Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 375,977
- 871,045
Sikusikiliza utetezi wake kwakuwa kwa asilimia 100 atakana uhusika na blahblah zingine
Hapa nataka tujadili asili/chanzo cha tatizo mwendelezo hadi ukomavu na athari zilizotokea sasa
Tatizo lilizaliwa kipindi cha Rais Benjamin Mkapa hasa kipindi chake cha 2000-2005 pale aliporuhusu wanasiasa wawe pia wafanyabiashara/ wafanye biashara
Utakatishaji pesa ukaanzia hapo... Mawaziri, wabunge na viongozi wengine wa chama na serikali wakazivamia biashara kwa nguvu . Mitaji ikiwa ni pesa walizokuwa wamezificha..
Sasa kwakuwa wengi hawakuwa na uzoefu wa biashara ama historia za biashara! Walishindwa haraka.. Kwahiyo wakaja na plan B ya kuwekeza mitaji yao kwenye wafanyabiashara wakubwa waliokubali kufanya Partnership!
Hizi biashara za hawa wafanyabiashara nazo baada ya muda zikafilisika .. Mfano ni Scandinavia na Sumry.. Makampuni ya kusafirisha abiria na vifurushi ndani na nje ya nchi.. Nitafafanua hili kwenye comments ili kufupisha mada
Mpaka Mkapa anaondoka madarakani wafanyabiashara wakubwa wakawa wamepata somo kupitia kwa wenzao waliofanya ubia na wanasiasa hivyo wakaja na mbinu mpya sasa ambayo itawahakikishia ulinzi wa biashara zao lakini pia kuepa kufilisika
This time around ubia ukawa tofauti sasa! Hawakuhitaji sana mitaji ya wanasiasa ama kama waliihitaji lakini wakaweka kigezo kwamba wao ndio wawe na mamlaka yote ya uendeshaji na mbia mwanasiasa abaki kusubiri faida ama gawio
Kwa sehemu nyingine kwa makubaliano maalum ya gawio ama faida wakawatumia baadhi ya wanasiasa kuwanasibisha kwamba biashara fulani ni ya mtu fulani ama ni mbia
Mwanzoni athari zake hazikuonekana maramoja.. Lakini kadiri wafanyabiashara hao walivyoyatumia majina ya wanasiasa wakubwa ndivyo walivyoanza kutengeneza matatizo kaka
. Kukwepa kodi kwa kutumia wanasiasa hao
. Kunyanyasa watendaji wa serikali wa idara mbalimbali huku wakitegemea ama kupata kinga ya wanasiasa
. Kuwanyanyasa wafanyakazi wao na kuwatishia kwamba hawawezi kuwafanya kitu kwakuwa hiyo biashara ni ya mwanasiasa fulani ama ni mbia
. Kudhulumu, kupora, kuteka, kufilisi hata kuua bila kuogopa mkono wa sheria kwakuwa tu wana backup ya mwanasiasa fulani
Ridhiwani huyu anayejitetea leo alitumika vibaya sana kipindi cha baba yake akiwa rais! Hakukuwa na biashara kubwa ama dili kubwa ambayo hakuachwa kutajwa kama mhusika mkuu ama mhusika muhimu
Si yeye binafsi, si baba yake au mama take! Si ndugu zake ama viongozi wa chama na hao wafanyabiashara walijitokeza hadharani kukanusha .. Pen fine waliona ni sifa!
Hali ilipozidi kuwa mbaya na huku Ridhiwani (Riz1, Riz one, Riz moko) akiwa ndio mtanganyika maarufu zaidi akatungiwa wimbo wa Riz one ongea na mshua (huku street kimenuka)
Sasa uhusika ukavuka mipaka toka kwa mtoto hadi kwa baba.. Home shopping center wakatajirikia hapo... Aliko Dangote, Rostan nknk wakakamata hatamu za dili na biashara kubwa kubwa kwa jina la JK.. Kukawa sasa kuna mtandao kamili unaojumuisha wanasiasa na wafanyabiashara kubwakubwa
Akaingia jiwe Mzee Magu akataka kurudisha heshima ya chama na ya nchi lakini mtandao ukamzunguka na Kumgeuka! Yaliyotokea ni historia!
Baada ya Magu kulala mahali anapostahili.. Mtandao ukarudi tena kwa nguvu zaidi lakini sasa kipindi hiki Ridhiwani akiwa hatajwi sana Ila ile historia ikiwa imezama vema mioyoni mwa wengi
Lake oil wakaja na nguvu mpya, ari mpya na kasi mpya... Wakabadili rangi jina na vitu vingi, wakafanya uwekezaji mkubwa na wa kutisha! Popote walipotaka kuweka kituo cha mafuta hakuna aliyewazuia.. Nasema hakuna! Kila walipokutana na vikwazo kuna majina makubwa yalitumika na mambo yakaenda walivyotaka
Lake oil ni mwathirika mkubwa wa uharibifu kwenye maandamano ya October 29.. Nyuma ya mafanikio yake kuna simulizi za kutisha sana toka kwa wafanyakazi na watu mbalimbali ambao walishawahi kupishana kauli na wakuu wa kampuni
Madereva waliotia shoti
Wafanyakazi ambao wengine walisingiziwa makosa mbalimbali
Waliolazimishwa kuuza maeneo yao
Waliofanya biashara na kukatokea shida nknk
Kwa simulizi za wengi hao jamaa ni untochable na ukiingia kwenye 18 zap utajuta kuzaliwa kwakuwa hakuna rangi utaacha kuona!
Leo hii Riz1 akija na utetezi wowote ule haumsaidii kisiasa wala kijamii kwakuwa ndio kwanza anaamsha vilivyolala.. Amechokoza tena wakati ambao sio sahihi kabisa.. Angekaa kimya kama miaka yote ingemsaidia zaidi
View: https://youtu.be/xwaZMI1Erro?si=Oe4KsScbwvTCknqt