Rostam aibukia kanisani!

Rostam aibukia kanisani!

...Mtikila tumemshtukia anatumiwa na CCM na siasa zake za kibaguzi na jazba hazina nafasi kwa wananchi walio wengi,ila tunashukuru mchango wake wa kuishtaki serikali katika mambo mengi ambayo naona wengi tulikuwa hatujui

Koba,

Unaweza kutufafanulia, je anatumiwa na CCM vipi? Kuchangiwa na Rostam hizo pesa tayari
ni kutumiwa na CCM?

Kweli Mtikila atakubali kwenda kote huko jela akitetea haki ya Mtanganyika ili atumiwe na CCM?

Nafikiri hili neno la kumwambia kila mwanasiasa ambaye hatukubali naye kwamba anatumiwa na CCM, limechuja na limepitwa na wakati.

Kuna wanasiasa kibao tunaowashabikia hapa, wanapigana vikumbo kila siku na viongozi wa CCM lakini hatusemi badala yake tunamshambulia mtu kama Mtikila ambaye kwa kweli kachangia sana kwenye mapambano ya kudai haki ya Mtanganyika.
 
Mtikila ndiyo kiboko yao!
Kama JK hawezi kazi apishe wanaume.
 
Mwanakijiji asantesana mkubwa, nina imani tanzania tungepata waandishi wanaojua kuuliza maswali kama wewe,mengi yangekuwa yamekwisha.nimefurahi sana ulipobaki kwenye swali lako kwamba yeye mchungaji alijua ra fisadi nihaje akakope pesa hizohizo anazizipigia kelele,mchungaji kababaisha lakini ukambana na mpaka umemaliza mahojiano naye jibu lake kwa hilo hakutoa.
mchungaji umeniangusha sana,nilikuwa nakuaminia sana,yani kwa ajili ya m3 tu umekubali kuzalilishwa.
 
Mwanakijiji thanks. Mtikila hakupewa msaada anasema alikopa. Na deni atalilipa sasa kosa liko wapi?. RA ka foji na mtikila amesema anambulula mahakamani. Patamu hapo ndio kwanza ngoma ya mchezo inaanza!!
 
Hiyo link ya changia iko wapi? Tupe physical address. Au kama kupeana anuani ya nyumbani michosho tupe PO BOX.
 
Jamani, kweli mtikila ni mbabaishaji, Lakini , kuna kitu ninakiona hapa. Mwanakijiji amebadilisha focus yake, naona kama anamtetea Rostam aziz vile.

Ukiangalia kwa makini utagundua Hili na ninaona anashift attention ya Rostam kwenda kwa mtikila.

Mwanakijiji ni na wasi wasi kama hujapewa kitu na Rostam
 
Kuhani na Mtanzania.. asanteni... maana haya mambo ya kuingiliwa hadi studio inakuwa kasheshe.. (no pun intended)..
 
Ukitaka kumlaumu Mtikila jiweke kwenye mazingira kama yake na kisha angalia wewe ungefanya nini?

Kwanza Rostam ni rafiki yake, pia kakopa tena wakati huo kashfa za Rostam hazikuwa zinaeleweka waziwazi.Tatu, mkopo haukuwa na masharti yoyote.

Nne, hakuona urafiki kumshambulia Rostam alipoona anatumia kanisa kujisafisha. Akawa wa kwanza hata kutaka kwenda mahakamani ili mafisadi akiwemo Rostam waadhibiwe.

Namwamini Mtikila kuliko wanasiasa wetu wengi.
 
Sasa kama MKJJ amebadilisha direction...Itakuwa vipi Mtikila awe mbabaishaji?
 
Kuhani na Mtanzania.. asanteni... maana haya mambo ya kuingiliwa hadi studio inakuwa kasheshe.. (no pun intended)..

Mwanakijiji,

Nilipenda sauti ya mwanadada aliyepiga simu, inaelekea kuna la moyoni alitaka kukuambia kwi kwi kwi!!!!
 
Ukitaka kumlaumu Mtikila jiweke kwenye mazingira kama yake na kisha angalia wewe ungefanya nini?

Kwanza Rostam ni rafiki yake, pia kakopa tena wakati huo kashfa za Rostam hazikuwa zinaeleweka waziwazi.Tatu, mkopo haukuwa na masharti yoyote.

Nne, hakuona urafiki kumshambulia Rostam alipoona anatumia kanisa kujisafisha. Akawa wa kwanza hata kutaka kwenda mahakamani ili mafisadi akiwemo Rostam waadhibiwe.

Namwamini Mtikila kuliko wanasiasa wetu wengi.

Mkopo ni fadhila?
 
Mchungaji Mtikila asubuhi hii anakutana na waandishi wa habari kutoa ufafanuzi juu ya kauli ya Rostam Aziz aliyoitoa hapo jana Kilimanjaro Hotel kwamba yeye amekuwa akitoa msaada kwa makanisa na misikiti mbalimbali hapa nchini.
Mch Mtikila hakukanusha juu ya madai ya Rostam (Nasita kumuita mheshimiwa) ya kwamba alimpatia msaada wa million tatu (3) yapo April. Swali kubwa ni kwa nini Mch Mtikila pamoja na kupewa fedha hizo yeye aliendelea kumbomoa Rostam badala ya kumsifia kama vile wapambe wengine waliokubali kuwa TOILET PAPER ya kumsafisha yeye? Kwa nini Msaada wa Rostam hakuutolea kanisani Full Salvation kama alivyofanya KKKT kinondoni?
Fedha hizo zilikuwa mkopo kama anavyosema Mch.Mtikila au Msaada kwa kanisa au kwa Mch Mtikila Personally?
 
Mtikila ni Mpuzzi ..Hata akisema neno lipi hatutamuelewa,alienda kuomba Pesa?unaenda kuomba pesa kwa adui yako...Kuna Upinzani kweli??Mie nakwambia tukianza kutaja Majina kwa wale waliopo kwenye Payroll za Rostam Mtashangaa
 
Hahaha...

Ngoja tumsikilize kwanza huyu Mchungaji tujue ana lipi la kusema. Nae RA haoni hata aibu ati kulalamika kisa Mzee wa Magabacholi kachukua milioni tatu na bado anamuumiza... Alitaka baada ya kutoa hiyo Pesa aabudiwe?

Mtikila nimemkubali!!!
 
Mtikila kweli umetuangusha Mchungaji wewe. kumbe na wewe ulipewa tena ulipewa tarehe ambazo mambo ya UFISADI ndo yalikuwa yanaunguruma sana hapa nchini. eti mkopo kwa nini hukwenda benki kukopa? Wachungaji wetu Mhhhhh
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom