Rostam aibukia kanisani!

Rostam aibukia kanisani!

Jamani kwakweli huyu Mch.Christopher Mtikila ananisikitisha sana. Sidhani kama ana dhamira ya kweli na nchi hii.Inavyoonekana ni mtu ambaye ana njaa zake na anatumia jukwaa la kisiasa kujipatia ridhiki yake ya kila siku.Zamani nilimuona mwanamapinduzi lakini matukio mengi ya hivi karibuni yamenifungua macho kwamba jamaa si lolote wala si chochote.Hawezi kukopeshwa na RA kama si mtu anayetumiwa kwaajili ya kufunika kombe kwenye kashfa nyingi zinazomhusu Mh.RA. Mtikila umeniudhi sana sina ninachoweza kukufanya!
 
He is al oser and he is losing big time.Kama aliomba fedha za watu na akajifanya domokaya its pay back time.
Every dog has its day.
 
Mtikila kweli umetuangusha Mchungaji wewe. kumbe na wewe ulipewa tena ulipewa tarehe ambazo mambo ya UFISADI ndo yalikuwa yanaunguruma sana hapa nchini. eti mkopo kwa nini hukwenda benki kukopa? Wachungaji wetu Mhhhhh

Benki kukopa Ukiritimba na riba ni kubwa mno!!! Kaenda pata 'Soft Loan' aaah kwa raha zake. Sasa wakati mambo ya Ufisadi yananguruma si nae alitaka azifaidi hizo pesa...
 
tatizo la umaskini linakandamiza sanaa demokrasia kuchipua kwa kasi inayofaa.
huyu mtikila yeye kwa sasa anatumia umaarufu wake kuchukua fedha kwa RA.
na RA lazima amtumie kwa malengo anayoyajua. tatizo mchungaji haaminiki na hahitaji rafiki wa kudumu ni malengo ya muda tuu
tumsikie porojo zake pia ila magazeti nayo yendelee kuuza maana hyo ndo story. mambo ya mwanjelwa, mwanhunzi, maswa wala media hawana muda nayooooo...
Mkate, mkaa, unga wa sembe bei juuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu...hamna uchambuzi kutwa ufisadiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii issues..
 
Mtikila hajatuangusha....kama kuna dume mpaka sasa kwenye hili game ni Mtikila. Yeye amemuendea Rostam Aziz kabla ya ripoti ya Dr Mwakyembe kutoka, amekopa/amepewa Mil 3. Lakini mara baada ya ripoti ya Rostam Aziz kutoka Mtikila hakumuonea aibu kwa sababu eti alishawahi kumkopa/kumuomba Mil 3 huko nyuma. Mtikila alipogundua kuwa Rostam Aziz ni Nyani, hakumuangalia usoni; aibu wala woga Mtikila akaanza kupambana naye moja kwa moja...

Rostam mpaka sasa ametuthibitishia kuwa yeye ni FISADI kwa kugawa/kutoa/kukopesha pesa kwa wanasiasa/mashirika ya dini na wanajamii wengine huku akiwa na nia ya kuonewa aibu akiwa anatuibia Watanzania.

Bravo Mtikila, pambana nao hao kama walivyo.

Hapendwi mtu, Taifa mbele.
 
Wether alikopa before or after report ya Dr Mwakyembe still does not justify what he is going to say at the Travertine Hotel.RA was a known fisadi siku nyingi sasa kama yeye kamjua RA juzi baada ya hiyo report sasa that is what he will have to answer to the Tanzanians.
 
duh maskin mtikila.wenzie wanan'gata alafu wanapuliza,sasa yeye anapuliza alafu anan'gata
 
Mtikila hajatuangusha....kama kuna dume mpaka sasa kwenye hili game ni Mtikila. Yeye amemuendea Rostam Aziz kabla ya ripoti ya Dr Mwakyembe kutoka, amekopa/amepewa Mil 3. Lakini mara baada ya ripoti ya Rostam Aziz kutoka Mtikila hakumuonea aibu kwa sababu eti alishawahi kumkopa/kumuomba Mil 3 huko nyuma. Mtikila alipogundua kuwa Rostam Aziz ni Nyani, hakumuangalia usoni; aibu wala woga Mtikila akaanza kupambana naye moja kwa moja...

