara pindi mgogoro unapotokea.

Hii ni kwasababu ya kuepusha mataifa au makampuni ya kimataifa, kila mmoja kuvutia upande wake kwenye matumizi ya mahakama za nchi zao pindi mgogoro utakapotokea kwenye mkataba husika.

Mfano, issue ya bandari, Tanzania avutie kutumia Mahakama Za Tanzania ikitokea mgogoro, na Dubai wavutie kutumia Mahakama Za UAE ukitokea mgogoro. Ili kuweka usawa kwenye matumizi ya mahakama basi inatumika ya Mahakama Ya Kimataifa Ya Biashara (Labda pande zote mbili wakubaliane kwa pamoja vinginevyo mahakama gani itumike kukitokea mgogoro).

2) Swala la Dr Slaa, anajulikana yule mzee ni muongo, mzandiki, mfitinishaji na mnafiki. Aliwageuka sio CHADEMA TU, aliwageuka watanzania wote waliokua wanapambana kuitoa CCM kwenye utawala wa kizayuni tokea uhuru wa nchi hii. Na hilo lingetimia 2015! Ila

Akauza utu wake na heshima yake kwa kununuliwa, Akaasi Kambi ya upinzani (Sio chadema tu), Akauza ramani zote za upinzani za kivita, kisha akakimbilia CANADA. Akawa akiishi maisha ya kifahari na upande mwingine akitengeneza sinema anafanya kazi "SUPER MARKET". Watanzania walivo vilaza, wakaamini Dr mwenye PhD anafanya kazi Super Market kufungia wateja mifuko.

TUKUBALI AU TUKATAE, tutafute sababu kila aina, tuwabague na kuwabeza hawa wanaoongea ukweli licha ya vyama vyao au itikadi;

SPEAKER WA BUNGE, MAWAZIRI, WABUNGE: - kwa pamoja, ndio wameifirimba Tanzania bila kilainishi wala mate kwenye hili swala la bandari! CCM bado ipo kwenye ubora wake wa kuliangamiza taifa!

1) Kupitia kwa Mwang'onda, CCM walitaka kuiuza Kigamboni.

2) Kupitia kwa Kagasheki, CCM walisafirisha wanyama pori kule Arusha. Tena kwa kutumia Uwanja wa Ndege wa KIA, cha ajabu tukaja kuambiwa "Tembo na Twiga wetu wameibiwa sana!!!". Hivi mtu mwenye akili timamu anaweza kuamini kwamba Tembo au Twiga anaibiwa? Mtu akimuiba Tembo au Twiga anakwenda kumficha wapi akishamuiba? Kwenye mfuko wa rambo au box umpitishe Airport mamlaka zisimuone? Watu wanakula hela, wanajichukulia wanyama na kuuza wanavotaka tunaambiwa wanaibiwa wanyama!!!

CCM ndio saratani inayoliangamiza taifa hili!
 
Huyu fisadi rostam anapata wapi nguvu ya kumsema slaa? Huyu si ndio alituuzia vocha feki na kampuni yake ya shivacom? Na hakushtakiwa?

Hawa ndio wamemwingiza mama kwenye matatizo ya bandari Kwa tamaa ya kutaka kupora mali za nchi? Na huyu mtanzania feki anapata wapi uhalali wa kuwazungumzia watanzania original?
 
Back
Top Bottom