Rose Kamili aizuia ndoa ya Dr. Slaa mahakamani

Rose Kamili aizuia ndoa ya Dr. Slaa mahakamani

Majahili wameshindwa tena.Kumnunua Rose Kamili ili kupunguza kasi ya CDM kuingia Ikulu ni kupaka upepo rangi.Huyu Rose tuhuma zake ziko waziwazi sasa kwamba kalipwa mamilioni ya Fedha ili kufifisha kasi ya kulikomboa Taifa.Tunamwapia hatafanikiwa.Shibuda alijaribu ameshindwa vibaya.Rose Kamili itamkuta aibu kuu muda si mrefu.Tunamshauri arudi CCM walikomtuma awaambie kazi waliyompa ameshindwa.Nani kamdanganya anaweza kupambana na nguvu ya umma?

Na wewe umelipwa kiasi gani kutetea uzinifu?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Huyu Rose Kamili amewafanyia chadema usaliti mkubwa tu, anajuwa pingamizi lake halitamsaidia kumpata Slaa, sasa nia yake ni ipi?hamtakiwi mumwache ndani ya chama chenu.Halafu hao ndo watunga sheria wetu, nchi hovyo sana hii.
 
Mama msijali Makamanda tuko Imara kuwalinda na kupambana na yeyote anayevuruga chama.
Mama tutaarifu maamuzi ya mahakama yatatolewa lini? Hapo hakuna kesi bali porojo za Magamba dhidi ya CDM.

Kuwadi wa mfano wako sijapata kuona , dume zima hata aibu huoni? huyu Josephine aligeuka lini mama yako au ndio unataka kumtambaa kwa visingio maanake inaonekana huu utaratibu ni kawaida

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Du! huyu Slaa kweli noma..... anafanya ufisadi hata kwenye mademu? sasa kumnyang'any mwanamume mwenzake ndo nini? mademu wameisha hapa bongo? Asiseme kuwa ni hila, kila mtu mwenye hisia anafahamu inasumbuaje akili unapokuwa mpenzi wako kaenda nje na lijamaa kama Slaa. Ni hai Rose kulifiatilia na Huyo mume wa Josephine pia.. kila mtu anadai chake. tusimtetee Slaa...huu ni ufisadi wa ngono...tripple udhaifu! tuwe makini na vudume kama hawa anaweza katiza na mwenzako pia .......
 
Unafikiri kiongozi/viongozi ganie wengine wanaweza kuwa 'mzinzi' na kwa nini watu hawatumii siku nzima kuongelea uzinzi wao?

Kwenye blue: Ulaghai ni kosa Tanzania? tangu lini?

Kama ulaghai si kosa kwa Chadema kwa sisi watanzania ni kosa kubwa sana; hasa kwa mtu mzima anayepaswa kuwa mfano kwenye jamii hili la uzinzi ndio usiseme tena wa hadharani !

Chama
Gongo la mboto DSM
 
ah! dr nae alikuwa wapi miaka yote asioe mpaka leo ansumbuana na vicheche tu hawa! wanaharakati wenzangu tuoe na kuolewa mapema! sasa haya ni mambo ya kusumbuana na mahakama kwa umri wa dr slaa jamani!
 
kwa mantiki yako, Kama uzinzi ni mbaya, nakuuliza, mzinzi aliyepekekwa mahakamani na yule ambaye ni mzinzi ila hajapelekwa mahakamani kwa sababu yuko ikulu. Nani nafuu kati yao.

Aweda
kitabu kitakatifu kinasema "usiikaribie zinaa" na nakumbuka kwenye waraka wa mtume Paulo kwa wagalatia ameikemea na kuikataza sana zinaa; sasa kama mpaka leo hii wewe na umri wako unauliza kama zinaa mbaya hapo ndipo ninapokushangaa; huyo mzinzi unayedai yupo ikulu ni hisia zako ambazo hazina uthibitisho ni maneno ya mitaani; lakini hili Dr. Slaa ni bayana aliyeathirika na uzinzi wa Dr. Slaa amelalamika hadharani na anadai haki yake .

Chama
Gongo la mboto DSM
 
si kweli,kuzaa na mtu kunathibitishi au kutoa uhalali wa mtu kulazimisha ndoa.Ndoa ni agreement kati ya watu wawili wanaokubaliana.
The issue is kama yafuatayo hayakuwahi kufanyika,

mahali kutolewa
ndoa ya kimila
ndoa ya kanisa au DC.
Haya yakifanyika unaweza kuweka zuio,kwa kuweka pingamizi huku ukiambatanisha vidhibitisho.
Mahakama haivunji ndoa bila kufuata utaratibu wote wa ngazi za chini.

Naomba mfuatilie majibu na mapingamizi yote ya mawakili utajua,watoto wa miaka 18 wanajua wapi pakumtoa baba yao jamani.

Wewe msiye haya hivi unajua maana ya ndoa? Ningekushauri usiwahusishe watoto wewe ndiye uliyesababisha watoto wakose malezi ya baba yao; pepo wachafu wa uzinzi wamekukaa akilini inabidi Ufanyiwe maaombeezi maalumu ya kukuosha janaba.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
mungu wa kuwa upande wa wazinzi mmempa rushwa?

ona aibu hata kidogo mwanamke. weka staha kwa huyo mama mwingine.


Kama wewe ni msafi basi endelea kufungua Bakuli lako hilo na kumshambulia Josephine...
 
Ilikuwaje Dr. Slaa aachane na mke wake kinyume na maadili ya kanisa linasema ndoa haivunjiki mpaka kifo? Je hii haioneshi kuwa Dr. Slaa hana uadilifu? Tunaomba atuambie kwanini aliachana na mke wake?

Sidhani kama Dr. Slaa alimuoa huyo Rose. Ninachofahamu Dr. Slaa ali-zini na haya ndio matokeo yake sasa. Kila kitu kina consequences. Cha muhimu nikumalizana na huyo mama watoto wake; omba msamaha kwa Mungu wako and then move on. Hata kama ni kweli watu wanaifanya hii issue ya kisiasa; nafikiri akishamalizana naye na akiomba radhi kwa Mungu wake then wanaojaribu fitina watashindwa tuu. Kwakweli haya mambo ya ndoa yananitishaga kidogo-yanahitaji hekima ya hali ya juu maana leo kwako kesho kwangu.
Hata hivyo kuna mambo yamenishangaza kidogo: 1)kusikia eti huyu mama anataka child support ya watoto watu wazima? 2) Watu wanazungumzia mbio za uraisi ; if I can recall Slaa alisema hatapigania tena ataachia wengine wapiganie (kama nakumbuka vizuri). Anyways; i guess it is up for the members to choose. Good Luck Dr Slaa.
 
....mkuu! maadam ndugu jamaa na marafiki "hawakuwamwagiaga michele" kusheherekia tukio la heri...hakuna ndoa hapo..na kuhusu hiyo sheria..naitazama kama sheria "nyingine toka ugenini" sawia na ile ya "toni blea"-ya sefu kumuoa chale, na jenifa kumuoa saada...
 
si kweli,kuzaa na mtu kunathibitishi au kutoa uhalali wa mtu kulazimisha ndoa.Ndoa ni agreement kati ya watu wawili wanaokubaliana.
The issue is kama yafuatayo hayakuwahi kufanyika,

mahali kutolewa
ndoa ya kimila
ndoa ya kanisa au DC.
Haya yakifanyika unaweza kuweka zuio,kwa kuweka pingamizi huku ukiambatanisha vidhibitisho.
Mahakama haivunji ndoa bila kufuata utaratibu wote wa ngazi za chini.

Naomba mfuatilie majibu na mapingamizi yote ya mawakili utajua,watoto wa miaka 18 wanajua wapi pakumtoa baba yao jamani.
Lo!
Josephine AKA The Spare Rib amesurface kumtetea D Slaa?
Dr Slaa has just entered a deeper hole!!
Now all hell will break loose
 
FJM Wewe ndo unakwepa hoja, hoja hapa ni kuwa asiye mwaminifu kwa vitu vidogo hata vikubwa pia. Hao walioko serikali wakati hawakuwepo hawakuwa waaminifu kwa vitu vidogo lakini bado tukawapa mambo makubwa na madhara yake ndo hayo, ufisadi kwenda mbele.

Hivyo rai yangu, ni kuwa mtu yeyote anayetaka kuwa kiongozi na kwa vile hatujawahi kumpa vitu vikubwa tumpime uaminifu wake kwa vitu vidogo. Na yule tuliyewahi kumpa vitu vikubwa tumpime kwa vitu vidogo na pia vitu vikubwa.

Na kama tukiwakuta sio waaminifu ama kwa vitu vidogo ama vikubwa na tukaendelea kuwaamini zaidi kuwapa kuwapa vitu vikubwa ama kuendelea kuhodhi vitu vikubwa.

Hakika sie ni tutakuwa wendawazimu.


Kiongozi mbona umekesha sana kwenye hii issue? Inakuhusu nini wewe hasa, au ndio wewe umekimbiwa nini? Maana kama ungekuwa kweli unakerwa na uzinzi wa viongozi tungekuwa tumekusikia siku nyingi i.e Igunga kwa mfano, au Morogoro na ile SMG yetu!
 
Hapa kama kuna mkanganyiko vile....suala la ndoa na siasa! Kama siasa imepachikwa kwenye siasa hii ni mbaya sana, ila kama ni masuala yao ya maisha ya kimahusiano hili naona halina shida. Sidhani kama haki za kindoa za mtu zikatishwe na mahusiano ya kisiasa. Ila kama ametumiwa.....hapo mh...

Hapa kinachoendelea ni kuchafuana majina tu; ndoa na siasa havina uhusiano kabisa ila kule kuchafuana majina hasa kwa kigezo kuwa "kama hawezi kuendesha nyumba yake ataendeshaje nchi" kunafanyika ili kumdiscredit dr.
Slaa.
 
Hapo kwenye red. Mkuu, ingekuwa ni hivyo, basi leo Mandela asingekuwa ameupata urais na hata Jacob Zuma. Mwanasiasa/ Kiongozi thabiti lazima akubali kupita kwenye tanuru la mashambulizi kutoka kwa wapinzani wake.

Mandela alimaliza tatizo la ndoa yake kwa kuidissolve; na ndiyo maana Madikizela hakuingilia wakati Madiba anaamua kumuoa Gracal. Zuma yeye alitumia misingi ya mila za kabila lake, kwa hiyo hajawahi kuwa na tatizo la ndoa. Kinachotakiwa ni kwa Dr. Slaa kumalizana kabisa na huyu Mheshimiwa mbunge ili kusiwe na jambo lolote baina yao mbele ya sheria kama lipo kwa sasa. Na kama hakuna jambo lolote baina yao, basi Dr. Slaa achukue hatua thabiti za kumnyamazisha huyu Mheshimiwa kisheria, ikiwa ni pamoja kutumia sheria zinazolinda watu dhidi ya kuchafuliwa majina yao mbele ya jamii.
 
Wewe unajua kwamba Ridhiwan naye ni Muhanga wa kutekelezwa na mzazi? au kwa vile mnamjua kipindi cha neema?

Sangarara mambo ya Ridhiwan kutelekezwa inahusu nini na hoja hii? anayemshutumu Dr Slaa ni mzazi mwanzake Rose kamili tena ni mbunge wa CDM.

Je ulishasikia mzazi gani wa Ridhiwan aliyempeleka mwenzie mahakamani kwa kuachiwa mtoto? Au unataka kufunika kombe mwanaharamu apite?

Kwa ufupi n JK sijamjua leo najua alipokulia aliyemlia mpaka kazi ya baba yake mpaka kifo chake na kisomo cha hitima nilikuwepo . Pia mzee mwenye jina la Jakaya namjua vizuri sana japo sikuweza kumzika lakini katika hitima nilikuwepo.

Isitoshe Ridhiwan ndio kipenzi cha JK vipi amtelekeze ? Hata watu wanapomuuliza mbona huyu mtoto unampenda zaidi jibu ni kwasababu mama yake ametangulia mbele ya haki hivyo anahitaji upendo wote kutoka kwa baba. Huyu ndio JK kipenzi cha watu na watoto!! Na pale mama yake mdogo( mlezi) Ridhiwan alipofariki bado JK hakukosa kuonesha upendo wake. Ndio maana hata leo JK akipita popote atakusanya watu hata ww najua utapenda mkono wake uuguse..
 
Ametelekezwa kivipi na kapewa kazi anapofanya kazi baby daddy wake?Unajuwa maana ya kutelekeza wewe?

Mkuu wangu jmushi1, hakika unanionea kuniuliza mimi maswali hayo hayo.....anayepaswa kuulizwa hayo ni Bi. Rose na sio mimi na ndio maana ktk post yangu; nime-base kwa kusema "Kama ni kweli......!" "Kama ni kweli......!" Inavyoelezwa na watu including na huyo Bi. Rose, ni kwamba amelekezwa na ndio maana nikasema kama ni kweli hayo yasemwayo, basi ni serious social crime!!!
 
Back
Top Bottom