Rose Kamili aizuia ndoa ya Dr. Slaa mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rose Kamili aizuia ndoa ya Dr. Slaa mahakamani

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Molemo, Jul 12, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Katika kile kinachoonekana kupunguza kasi ya CDM na kiongozi wake machachari Dr Wilbroad Slaa Mbunge wa viti Maalum wa chama hicho Rose Kamili amekwenda mahakamani kumshtaki Katibu mkuu wake Dr Wilbroad Slaa kwa kile anachopinga uhusiano wa Dr Slaa na mke wake mtarajiwa Josephine Mushumbusi.

  Katika hati ya mashtaka aliyo nayo Rose analalamikia kutelekezwa yeye na watoto wake wawili baada ya Josephine kuingilia ndoa yao.Anaiomba mahakama itamke uhusiano wa Dr Slaa na Josephine ni batili.

  Kuna tetesi zimezagaa Rose Kamili amenunuliwa ili kuvuruga mijakati ya CDM kuiandama serikali ya CCM

  Source:Tanzania Daima

  Updates from Mwananchi...Majibu ya Dr Slaa
  Dk Slaa: Nimeyazoea
  Alipotakiwa kuzungumzia kesi hiyo nje ya Mahakama, Dk Slaa alisema: "Hayo mambo nimeyazoea na kimsingi hayanipi shida yoyote."
  Alipoulizwa endapo anajipanga vipi kulipa fidia hiyo alijibu: "Kesi ni kesi hivyo siyo kila kinachoombwa kwenye kesi lazima kilipwe."
  Hata hivyo, Dk Slaa alisema asingependa kuzungumzia suala hilo kwa undani kwa kuwa liko kwa mawakili wake lakini akasema amebaini kuwa hizo ni hila na michezo michafu ya kisiasa.
  "Kwanza siyo pingamizi moja tu, kuna pingamizi mbili mahakamani lakini kwa ufupi ifahamike kuwa hizo ni hila."
   
 2. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,855
  Likes Received: 4,529
  Trophy Points: 280
  Duh! Ebwana eh!
   
 3. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Mmmh!

  Hii inakuja siku mbili baada ya kuipa ukweli serikali!

  Inawezekana ni kweli.

  Lakini sijawahi sikia mtu akishitakiwa na X wake kisa mchumba mpya!
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,455
  Likes Received: 81,692
  Trophy Points: 280
  Alikuwa kimya kipindi kirefu sana...aliibuka miezi miwili au mitatu kabla ya uchaguzi wa 2010 baada ya magamba kumpa bulungutu la nguvu na kisha akapotea kabisa, sasa inaelekea kishachukua bulungutu jingine la magamba ili amchafue tena Dr Slaa.
   
 5. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Kumradhi, mimi bado ni Mugya (mgeni) hapa JF.

  Hivi Rose Kamili bado ni mke halali wa Dr Slaa?
   
 6. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Wivu tu unamsumbua huyo . Ritz, Zomba
   
 7. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hivi penzi huwa linalazimishwa jamani?!
   
 8. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Tusiwe biased bwana, kama mwanasiasa ambae ni kioo cha jamii lazima social responsibilities zitimizwe! Josephine (first lady wangu binafsi) hajapata hati ya talaka kwa mumewe na ndo iko mahakamani. Kama Rose Kamili nae hajatalikiwa na mumewe, ana haki ya kumshika ugoni na kudai matunzo ya watoto. Hili sio suala la chadema, ni suala lao binafsi.
   
 9. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Mkuu, huyu Bibie ni mbunge wa viti maalum wa CHADEMA, unataka kusema Chadema hawakujua kuwa analipwa na CCM?

  Kuna waliosema alipewa ubunge na Chadema ili kuzibwa mdomo kuzungumzia suala la "ndoa" yake na Dr.Slaa......posho haijatosha?
   
 10. M

  Molemo JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Rose hajawahi funga ndoa na Dr Slaa bali alizaa naye watoto.
   
 11. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #11
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Nimresoma stori hiyo muda mfupi Tanzania daima:


  Ndoa ya Dk. Slaa yapingwa

  na Happiness Katabazi

  ALIYEKUWA mke wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Rose Kamili Slaa nee Sukum, amefungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, akiiomba izuie Dk. Willibrod Slaa, asifunge ndoa na mchumba wake, Josephine Mushumbusi.

  Kwa mujibu wa hati ya madai ya kesi hiyo ya masuala ya ndoa iliyopewa na Na. 4/2012 ambayo gazeti hili inayo nakala yake, ambayo tayari imepangwa kusikilizwa na Jaji Laurence Kaduri, ilifunguliwa mahakamani hapo hivi karibuni na wakali wa mlalamikaji Joseph Thadayo.

  Washitakiwa katika kesi hiyo ni Dk. Slaa na mchumba wake, Josephine, ambapo mlalamikaji anaiomba mahakama isikubali shauri hilo lipelekwe kwenye Bodi ya Maridhiano ya Masuala ya Ndoa kwa ajili ya kupatanishwa.

  Katika dai la pili, Rose anaiomba Mahakama itangaze kuwa yeye na Dk. Slaa bado ni wanandoa na dai la tatu anaiomba itamke kuwa ndoa baina yake na Dk. Slaa bado ni halali kisheria na kwamba ndoa nyingine itakayofungwa kinyume cha sasa itakuwa ni batili.

  Katika dai lake la nne, mlalamikaji ambaye sasa ni Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA), anadai kuwa Josephine, alimshawishi mumewe (Dk. Slaa) kuivuruga ndoa yao.

  “Pia nia ya wadaiwa hao wawili ya kutaka kufunga ndoa Julai 21 mwaka huu, katika eneo lolote lile, ndoa hiyo ihesabike kuwa ni batili.

  “Pia naiomba mahakama iwaamuru wadaiwa wanilipe fidia ya sh milioni 50 kama gharama za matunzo ya watoto wawili, Emiliana na Linus aliyezaliwa mwaka 1987,” alisema.

  Rose anadai kuwa walianza kuishi pamoja na Dk. Slaa kama mume na mke, na amekuwa akiwahudumia watoto hao peke yake tangu mwaka 2009 baada ya Dk. Slaa kumkimbia.

  Pia anaiomba mahakama imwamuru Josephine naye amlipe fidia ya sh milioni 500 kwa sababu alimsababishia usumbufu mkubwa na kumharibia ndoa yake.


  Ninaona kuwa inabidi Dr. Slaa atatue matatizo yake ya kifamilia kikamilifu kabla hajaendelea mbele zaidi na harakati za kisiasa kwani hayo ndiyo yatakayomwangusha hasa kwa vile aliingia maisha ya familia baada ya muda mrefu wa celibacy.

  Unfortunately mambo kama haya ndiyo yanayoweza kutumika kuvuruga chama chao. huyu mama huenda keshapatiwa burungutu kubwa sana na CCM kusudi amvuruge Slaa na CHADEMA yote, sidhani kama yeye ni mbunge wa CHADEMA kwa dhati na huenda alipewa kiti hicho kinyemela kwa njia ya kumnyamazisha lakini hataki kunyamaza kwa vile upande wa pili una donge nono zaidi ya analopata kwenye ubunge huo.
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,455
  Likes Received: 81,692
  Trophy Points: 280
  G hata Shibuda ni mbunge wa CHADEMA, si unaona vituko vyake dhidi ya CHADEMA na kuifagilia magamba kwa sana? Wengine huweza kununuliwa kirahisi sana ili kuchafua hali ya hewa chamani.
   
 13. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Unazungumziaje kanuni inayowahesabu wawili wanaoishi kinyumba kwa zaidi ya miaka miwili kuwa ni sawa na wanandoa?
   
 14. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #14
  Jul 12, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Well, if that is the case, then ana haki ya kudai matunzo ya watoto. Mahakama itaamua kama ni kwa kiasi gani.
   
 15. M

  Molemo JF-Expert Member

  #15
  Jul 12, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hawakuwahi kuishi pamoja ila walizaa pamoja
   
 16. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #16
  Jul 12, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Kuna mambo mwengine nadhani tunaingiza siasa hata katika mambo yasiyohusu.

  Kama Rose Kamil hapati haki zake za msingi kwa baby daddy wake asichukue hatua kwa sababu za siasa?

  Slaa angeondoa hizo loop holes wala asingeshtakiwa pahali
   
 17. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #17
  Jul 12, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Hawakuwahi kuishi pamoja lakini walizaa watoto (3?)....you are joking, right?!
   
 18. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #18
  Jul 12, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Kwani wanaozaa na waume wa watu wanazaaje? Its a 5 minutes process to make a baby mwalimu!
  And I thought watoto ni wawili?
   
 19. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #19
  Jul 12, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Wait a minute! Hao Emiliana na Linus wamezaliwa 1987? Yaani anataka matunzo ya a 25 yrs old man and a woman (manake sio girl tena)? Ama anadai arrears? Mmh, fishy!
   
 20. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #20
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Huyu Rose inabidi achukuliwe hatua za kinidhamu ikibidi afukuzwe
   
Loading...