Rostam mpaka sasa ametuthibitishia kuwa yeye ni FISADI kwa kugawa/kutoa/kukopesha pesa kwa wanasiasa/mashirika ya dini na wanajamii wengine huku akiwa na nia ya kuonewa aibu akiwa anatuibia Watanzania.

Bravo Mtikila, pambana nao hao kama walivyo.

Hapendwi mtu, Taifa mbele.
Yebo Yebo tunashukuru kwa uchambuzi wako huru.
 
Mtikila namfananisha na mtu aliyeweka punje za mahindi ya moto kinywani. Huku akihangaika kuyapoza ndani kwa ndani mkidhani anayatema lakini ghafla nakuta kanyamaza kumbe kayameza.
 
mtikila Mchungaji Na Hao Kondoo Wa Wanaochungwa Nae Huyu Mchunga Ndio Kazi Yake Kuchota Huku Nakule . Wakati Wa Sakata La Manji Na Mengi Usiku Tukimwona Haideri Plaza Akishuka Kila Jioni Sasa Hapo Ipo Ofice Ya Nani Kazi Kwenu Lakini Nilikutana Nae Akitoka Huko Kama Paka Mwizi . Asubuhi Tayari Yupo Maelezo Ku Ropoka .... Domo Kaya Kweli . Likaja Sakata La Kadhi Kaitwa Atumike Tena Usiku Usiku Huyo Avinjari Ndani Kwa Wachungaji Wenziwe Pale Kivukoni Na Baadae Kama Ada Lazima Apite Haideri Plaza Kwa Mangi Meza Akajaze Chaji Za Kuropoka . Kwa Hio Kuchukua Tena Kwa Rostam Si Ugeni Ndio Mjini Bongo Utaishi Vipi? Mabo Ya Bongo Hayo , Kazi Kwenu Wachunwaji Wa Mtikila
 
Wenye kuanza kumlaumu Mtikila na huku wakidhani yeye ndiye mwenye makosa na si RA...Basi hapo ni sawa na kumlaumu mtoto aliyepewa sumu na huku ukimwacha aliyetoa sumu kwa kudai kuwa mtoto ni mjinga na ni kwanini alipokea sumu na ama kunyeshwa.

Huyu mtu (ROSTAM) nayeye alikuwa na malengo.

Tunajuwa Mtikila ni njaa ilimsumbuwa...Lakini hilo halimfanyi kuwa Fisadi.

FISADI HALIN NJAA...NA MTIKILA NI SURVIVOR...KWANI MWALIMU ALIPEWA PESA ZA KAMPENI NA NANI?
ANDY CHANDE AMBAYE NI MAFIOSO NI RAFIKI WA BABA WA TAIFA...!

Tumwache aplay part yake na sisi tuplay yetu kwani hata hao wanaojidai kuwa hawakupokea chochote na wale wenye kujidai hawamwogopi RA...HIVI RAIS AMUOGOPE HALAFU MNAMWACHA NA KUMPARAMIA MTIKILA!?

JF HAITAKUBALI.

Esp mimi sitakubali.

Just kama ilivyokuwa kwa Mwakyembe...Tutapigania hoja na RA akajibu hoja bungeni na mahakamani.

Na kama na yeye hataki siasa...Basi na aseme ni ki vipi hizo milioni tatu zake zinahusiana na mabilioni ya dola alizokwapuwa pamoja na utajiri wetu.

Na kama Mtikila ana makosa...Basi sijui ni rais gani atakayekuwa hana makosa kwenye historia yetu na kama RA ana uwezo wa kumfungulia mashtaka Mtikila basi na afanye hivyo kwani sisi pia tunamfungulia mashataka.

Hatuaki siasa tena!

Na nyie watanzania mnaofuatilia haya mambo hapa jf mjuwe kuwa sasa watanzania wote duniani wameunganishwa na hakuna ukiritimba kama wa mwalimu aliyezuia watu kwenda nje ya nchi.

Wakati huu kuna fikra a kimapinduzi na kimaendeleo.

