Rostam aibukia kanisani!

Ingekuwa vema mtikila akatufahamisha hao wengine waliomkopesha maana kwa hali hii, sitashangaa kuona kuwa hata akina Lowassa, Chenge na marehemu Billali wote wanamdai.
 
hivi Mtikila anapata ruzuku, si najua kuwa chama chake hakijasajiliwa rasmi na msajili wa serikali kama chama cha siasa ingawa kipo,au?

Maana nilifikiri wanaopata ruzuku ni wale wenye wabunge tu, au?

Kama ndio hivyo kuwa hana ruzuku, sasa naona atakua na sababu na kisingizio cha kukopa kwa RA.
 
Mtikila ni ndumilakuwili , na kwa hili nitamshukuru Rostam kwa kum-expose huyu bwana . Kwa nini alienda kuomba mkopo kwa Rostam wakati kuna financial institution zinayofanya hizo kazi ? Si huyu Mtikila ndiye aliyeanzisha slogan ya magabachori na jee si huyu Mtikila ambaye amekuwa akidai ya kuwa Rostam ni raia wa Iran , sasa inakuwaje behind the scene ni Mtikila huyu huyu anaenda kuomba mkopo ? Mbaya zaidi anadai ya kuwa Rostam ni rafiki yake.



Pili , Ni lazima tutoe credit pale panapostahili credit ! Katika hili sakata nzima Rostama ameonyesha uwezo wa hali ya juu katika kuchanganua mambo . Sasa nimejua kwa nini huyu mtu watu wengi walidai ya kuwa alimweka Kikwete madarakani . Jamani kama mlisikiliza hotuba yake pale kanisani , huyu bwana anajenga hoja kwa kutumia "pathos" , ametumia watoto wake ili kuweza kuibua hisia , wanasiasa wachache sana wa Tanzania wanajenga hoja kwa staili hii. Lakini zaidi ameweza kujidifferentiate yeye na viongozi wengine wa serikali ambao ni Manungayembe .


Mimi nadhani huyu bwana ni smart , na sababu kubwa ya kumtoa Mtikila kafara ni kusend message kwa wale wote waliochukua mikopo kwake " viongozi " kuwa if you will dare to speak then you must be ready to face the consequence.
 
Hakuna jiwe litakalo baki juu ya jiwe.

Mpinzani aliye safi amfikishe RA mahakamani tuone umahili wa wapinzani. Fatuma litakalotoka huko itakua balaa tupu.
 
hivi Mtikila anapata ruzuku, si najua kuwa chama chake hakijasajiliwa rasmi na msajili wa serikali kama chama cha siasa ingawa kipo,au?

Maana nilifikiri wanaopata ruzuku ni wale wenye wabunge tu, au?
DP ya Mtikila haipati ruzuku yoyote kwa sababu haina Mbunge hata mmoja na haina Diwani hata mmoja. Lakini mimi namwona Mtikila kuwa shujaa: kachukua fedha ya RAI lakini tofauti na Wabongo wengine, "fadhila" hiyo haijamfunga mdomo pale inapobidi kumshughulikia RAI. Kirefu cha RAI ni Rostam Aziz of Iran.
 
Mtikila na Rostam lao moja: Ila kwa sasa Rostam anaweweseka na siku si nyingi wanasiasa na waandishi watakaomgeuka nao atawataja na fedha alizowapa. Jambo la msingi ni kwamba, siku mtikila anakabidhiwa hizo fedha zinaoana na siku Mtikila alipofungua kesi dhidi ya gazeti la Mwanahalisi, na siku alipofungua kesi dhidi ya Mwanahalisi, ndio siku Rostam alifungua kesi dhidi ya Mwanahalisi. Hapo kuna kazi kweli kweli. Lakini kwa CCM wanapaswa kumfukuza Rostam kwa kushirikiana na wapinzani tena kwa kuwafadhili dhidi ya serikali na chama chao

CCM waifukuze bank yao!!! Siyo rahisi, labda enzi za Mwalimu huyu zamani angeshakuwa history ndani ya CCM lakini siku hizi kumejaa mafisadi na walafi ndani ya chama hicho. Hakuna hata mwenye ubavu wa kutoa sauti kwamba fisadi RA afukuzwe chama. Kwanza atakuwa na wasi wasi na yeye 'mikopo' aliyechukua toka kwa fisadi inaweza kuanikwa hadharani.

Nadhani huko CCM sasa hivi wana wasiwasi mkubwa maana wanapita pita kuchukua mabulungutu ya 'mikopo' kwa akina Manji, Jeetu Patel, Vithalani yule wakala wa Rada, ndege ya Rais, magari ya jeshi na helicopters na si ajabu wote hawa wana risiti za wote waliochukua mshiko toka ndani ya CCM na serikali.

Wacha Pinda, Mwanasheria Mkuu Mwanyika na Mkuu wa polisi waseme 'mafisadi ni matajiri wakubwa, wakikamatwa nchi itawaka moto' lakini nchi haitawaka moto bali viongozi walafi na mafisadi ndiyo watawaka moto.
 
Umefuatilia issue ya Mtikila, TIB na wahindi? Nyumba yake ilivyopigwa mnada halafu akarudishiwa kinyemela na wahindi?

What more do you need?

wewe sijiu unaongelea mtikila kunyanganywa nyumba, ama sijui nyumba kuungua moto! hatuko katika sera za gabachori hapa! usiihamishe mada!
 
Suala hapa ni kwamba je, CCM walimtuma Rostam ku deal na Mtikila? Na kama wasimpomhoji, ndipo sasa tutathibitisha tetesi kwamba CCM inawanunua na kuwatumia baadhi ya viongozi wa upinzani. Hapa si suala la kuwa na mahusiano na ushirikiano na wapinzani. Hatukatai, wapinzani kuwa na uhusiano na CCM. Wengi wana mahusiano lakini uhusiano wa Mtikila na Rostam, unatia shaka. Kabla ya Rostam mwenyewe kusema hayo, ungemuuliza ama ingeandikwa, angetishia kushitaki. Leo kasema yeye, tunashindwa kutafakari
 
MAJIBU YA MTIKILA.

“Ni kweli niliomba fedha kwa Rostam kama mkopo, na nikaandika kwa mkono wangu maelezo kwamba nitazirejesha. Nilimueleza kibanda changu pale Mikocheni kilikuwa kimechakaa na kilihitaji marekebisho. Sikwenda kwake kuomba fedha za ujenzi wa kanisa,” alisema Mtikila ambaye alidai alikuwa akijiandaa kumchukulia hatua za kisheria mwanasiasa huyo.” (Gazeti la Tanzania Daima).

**********************************************
“Ni kweli, Rostam ni rafiki yangu sana, tena siku nyingi, lakini alinipa sh 3 milioni kama mkopo, si fedha za kuendeleza kanisa kama anavyosema. Muulizeni kanisa gani, mimi sijengi kanisa wala siendelezi, wapo wafadhili wa kanisa. Ni fedha za mradi wangu na ni mkopo,” alisisitiza Mtikila.

Mtikila alipoulizwa tena katika mahojiano mafupi kwa njia ya simu, kwamba mkopo huo alipaswa kuurejesha kwa muda gani na ni mradi gani hasa aliufanya, alijibu tena: “Ni mradi wangu fulani hivi, muda wa kurejesha mkopo ulipaswa kuwa within two months (ndani ya mienzi miwili)”,
Katika mahojiano hayo, Mtikila alipoulizwa zaidi, kwamba hadi jana miezi miwili ilipita vipi hakuweza kurejesha fedha hizo, alijibu:
“Ahaa ni kana kwamba mkopo ni mkopo tu, hata serikali bado inadaiwa na wafadhili na haijalipa hadi sasa, ila mimi nitamlipa ndani ya wiki moja hadi mbili kuanzia sasa,”

Mtikila alipoulizwa zaidi, kwamba hata kama ni mkopo, vipi alikopa fedha kwa mtu ambaye amekuwa akimuita fisadi na mwenye kumiliki fedha chafu kwa kuwa pia alipinga Rostam kutoa fedha kwa KKKT, alijibu:
“Ni kana kwamba zile fedha si chafu ni za nchi yetu, ni za serikali yetu sema tu matumizi yake na amezipataje” Gazeti la Mwananchi..
 
Mtikila kweli umetuangusha Mchungaji wewe. kumbe na wewe ulipewa tena ulipewa tarehe ambazo mambo ya UFISADI ndo yalikuwa yanaunguruma sana hapa nchini. eti mkopo kwa nini hukwenda benki kukopa? Wachungaji wetu Mhhhhh


Niliposema viongozi wetu wa dini wanatumiwa na mafisadi watu hawakuniamini. Hata hawa wa kkkt wanaojidai kumkana mwezeshaji wao rostam hawana lolote, ukiwachunguza vizuri utakuta nao wako sawa na mwenzao mtikila. Kazi yao kubwa ni kuchukua vijisenti vya mafisadi ambayo yamegeuka kuwa miungu wao.
 
Huyo ndiye Mtikila ule upande mwingine wa PRIVATE. Sema tu RA sio MSTAARABU, hakupaswa kulisema hili. Tuendelee kumbana tu, anayo mengi mengine ya akina EL, JK,...
 
Kitendo cha Rostam Kugushi stakabadhi ya malipo aliyoyafanya kwa mchungaji Mtikila akiwa katika harakati za kujisafisha ni jambo baya na ni mbinu chafu za kifisadi.

Ikiwa ameweza kuforge stakabadhi tu ili kuhalalisha kile anacjhokotaka vipi kuhusu mambo mengine mazito.

Kauli ya mtikila tusiibeze na kutoifanyia kazi. "Rostam ameghushi stakabadhi"
 
mtikila ni hodari wa kupeleka watu mahakamani. iwapo kweli rostam ame ghushi stakbadhi hiyo mwache ampandishe kizimbani.....kwa sababu hapa naona wanasiasa wanataka wananchi tuuchague kambi BLINDLY bila ya kupewa ukweli wa jambo lenyewe
 
kaaz kweli kweli
lakini si alipokea hela??? haijalishi kakopa au kamfisadisha ila cha msingi kapokea mijisenti and he's at it... let him face it
 
Saga ya Rostam na Mtikila ni vumbi la jangwanai mwachoni mwetu ili tusione mbele. Fact zilizopo hapa ni kuwa Rostam ni fisadi, na Mtikila ni mlamakombo ya fisadi. Kati ya wanaisasa wote nchini, sikutegema kuwa Mtikila angeweza kwenda kuomba hela kwa Rostam katika mazingira haya ya Richmond ambayo imeanzna tangu mwaka 2006; halafu hela zenyewe eti ni shillingi millioni tatu tu jamani! Dunia yetu hii ikoje? Inawezekana kuwa Mtikila alitegeshewa hela hizo, naye akajiingiza bila kujua maana yake, na sasa ameumbuka na anaona aibu kusema ukweli kuwa alinaswa; amekuwa kama changudoa.

Ukweli ni kuwa sasa hivi Rostam anatafuta namna ya kuzima vuiguvugu la Richmond kwa kutumia hela hizo hizo. Mkataba ule ulimwingiza zaidi ya shilling billion 100, ukiachilia mbali zile za EPA. Kwa hiyo kutoa milion tatu kwa Mtikila na nusu milioni kwa KKKT na nusu milioni nyingine msikitini ni jambo dogo sana. Jana nilipokuwa naangalia movie za Mr. Bean na wanangu, tulicheka sana wakati Mr Bean alipokuwa ana-trespass akabwekewa na mbwa, halafu yeye akaamua kumnyamazisha mbwa yule kwa kumtupia mfupa usiokuwa na mnofu wowote. Hapa Rostam ametrespass, na Mtikila alitaka kubweka akatupiwa mfupa. Makubwa hayo.


Funzo kubwa hapa tunalolipata ni kwamba tunalazimika kuwa makini sana na wanasiasa wetu. Mtikila na Mzee Mapesa waliwahi kunyang'anywa nyumba zao ila wakafadhiliwa na CCM wasizipoteze. Wanasiasa wa aina hii tusiwaamini kabisa kwani wanaloongea ni kinyume na wanalofanya. Mtikila ameonyesha kabisa kuwa ukimpa hazina yetu hatakuwa na tofauti yoyote na hawa hawa mafisadi waliotumaliza. By extrapolation, hata mzee Mapesa naye nilishamtoa kwenye list ya wanasiasa wakweli.
 
Kugushi...

Duh. Huu mjadala mi sitaki hata usikia maana inaonekana ambavyo huyu jamaa anafanikiwa twist minds za watu... Mtikila anawedha kuwa amejifedheesha na kuwasikitisha sana wale ambao walikuwa wafuasi wake, lakini kwa kiasi kikubwa Rostam nae kafanikiwa kugeuza mind za watu na sasa tunakaa tunabishana tu husiana na matendo ya Mtikila badala ya issue za ufisadi.

RA anaanza kufanikiwa katika kampeni zake za kujisafisha. He is creating a diversion and JF tuunamwangalia katika hilo.
 
Mtikila naye anataka kucheza "Both sides of the fence" Yeye kadakishwa mijisenti, kuona jamaa anaweza kumsema hadharani, huyoooo anajiwahisha kwenye vyombo vya habari kudai saini yake imegushiwa. Na yeye ni hodari wa mahakama; tumuone aende huko akalalamike. Na ikidhibitishwa kuwa saini yake imegushiwa, nitakuwa wa kwanza kuja hapa kumuomba samahani.
Mchanga wa macho tu huo!!
 
Japo kweli Mtikila hapa kakamatika, na kupunguzwa kasi ya kuwakemea mafisadi, lakini bado hili haliondoi hoja ya nguvu kwamba:
Rostam hajawatendea haki wana KKT kutumia mimbali kujisafisha! Kumualika kwao si kosa hata kidogo, kosa ni ujumbe alio utoa hauhusiani kabisa na kumtukuza Mungu wala kuliendeleza kanisa. na hasa hili ndo chukizo kwetu.
 
hii nchi inavyoendeshwa ni kama vile story ya tamthilia, coz ukitoka part hii unakwenda hii, ukitoka hii unnakwenda ile, mara EPA mara richmond, mala balali, mala uchawi bungeni, mala wangwe mala rostam na mtikiila...mwisho wa siku wadanganyika wanashindwa waamini lipi waache lipi coz wameshabuluzwa vya kutosha na hawajui hata waanzie wapi
 
hilo kanisa lilifikiri nini mpaka likamualika hapo mwanzo? au ndio kuganga njaa kwa baadhi ya waumini?

viongozi wetu si waandilifu lakini na sisi wananchi wa kawaida tamaa ya pesa inatuongoza kuelekea kubaya.

mtu kama rostam si wa kumualika nyumbani kwako seuze kwenye nyumba ya mungu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom