Rostam aibukia kanisani!

Rostam aibukia kanisani!

hawa wawili hawatofikishana mahakamani.. this is the biggest scam of all times.. hawa wanacheza mchezo wa "good cop bad cop"...
Unajua, the more I read between the lines nazidi kupata picha nyingine kabisa. Wataishia patamu!
 
Spika apiga marufuku mjadala wa Pinda

SPIKA wa Baraza la Wawakilishi, Bw. Pandu Ameir Kificho, amepiga marufuku mjadala uliozuka katika Baraza la Wawakilishi ukipinga kauli ya Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, kwamba Zanzibar si nchi.

Bw. Kificho alisema suala hilo kwa sasa linashughulikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, ambayo tayari imetoa maelekezo katika kulipatia ufumbuzi tatizo hilo.

"Wajumbe wa Baraza, kuanzia sasa napiga marufuku mjadala uliozuka kwamba Zanzibar si nchi au ni nchi ... suala hili kwa sasa linashughulikia na Ofisi ya Waziri Mkuu," alisema Bw. Kificho.

Alisema tayari Waziri Mkuu ametoa maelekezo na kuwataka wanasheria wakuu wawili kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutoka Zanzibar kukutana na kulipatia ufumbuzi tatizo hilo, ambalo linatokana na tafsiri ya Katiba.

Bw. Kificho alikuja juu baada ya mjadala huo ambao uliibuliwa na Bw. Pinda Dodoma baada ya kuulizwa swali na Mbunge wa Chwaka, Bw. Yahya Kassim Issa, aliyeuliza kama Zanzibar ni nchi kamili na kuzusha malumbano katika chombo hicho.

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walianzisha tena mjadala huo katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, ambapo Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba pamoja na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, kusisitiza kwamba Zanzibar ni nchi kamili.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Bw. Mzee Ali Ussi, alimtaka Waziri Mkuu Pinda, kuliandikia barua Baraza la Wawakilishi na si kuwataka Wanasheria Wakuu wa Zanzibar na wa Muungano kukutana.

Bw. Kificho alitumia nasaha hizo kwa lengo la kupunguza kasi na munkari ya wajumbe wa Baraza ambao walionesha wazi kukasirishwa na kauli ya Bw. Pinda.

Kauli ya Waziri Mkuu Pinda kwamba Zanzibar si nchi imezusha mtafaruku mkubwa kwa wananchi wengi wa kawaida wa Unguja na Pemba ambao wameelezea hofu yao sasa ya kumezwa na Bara.
Tuma kwa Rafik

SAsa wanataka waitwe nchi?haya basi Zanzibar ni nchi mmeridhika?Rubbish they are under us and they should thank us for all we are doing for them coz hawatusaidi ketu maana sisi tukipata msaada unawahusu ila ya kwao haituhusu.
 
i love this movie .........mtikila na rostam
 
Tumuone Aende Mahakamani Akathibitishe Madai Yake Maana Kila Mtu Kwake Si Raia Wa Tz, Akathibitishe Hilo Huko Na Si Magazetini
 
kesi Ya Mtikila Dhidi Ya Mwanahalisi Ni Namba 55.
Kesi Ya Rostam Dhidi Ya Mwanahalisi Ni Namba 54.
Kesi Ya Mtikila Dhidi Ya Tanzania Daima Ni Namba 57.

Kesi Hizi Zimefunguliwa Mwaka Huu Mwezi April ,kumbuka Huyu Mchungaji Alipewa Fedha Muda Na Siku Hizo Hizo.

Nawatakia Tafakuri Ya Kina.

He! Mbona Hapa Naona Kizunguzungu!??
 
kaaz kweli kweli
lakini si alipokea hela??? haijalishi kakopa au kamfisadisha ila cha msingi kapokea mijisenti and he's at it... let him face it

Kwanza cha msingi tungenza na Rostam na habari yake ya kufoji, ya mtikila baadae, tufocus theme ya post
 
Za mwizi 40......Mtikila aliishi na kula mjini kwa style hii ya blackmailing kwa muda mrefu sana,na siasa zake za kugawanya watu kwa kutumia uzawa/uzalendo/udini watu walizishtukia zamani sana la sivyo leo tungekuwa tunapigana wenyewe kwa wenyewe,i'm glad hili tapeli wamelianika wazi sasa!
 
mtikila ampeleke rostam kuhusu kufoji, na rostam amshitaki mtikila kwa kumwita mu-iran!

mpaka sasa sijaona ndani sawa sawa kwenye hii game wanayoicheza hawa watu........ila nipo macho nasubiri....yatazuka mengi
 
Kwanza cha msingi tungenza na Rostam na habari yake ya kufoji, ya mtikila baadae, tufocus theme ya post

...pesa si amechukua? Yes, nafikiri hakuna ushahidi zaidi ya huo...hayo mambo ya forgery receipt ni spin tuu na hakuna mwenye akili atasikiliza huo upuuzi,kibaya zaidi inawezekana alichukua kwa jina la kanisa kumbe ni zake!
 
Kitendo cha Rostam Kugushi stakabadhi ya malipo aliyoyafanya kwa mchungaji Mtikila akiwa katika harakati za kujisafisha ni jambo baya na ni mbinu chafu za kifisadi.

Ikiwa ameweza kuforge stakabadhi tu ili kuhalalisha kile anacjhokotaka vipi kuhusu mambo mengine mazito.

Kauli ya mtikila tusiibeze na kutoifanyia kazi. "Rostam ameghushi stakabadhi"

Kama Mtikila ashakubali alikopeshwa Tsh3million na RA, kuwepo au kutokuwepo kwa stakabadhi za kufoji kutasaidia nini? Mtikila admitted that he got money from RA, what is the the use for us to start urguing about receipts? WE do not need any authenticity of receipts as long as Mr. Mtikila has admitted getting money from Mr. Rostam Aziz.
 
Mchungaji afadhali akae kimya tuu, huyu jamaa anadai yeye na RA ni marafiki wa siku nyingi, sasa labda hizi million tatu ni zile zilizo kwenye payment voucher pekee, labda kuna zilizo tolewa na RA kwenda kwa mchungaji bila maandishi, kama alichukua million tatu kwa maandishi na kwa mkopo inatia shaka kama hajawahi kuchua nyingine bila maandishi, huyu bwana mchungaji miaka mitano sita iliyopita aliingia ofisini kwetu hapa mitaa ya posta mpya akaanza kumuomba accountant wetu mwenya asili ya kihindi kama RA kiasi cha shiling 20,000 anunulie airtime ya mobile phone yake, accountant wetu alikataa akamwambia hakuna fungu lolote atakalotoa hiyo sh 20,000 kila pesa inayotoka nje lazima iwe accountable, mchungaji alikasirika sana nakuanza kuongea manenoi kama " na ngojeni nichukue nchi nyie magabacholi, watu wenye echunguy na nchii hamuwaoni" accountant akaona sasa hii imekuwa tabu, ikabidi ampatie sh 10,000 kutoka mfukoni kwake, and mind you mchumgaji alikuwa hafahamiani na mtu yeyote pale ofisini...sasa itakuwa swahiba wake rostam, nchungaji kama na wewe unahudhuria jamvi hili la JF nakushauri ukae kimya au utoe ushahidi dume dhidi ya swahiba wako RA
 
....watu walikuwa hawajui wanadeal na mwehu pale,mungu wangu yaani huyu ndio angekuwa raisi nafikiri Amin angeonekana malaika!
 
Kuhusu makanisa mimi nilishasema hapa, na points nyingi anazo raise ni muhimu.With churches like these, unaweza kuwalaumu wasiotaka kwenda kanisani?

Tatizo langu ni jinsi anavyo present!

Kwa hiyo lilikuwa jambo jema kwake kuitisha Press Conference Jumapili iliyopita na kujieleza. Japo waandishi hawakumbana kweli kweli kwa maswali mazito kama vile ya kumtaka aeleze ni vipi watu ambao wako karibu na yeye kimahusiano walimtaja katika ripoti ya Kamati ya Dk. Mwakyembe kuwa ana mahusiano na kampuni ya Richmond n.k, mwanga kidogo umepatikana.