Fikra MPYA ambazo Tanzania haijawahi kuwa nazo.Viongozi wetu wana fikra za kizamani na sasa ni wakati wa CHANGE.

Tunataka UHURU WETU...TUNATAKA MALI ZETU ZITUNUFAISHE SISI NA WATOTO WETU PAMOJA NA VIZAZI VIJAVYO!

Ni aibu kubwa kwa sisi watanzania kuendelea kuwa omba omba hadi nchini mwetu.

Tunaomba si tu kwa waungu na waasia na wahindi..Bali hata WAARABU na wanasiasa wetu nao wamegeuka omba omba wakiongozwa na JK na sasa RA amekuwa mwiba kwao.

Mtikila afanye kazi yake na Mungu atamlipa.
 
Mtikila kukopa pesa kwa Rostam sioni kama ni tatizo kwavile walikuwa ni marafiki, na ni jambo la kawaida sana hapa kwetu Tanzania kwa mtu asiye fisadi kukopa pesa ilikukamilisha mambo kadhaa kwa maisha yake, as mishahara haiendani na ugumu wa maisha. Tatizo linakuja kwa Rostam ambaye alitegemea kuwa kwavile amemkopa pesa rafikiye basi huyo rafikiye awe kibaraka wake, kamwe asifungue mdomo juu yake which was wrong on Mtikila's side, yeye anatimiza wajibu kama watanzania wengine wenye mapenzi mema na Tanzania kukemea ufisadi, hajali ni nani na amemfanyia nini,,,kitu ambacho naona ni sahihi kabisa, sisi sote (ambao si mafisadi) kuna namna moja au nyingine tumeweza omba msaada kwa wenye navyo na tumesaidiwa, je nao wangetugeuka na kutangaza hadharani tungeendelea kujilaumu au tungemuona huyo alietugeuka kuwa ni mnafiki tu.
Rostam amedhihirishia umma kwamba yeye ni fisadi No1. kwanini hakujibu tuhuma za ufisadi akaingia katika kutapatapa ooh, naishi na mke wangu, nafanya biashara tangu 1700's hilo sio alilotakiwa kueleza!!! Kama ni biashahara halali then Tanzania ingekuwa kati ya nchi tajiri ati, tangu enzi hizo mtu anapata mipesa tu.
and last, lawama zote ziende kwa vyombo vya sheria hapa Tz, mtu kama ni fisadi ashitakiwe, afungwe! mambo ya kuwaacha mitaani wajitutumue na kuita waandishi kushuka nao verse za taarabu sio sahihi, na kuanzia sasa tutegemee press conference nyingi tu, ndio kumekucha sasa.
 
Wether alikopa before or after report ya Dr Mwakyembe still does not justify what he is going to say at the Travertine Hotel.RA was a known fisadi siku nyingi sasa kama yeye kamjua RA juzi baada ya hiyo report sasa that is what he will have to answer to the Tanzanians.

Mtikila atajibu vipi wakati hao mafisadi wenyewe bado wanadai ni wasafi na hawajakubali kwamba wao ni mafisadi na vyombo vya sheria vimeshindw kuwachukulia hatua kama mafisadi na wahujumu uchumi?
 
Kama watanzania wote wangelikuwa kama Mtikila basi tusingelikuwa na matatizo. Watanzania ukifika uchaguzi wengine wanapewa kanga, vitenge, bia nk. Wakishapewa vitu hivyo wao ikifika wakati wa uchaguzi wanauza uhuru wao kwa sababu wamepewa rushwa.

Sasa Mtikila anatuonyesha kuwa hata mkipokea vitu hivyo Mtu ambaye hafai endelea kumuona hafai, mbabaishaji endelea kumuona ni mbambaishaji, fisadi endelea kumuita fisadi.

Kwa hiyo FISADI Rostamu nafikiri anaanza kufika pazuri kama alitegemea kutoa hongo kutamsaidia naona sasa ataishia kutuonyesha jinsi anavyofanya kwa baadhi ya watendaji na viongozi wetu katika kuhakikisha anahujumu taifa letu. Fisadi lazima aitwe fisadi na lazima abebe mzigo wake.
 
Na kama ni kukopa na kuomba omba kama mataahira ni mwalimu na marais wengine wote waliopita wanafacilitate.

Kwa kusema na kutuambia sisi pamoja na kina Mtikila tuimbe pambio kuwa sisi ni masikini na tusubiri tufe ili tuende kwa Mungu tunayemwabudu na huku mafisadi waki ishi raha mustarehe na wakiomba Mungu hata waishi milele.

Nasema hivi..Tabia ya u omba omba na kukopa kopa ni ya asili ya Mtanzania amabayo sisi kizazi kipya tunaikataa kwa nguvu zote na ndio maana tunasema hatutaki tena misaada na Mtikila kashajifunza na inataiwa ashirikiane na wazalendo wengine wanaokiri kuwa sisi ni MATAJIRI NA HIVYO HATUTAKI TENA KUWA OMBA OMBA WALA KOPA KOPA.

Na kama ni kweli benki za MAKABURU ZINA RIBA KUBWA NA YA KUPITA KIASI THEN KOSA SI LA MTIKILA!

Kama kweli madini na mali zetu zingekuwa vinatunufaisha basi hata kusingekuwa na mafisadi kama hawa kina RA na wenzake na pia hata kanisa la kinondoni lisingekosa milioni 5..Na kwaya isingeweza kukosa milioni mbili kama mchungaji mwenyewe pia si FISADI.

Kama kusingekuwa na UFISADI...Basi mtu kama Mtikila milioni tatu si lazime angeenda kwa Roastama!

Ni kivipi uende kwa mwarabu kuomba pesa zako mwenye ewe MTANZANIA!?

MTIKILA NA WEWE UJIFUNZE NA KAMA UKIGEUKA NA SISI TUTAKUSHUGHULIKIA!

Sisi wengine ni kizazi kinacho bridge kati ya awamu zote nne.

Tunajuwa historia ya awamu zote...Tunajuwa hata histora yako wewe Mtikila...Lakini huu si wakati wa nyuma kwani wengine tumejitolea muhanga kabisa na nina imani tutaingia kwenye Historia kama si ya Tanzania na Afrika..Basi ni ya dunia!

Tumeshuhudia mambo ya kina Lamwai,Marando na Kaburu...Tumegunduwa kuwa na wao pia ni MAFISADI KWANI WASINGEMFANYIA MREMA MBAYA HATA HAYA YASINGETOKEA!

Ufisadi ulioko na wapinzani pia ni wa kulaumu!

Na kama wasipokuja pamoja wakati huu na wao kusuburia wachafuane wenyewe kwa wenyewe kwasababu ya tamaa za madaraka..Then nyie mtaangukia grupu moja na mafisadi...Na kama kweli vurugu za wenyewe kwa wenyewe zikianza...Basi wapinzani ndio walimwe risasi kabla hata ya ccm kwani UKUWADI NI MBAYA ZAIDI KULIKO MKUWADIWA!
 
Mtikila huyu ndiye huwa anatumiwa na CCM kuwagawa wao kwa wao na ndiyo kazi yake,alipewa pesa nyingi sana na kina Rostam kumbomoa Sumaye ..Pesa yenyewe kapew Mwezi wa nne tu..sasa lazima kama tunataka Mabadiliko inabidi wapinzani wajipange kweli na watoe magugu yote.Ole wenu CHADEMA..Ngurumo alishwaandikia toka Jumapili na sitaki kurudia tena..

My TAKE
Baada ya wiki kupita na kumezuka matukio mengi ambayo ni ya hatari sana,angalia kuanguka kwa Wangwe,kusakamwa kwa Rostam,Waziri mkuu kusema Zanzibar si nchi,Spika kutangaza hakuna Uchawi Bungeni,Rostam kujibu tuhuma..utaona kuna mambo ambayo yanatumika kutugawa

1.Ukabila
2.Udini
3.Ubaguzi

Tunakoelekea mie sijui ila ni kubaya sana hii inafanywa ili kujenga Chuki kati yetu na mwisho wake ni kuua Upinzani kabisa,Alchoongea Rostam kaandikiwa na kikundi cha watu na siyo peke yake.Kavunja Kanuni za Bunge na hatafanywa chchote sababu alithubutu kuzungumzia Suala la RDC wakati Mjadala ulishafungwa Bungeni..

Ila ukiangalia ni kwanini alifanya hivi?kafanya hivi baada ya kuona Spika amekosea kwa kulidanganya Bunge at the first Place wakati akielezea kuna watu wawili walionekana Katika ukumbi wa Bunge Usiku..Spade a spade...Siasa za kuviziana ndizo zinatawala...

Nasita kuendelea kuwapinga MAFISADI.sijui nijiunge nao?...nina mpango mmoja na naomba nijiunge nanyi
 
......kama aligundua Rostam ni fisadi mbona haurudisha hizo pesa? ni njaa tuu hakuna lolote hapo,na hizi siasa za chuki kwa wananchi wengine na tabia zake za ku attack wengine sio raia kuna watu wanashangilia lakini ni very dangerous,bila Nyerere kumponda huyu jamaa angeleta balaa huyu.
 
Kama serikali yetu inaomba omba na kukopa kopa..Mtikila ana kosa gani?

Kama ni kweli kuwa bejeti yetu karibia yote inawategemea WAARABU NA WAZUNGU BILA KUSAHAHU WAASIA...THEN MTIKILA YEYE NI NANI WA KUANDAMWA?

Si kila mtu anajuwa UMASIKINI WETU UMESABISHWA NA VIONGOZI WETU AKIWEMO ROSTAM?!

Je hakuna BENKI ZA KIFISADI?

Ukienda kuchukuwa mkopo huko na wewe FISADI?

Vipi kuhusu yule LAST HOPE ALIYEPOZA KADI YAKE NA BENKI IKAMWAMBIA AENDE POLISI KABLA HAWAJAIFUNGA AKAUNTI YAKE?

Uhuru ni wa MAKABURU NA WAO NDIO WANAENDESHA NCHI KWA KUPITIA MAKAMPUNI YAO NA TUWAACHE KINA MTIKILA WAPIGANE!

Vipi kuhusu wanaotumia VODACOM ya ROSTAM?

Na wao wamehongwa?

ACCHENI UTANI BANA!

Ila na wewe MTIKILA USIDHANI KUWA HIZI NI SIASA ZA MIAKA YA TISINI HIVYO UWE MAKINI KWANI WAKATI HUU NI THE MOST DEFINING MOMENT IN THE HISTORY OF OUR COUNTRY NA TRUST ME UKITELEZA THIS TIME UMEKWENDA MOJA KWA MOJA!
 
Mtikila na Rostam lao moja: Ila kwa sasa Rostam anaweweseka na siku si nyingi wanasiasa na waandishi watakaomgeuka nao atawataja na fedha alizowapa. Jambo la msingi ni kwamba, siku mtikila anakabidhiwa hizo fedha zinaoana na siku Mtikila alipofungua kesi dhidi ya gazeti la Mwanahalisi, na siku alipofungua kesi dhidi ya Mwanahalisi, ndio siku Rostam alifungua kesi dhidi ya Mwanahalisi. Hapo kuna kazi kweli kweli. Lakini kwa CCM wanapaswa kumfukuza Rostam kwa kushirikiana na wapinzani tena kwa kuwafadhili dhidi ya serikali na chama chao
 
......kama aligundua Rostam ni fisadi mbona haurudisha hizo pesa? ni njaa tuu hakuna lolote hapo,na hizi siasa za chuki kwa wananchi wengine na tabia zake za ku attack wengine sio raia kuna watu wanashangilia lakini ni very dangerous,bila Nyerere kumponda huyu jamaa angeleta balaa huyu.

Habari za watutsi kuvamia jeshi na financiali institutions kama BOT we umezichukulia vipi?
Kwamba hata mipaka aliyoweka mwalimu si afadhali hata ile ya mkoloni?
Kusema unapenda demokrasia na kuyachukia baadhi ya makabila na kuwakumbatia wageni ndio USHUJAA HUO?
Kusema Mtikila na Mrema walikuwa hawana akili timamu bali MKAPA NI USHUJAA?
Kwenye debate kama hizi....NO WAY!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom