Ridhiwani achafua hali ya hewa Times FM

Ridhiwani achafua hali ya hewa Times FM

Waryoba ni mtu ambae ana jitambua siyo kilaza kama yeye alivyo kilaza.
 
tatizo la nchi za kiafrika, baba akiwa Rais basi mtoto naye ni Rais mama pia ni Rais - kazi tunayo.

ulikuwa hujui hilo. Dereva wa rais ni rais wa madereva wote kwenye nchi husika. Hata beki tatu wa rais ni rais wa mabeki 3 wote kwenye nchi husika.

So no matter u like or not, Ridhiwani ni rais wa vijana wote Tanzania. Asietaka agome kula msosi wa kesho cku nzima
 
CCM na Serikali yake wanajaribu kukwepa zanzibar kuvunja katiba ya jamhuri ya muungano. Tuna nchi mbili, serikali mbili, wa kulaumu Warioba? Tume za shelukindo, jaji kisanga, jaji nyalali, tume ya amina salum ali, sakata la jumbe, ccm hazioni haya kwamba suala lilikuwa ni serikali TATU? Kwanini leo ione serikali tatu ni hoja ya warioba?

Muhimu ni je - nani wa kulaumiwa kwa zanzibar kuvunja katika ya jamhuri ya muungano kwa kujitangaza kama nchi kamili? Warioba?

Wazanzibari hawawezi rudi nyuma kwani mkataba wa muungano (1964) ulilenga serikali tatu. Ni zamu yetu Tanganyika kufanya kama wao kwa manufaa ya muungano na wananchi wa pande zote mbili.


Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla.



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
kakosa uhalali wa kuwa kiongozi
uwezi kuwasemea wazee wote na kuwatukana watu wazima kisa ni siasa
RIDHIWANI KIKWETE jifunze adabu kama ukufundishwa adabu na wakubwa zako
usiuonyeshe upumbavu wako hadharani
 
..hizi kejeli za ridhiwan sizishangai....maana yeye ni uzao wa utawala wa hovyo uliopanga kwenye ikulu yetu sasa....kejeli za huyu mtoto wa JK kwa Jaji Warioba hazina tofauti na kajeli anazofanyiwa Warioba na ikulu...haya yote ni matokeo ya kuwapangisha majizi na matapeli kwenye ikulu yetu....Watu hawa watu wamaana kwo ni wale wenye maslahi nao na family zao....hata kama ni majizi ya mali za umma kwao haijalishi kama watafaidika....Wamejenga kibri na dharau kwa wanaotofautiana nao hata kama tofauti hizo ni kwa maslahi ya nchi....

..Labda niulize tu jukwaa hapa.....hivi walisema nini kilimuua yule mbunge Bwanamdogo wa Chalinze???ningependa sana kujua .maaana kwa matendo ya ikulu....na kejeli huyu mtoto....sitashangaa kama ameandaliwa kuwa mbunge wa Chalinze kwa hila.....inawezekana kabisa hii....maana haya mambo ya kuhusisha kifo kama hatma ya mtu na wadhifa wake yamejitokeza sana kwa watu hawa.....sitasshangaa kusikia walim fix Bwanamdogo chalinze kama mkakati wa huyu dogo kutawala Chalinze.....kwa baba yake...bahati mbaya sana hutuna forensic medicine experts hapa TZ.....kuna watu wengi wamedhuriwa kwa order za ikulu.....kwasababu tu za kimaslahi...ama kutofatiana......Naomba mzee Warioba alindwe...wasije wakawatamdhuru watu hawa wabaya....
 
Hivi kwani Ridhiwan si ndo aliyepata division iv matokeo ya kidato cha nne? Mimi sishangai hata kidogo kama ameropoka namna hiyo. Kwani tunatakiwa kusiskiliza hoja gan kutoka kwa form four failure? Nafikiri yuko sahihi tu kwa vile hatumii akili vizuri katikta kufikiri, yeye na wengine wanafikiri hii nchi ni mdoli wa kuchezea nyumbani kwao. Mungu tubariki vijana tuelewe huu uzandiki na kupinga kwa nguvu zote.:amen::amen:
 
hata uwe mrefu vipi hauwezi kuiona kesho,mtoto wa late ghadaf juzi aliomba radhi kwa wananchi wa libya kwa kuwakosea kipindi baba yake anatawala,Rizimoko acha dharau warioba ni sawa na babu yako.
 
Nakubaliana na hoja yako na ulicho kiandika ndio hicho CCM tunakitaka.

Kama utakumbuka kauli ya rais, alisema hana tatizo na serikali tatu, kama utakumbuka kauli ya Nape kama msemaji wa chama, alisema CCM haina tatizo na serikali tatu kama Watanzania wakihitaji.

Jambo ambalo sikubaliani nalo ni hizo kauli za wapinzani kama vile, "Tanganyika haiepukiki", mara "bila Tanganyika patachimbika" etc

Kauli hizo ni wazi kuwa zimekaa kishari na zina viashiria vya uvunjifu amani. Sasa niwahikikishie wote wenye kauli hizo, endapo watathubutu kujaribu kwa namna yoyote kuidai Tanganyika kimabavu, basi nitakuwa mstari wa mbele kushinikiza FFU kuwaua tena kwa kuwapiga risasi za kichwa watu wote wa aina hiyo.

Hatuwezi kuendelea kuvumilia kauli za wapuuzi wachache wanaotaka kuingiza nchi yetu kwenye machafuko kisa matamanio yao kwa Tanganyika. Wakileta fujo wataenda kukutana na Tanganyika yao kuzimu.

Ukiendelea kuongea hivi bila kufikiria mara mbili, tofauti yako na Ridhiwani itakua ni ndogo sana.
 
H=kama ndio ameongea hayo hata mm ameniboa sana yeye angeongea kilichompeleka kule sio kumshambulia mzee wa watu amemkosea nini warioba yeye warioba amefanya kazi yake kama alivyotuagizwa na mkubwa wake raisi kikwete na ndiye aliyemchagua kufanya hilo jukumu iweje haka katoto kanashadadia na kumponda mzee wa watu aangalie kuwa hayo maneno kama ameyaongea atakuja kuyalipia kwani asiyefunzwa na wazazi ufunzwa na ulimwengu asifikiri baba yake ndo mzazi wake pekee hata huyo waarioba tulijiofunza mwanzo sie ni baba yako sio yule aliyekuzaa tu ndo astahili kuitwa baba hata aliyekuzidi miaka kiasi hicho naye ni baba ameniboa ridhiwani amenikera na kunichefua aende kuomba msamaha kwa warioba vinginevyo jimbo la chalinze atalisikia kwa mbali ngoja tushike ile nafasi kiaina hapa kama ataipata anafikiri atakuja siku awe rais kama baba yake asifikirie hivyo ameshajiroga


nilikuwa namsikiliza riziwani mtoto wa jk akiongea times fm leo hii… dah! Hata kama ni mtoto wa mkuu wa kaya ila ana dharau,

namnukuu "kuna watu ambao wameshamaliza muda wao wa kuishi,muda wao wa kucheka hapa duniani lakini ndio wa kwanza kushadadia serikali tatu, namshangaa warioba anavyopayuka kuwa anataka serikali tatu, kila siku anafanya interview kwenye redio tv na magazeti,ameshikilia maoni ya watu kama yake binafsi. Mbona wakati akiwa kijana na akiwa waziri hakuwahi kudai serikali tatu ila alikuwa anashikilia serikali mbili? Iweje leo anapayuka kudai serikali tatu?

Ila kwa sentensi hiyo kanikoroga akili! Kumbe naye anataka serikali mbili,warioba kutetea hoja za wananchi imekuwa nongwa sana kwa watu wa ccm?

Ridhiwani umeniboa!
 
Hivi unakumbuka malumbano ya hoja ya jana itv stesheni kuna mtu alisema kuwa
je ibilisi naye anapenda mtu mnafiki au mkweli ? Watu kimyaaa akaendelea kusema kama ibilisi angekuwepo hapa basi asingependa mtu mnafisi ndivyo alivyo huyo mtoto wa kiongozi wetu anajipendekeza apate jimbo la chalinze ameshajikwaa ataliona labda wafanye maarifa kama ya 2010
ukiendelea kuongea hivi bila kufikiria mara mbili, tofauti yako na ridhiwani itakua ni ndogo sana.
 
Kwa wale ambao wamefika chuo kikuu na kupata angalau shahada moja, hemu tuwe mstari wa mbele kusaidia wale ambao hawakupata elimu.

Ndugu zangu, katika kukusanya maoni ya watu, kuna njia mbalimbali hutumika, na matumizi ya njia hizo ndio zitapelekea uhalali wa data zilizopatikana na hivyo matokeo ya tafiti.

Kwa njia alizotumia Warioba na vibaraka wake, ni wazi kuwa "data" zake hazina uhalali wowote kwa kuwa sio data za kisayansi.

Mtafiti hawezi kukusanya maoni ya kajikundi fulani cha wananchi (ambacho labda kanataka serikali 3) halafu aje ahitimishe kuwa wananchi wanataka serikali tatu. Huo ni wendawazimu.

Yeye kama mwenyekiti wa tume akupaswa ku-generalize, angesema tu kwa mujibu wa data, idadi hii ilitaka hivi, hiyo ilitosha. Ila sio kudanganyana kuwa Watanzania tunataka serikali tatu kwa kutumia maoni ya watu 30,000.

Hata standards za sampling pekee zinatosha kuikataa rasimu ya Warioba.

hivi wana-CCM hawakutoa maoni yao?achen kuweweseka!
 
Nilikuwa namsikiliza Riziwani mtoto wa Jk akiongea Times Fm leo hii… dah! Hata kama ni mtoto wa Mkuu wa Kaya ila ana dharau,

Namnukuu "Kuna watu ambao wameshamaliza muda wao wa kuishi,muda wao wa kucheka hapa duniani lakini ndio wa kwanza kushadadia Serikali tatu, namshangaa Warioba anavyopayuka kuwa anataka Serikali tatu, Kila siku anafanya interview kwenye redio tv na magazeti,ameshikilia maoni ya watu kama yake binafsi. Mbona wakati akiwa kijana na akiwa Waziri hakuwahi kudai Serikali tatu ila alikuwa anashikilia serikali mbili? Iweje leo anapayuka kudai serikali tatu?

Ila kwa sentensi hiyo kanikoroga akili! Kumbe naye anataka Serikali mbili,Warioba kutetea hoja za wananchi imekuwa nongwa sana kwa watu wa CCM?

Ridhiwani umeniboa!

qu ma nyoko.
 
hivi wana-CCM hawakutoa maoni yao?achen kuweweseka!

kimeniuma sana aisee. Kulizagaa habari kile kipindi cha kampeni(2005) cha baba yake kuwa aliahidi kuwa kinyume na baba yake vinginevyo amwahidi sehemu ya urais wake otherwise ataweka kila kitu hadharani alivyomfanyia mama yake. Labda ndo sababu hata akifanya cha ajabu baba yake anamwangalia tu. Atafunza na ulimwengu tu.
 
Back
Top Bottom