Mbwambo anawatosa "waandishi" kwa kutokuuliza maswali magumu kama yeye si muandishi, kwa nini wewe hukuuliza?

Hata hutuambii kwamba ulijitahidi kuuliza lakini hukupewa nafasi, hukuwapo mjini, ulikuwa unaumwa, ulikuwa na majukumu mengine, au ilikuwaje ukashindwa kuwapo kuuliza maswali yako.

Kaandika hivyo, kaona sawa na mhariri kapitia, kachapisha!

Kwa muda mrefu sasa kumekuwepo na tuhuma za ufisadi dhidi ya uongozi wa Usharika huo, na mwezi uliopita tu ulisambazwa waraka wa wanakwaya kwa washarika uliotumwa kwa uongozi wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani ambao uliorodhesha tuhuma mbalimbali za ufisadi unaoendeshwa na uongozi wa Usharika.

Kutuambia tu kuwa kuna tuhuma za ufisadi bila hata ya kutaja in passing tuhuma zinahusisha nini hakutusaidii sana na vile vile kunaweza kushusha credibility yako.Je unazijua tuhuma? Kama unazijua zitaje, kama huzijui usiseme chochote kuhusu tuhuma ambazo huzijui kwani utakuwa more of story za kijiweni than journalistic reporting.

Utasikia Baba Mchungaji akiwahamasisha washarika wake kuleta mavuno kwa kusema: "Leteni kila kitu na tutakibariki kwa jina la Yesu. Leteni mavuno yenu yanayotokana na biashara zenu na tutayabariki. Haijalishi kama pesa zako zinatokana na biashara ya baa au ukahaba. Ukishazileta hapa tunazibariki madhabahuni katika Jina la Yesu, na zinakuwa safi! Bwana Asifiwe!"

Bwana Mbwambo, utasikia? utasikia? usituambie tutakachosikia kwani unaweza kukaa chini na kutuambia habari kedekede "tutakazosikia". Inawezekana kabisa haya mambo yanatendeka, lakini usituambie "utasikia".Tuambie nimeenda kanisa fulani, nikamsikia mchungaji fulani akiwahimiza watu walete mavuno ya ukahaba kanisani. Hii ndiyo tofauti kati ya journalism na hekaya, the blatant accusation, even if accurate in some cases, blankets all people of the cloth, some fairly some unfairly like the proverbial "mtego wa panya".Hatutaki hili, tunaamini katika fairness.

Andika vitu vilivyo fair, kama huwezi acha kuandika kabisa.

Nasikia katika kanisa moja mtuhumiwa wa ujambazi naye ni mzee wa kanisa kwa kisingizio kuwa "ameokoka", lakini inadaiwa bado hajaacha shughuli yake hiyo ya zamani.

Nasikia? Nasikia!

Yaani Mbwambo ndiyo umeenda this low kutuletea mambo ya "kusikia".Hujaweza hata kutumia euphemism zenu mnazotumia mnapokuwa hamna source "vyanzo vyetu vya habari vya kuaminika" umesettle na maneno ya kusikia? Ulihakikisha hayo maneno ya kusikia au unaleta gossip kwenye habari?
 
Kama Bush vs OSAMA vile wamewaumiza wengi mwisho ni wao wawili sasa.

Lakini RA asijepia akafikiri Mchungaji hajui hafanyalo unless wote wawili wanaigiza kwenye macho ya watanzania.

Kwa kifupi inawezekana wamepanga kutupotezea muda.
 
Kuhusu makanisa mimi nilishasema hapa,

With churches like these, unaweza kuwalaumu wasiotaka kwenda kanisani?

Mbwambo anawatosa "waandishi" kwa kutokuuliza maswali magumu kama yeye si muandishi, kwa nini wewe hukuuliza?

Hata hutuambii kwamba ulijitahidi kuuliza lakini hukupewa nafasi, hukuwapo mjini, ulikuwa unaumwa, ulikuwa na majukumu mengine,
au ilikuwaje ukashindwa kuwapo kuuliza maswali yako.

Kaandika hivyo, kaona sawa na mhariri kapitia, kachapisha!

Kutuambia tu kuwa kuna tuhuma za ufisadi bila hata ya kutaja in passing tuhuma zinahusisha nini hakutusaidii sana na vile vile kunaweza kushusha credibility yako.Je unazijua tuhuma? Kama unazijua zitaje, kama huzijui usiseme chochote kuhusu tuhuma ambazo huzijui kwani utakuwa more of story za kijiweni than journalistic reporting.

Kila mara mimi huwa nasema kuwa ni rahisi sana kutupia lawama wengine kuliko kuwajibika wewe mwenyewe binafsi. Sasa labda yeye siku hizi sio mwandishi lakini kwa jinsi alivyowakosoa ni kama vile yeye yuko kwenye fani ingine kabisa.....mmmhhhh....binadamu ndivyo tulivyo.
 
Kesi ya Mtikila dhidi ya mwanahalisi ni namba 55.
Kesi ya Rostam dhidi ya Mwanahalisi ni namba 54.
Kesi ya Mtikila dhidi ya Tanzania Daima ni namba 57.

Kesi hizi zimefunguliwa mwaka huu mwezi April ,kumbuka huyu mchungaji alipewa fedha muda na siku hizo hizo.

Nawatakia tafakuri ya kina.

1+1=2

Saa ya mafisadi kuumbuka ni sasa: Lowasa -down, Kalamagi -down, Msabaha -down, Mzee wa tujisenti-down, Mtikila-down, --Wataendelea kumbuana kweli kweli mafisadi hawa.

Msishangae kuwa atakayefuata anaweza kuwa ni mtu mzito sana hasa iwapo serikali itamwekea presha Mheshimiwa Aziz kuhusiana na skendo zinazomzunguka za Kagoda, Richmond na Dowans n.k.

Ngoja nifandushe Kiigereza kidogo mafisadi hawa (teh!! teh!! teh!!)

"Let them say, our eyes ...= ...Waache waseme, yetu macho"

"We didn't depend Mtikila to be this ...= ...hatukutegemea Mtikila kuwa hivi"
 
Hivi kwanini kama kuna mtu asiwe anaoomba maswali hapa JF ili tuwape waulize?I would like to know shilling ngapi walilipwa
 
kaaz kweli kweli
lakini si alipokea hela??? haijalishi kakopa au kamfisadisha ila cha msingi kapokea mijisenti and he's at it... let him face it

...'baniani mbaya kiatu chake dawa!',

...nikikumbuka wananchi waliojaa mori baada ya Mheshimiwa kabisa Mchungaji Christipher Mtikila kutamka hadharani ubaya wa Magabacholi, kumbe ni katika njia za 'kula na vipofu'

'Do what i say, but don't do what i do!"~ songs-of-songs

...wanasiasa wetu ndivyo walivyo!
 
hii nchi inavyoendeshwa ni kama vile story ya tamthilia, coz ukitoka part hii unakwenda hii, ukitoka hii unnakwenda ile, mara EPA mara richmond, mala balali, mala uchawi bungeni, mala wangwe mala rostam na mtikiila...mwisho wa siku wadanganyika wanashindwa waamini lipi waache lipi coz wameshabuluzwa vya kutosha na hawajui hata waanzie wapi

Ni suspence,suspence..mwishowe tragedy!
 
...'baniani mbaya kiatu chake dawa!',

...nikikumbuka wananchi waliojaa mori baada ya Mheshimiwa kabisa Mchungaji Christipher Mtikila kutamka hadharani ubaya wa Magabacholi, kumbe ni katika njia za 'kula na vipofu'

'Do what i say, but don't do what i do!"~ songs-of-songs

...wanasiasa wetu ndivyo walivyo!

nakumbuka mtikila aliwatembeza watu maandamano mafupi yaliyoanzia jangwani na kuishia dar tech coz pale palikuwa na FFU wa kutosha ambao waliwafturu watanganyika na kila mmoja kutokomea pasipojulikana...
ukiuliza nini eti mtikila kawatuma wakawatimue wahindi ambao yeye aliwabatiza jina magabacholi duh

ila cha kushangaza yeye hakuandamana, na ndio hapo sasa napata picha kuwa huyu jamaa ni CCM ila anakoroga tu wazalendo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom