Tatizo letu waTZ kila mtu tuna mshakia kiasi kwamba kila mmoja tunamchanganya na mafisadi. Siamini kuwa kuna mtu aliye kamilika by 100%. Hata huyo baba wa Taifa Hayati J.K. Nyerere hakukamilika lakini haitoshelezi kumuweka kundi moja na mafisadi.
Nashauri tujaribu kuwapa watu credit stahili zao. Ni muhimu watu wasisahau kuwa popote penye watu zaidi ya mmoja lazima approach ya mambo itatofautiana kulingana na mtizamo wa kila mmoja kwani kila mmoja ni unique kwa kila kitu, la msingi ni kufikia muafaka ni approach gani at least inaungwa mkono na majority kwa hoja za msingi siyo tu kwa uwingi (hapa ndiyo umuhimu wa kiongozi kuchukua uwamuzi kitu kinacho mshinda msanii J.M. Kikwete.
Ni bora ya akina Mtikila, Lyatonga, Cheyo, Mbatia, Mabere, n.k. kuliko wanafiki akina Lamwai, Kaburu, Nswazingwako, Akwilombe, Tambwe, n.k. Tunahitaji kuwaunga mkono akina Mtikila ili waone support nyuma yao wapate nguvu yakufanya wanayoweza. Mpinzani wa kubabaisha hawezi kuvumilia taabu za kupigwa mabomu, kuvunjwa viungo vyao, kufunguliwa kesi zisizo na kichwa wala miguu, kufungwa, n.k. kwa kipindi cha miaka karibu 15.
Tusitarajiye kupata watu wa extremes kwani pia wana matatizo yao. Naomba tuwaunge mkono hawa wanaojaribu kama akina Mtikila na wenzao.
Rgds,