[
Mkuu nauhakika hujui maana ya unafiki,
unafiki ni kusema nafanya A ila nyuma ya pazia unafanya B. Is this the case ktk sakata hili? Sasa Slaa anayesema yuko na Jose na ndivyo ilivyo, je ni mnafiki?
Wanafiki ni wale wazinzi lakini mbele ya macho ya umma au hapa JF wanasema sisi watakatifu kitu ambacho ni kinyume chake ktk uhalisia wake. Baada ya hiyo shule, nakuuliza tena, je, Slaa ni mnafiki.
Nyie watakatifu naona mmeishiwa hoja, wacha nizime laptop yangu.
Narudia tena wanafiki wana mji wao; hivi wewe Aweda unajifanya hujui maana ya zinaa, hujui nini maana haya ndoa; bado pia unajifanya hujui ni maana ya talaka?
Sasa kama wewe si mnafiki ni kitu gani? Hoja iliyopo ni Dr. Slaa kuikimbia familia yake na kwenda kuishi na kimada kujinadi mbele ya watanzania kama yeye ni mtu safi kimaadili huku akijua fika si msafi je kama huo si unafiki ni kitu gani nitafutie jibu au unataka tukufungulie vitabu vitakatifu ili ujue mzinifu na mnafiki ni watu wa namna gani?
Chama
Gongo la mboto DSM