Ridhiwani achafua hali ya hewa Times FM

Ridhiwani achafua hali ya hewa Times FM

Tugutuke

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2011
Posts
501
Reaction score
168
Nilikuwa namsikiliza Riziwani mtoto wa Jk akiongea Times Fm leo hii… dah! Hata kama ni mtoto wa Mkuu wa Kaya ila ana dharau,

Namnukuu "Kuna watu ambao wameshamaliza muda wao wa kuishi,muda wao wa kucheka hapa duniani lakini ndio wa kwanza kushadadia Serikali tatu, namshangaa Warioba anavyopayuka kuwa anataka Serikali tatu, Kila siku anafanya interview kwenye redio tv na magazeti,ameshikilia maoni ya watu kama yake binafsi. Mbona wakati akiwa kijana na akiwa Waziri hakuwahi kudai Serikali tatu ila alikuwa anashikilia serikali mbili? Iweje leo anapayuka kudai serikali tatu?

Ila kwa sentensi hiyo kanikoroga akili! Kumbe naye anataka Serikali mbili,Warioba kutetea hoja za wananchi imekuwa nongwa sana kwa watu wa CCM?

Ridhiwani umeniboa!
 
Nilikuwa namsikiliza Riziwani mtoto wa Jk akiongea Times Fm leo hii… dah! Hata kama ni mtoto wa Mkuu wa Kaya… ana dharau, namnukuu "Kuna watu ambao wameshamaliza muda wao wa kuishi,muda wao wa kucheka hapa duniani lakini ndio wa kwanza kushadadia Serikali tatu, namshangaa Warioba anavyopayuka kuwa anataka Serikali tatu,… kila siku anafanya interview kwenye redio tv na magazeti,ameshikilia maoni ya watu kama yake binafsi… mbona wakati akiwa kijana na akiwa Waziri hakuwahi kudai Serikali tatu ila alikuwa anashikilia serikali mbili? Iweje leo anapayuka kudai serikali tatu?"… na mengine meeeengi! Ila kwa sentensi hiyo kanikoroga akili! Kumbe naye anataka Serikali mbili… Warioba kutetea hoja za wananchi imekuwa nongwa sana kwa watu wa CCM…
Riz Moko umeniboa!

Sasa ulitaka atetee serikali Tatu wakati chama kinataka Serikali mbili?Sasa kama wakati wa Warioba umekwisha yeye anauhakika wakuishi kufikia miaka ya Warioba?Na baba yake ana miaka mingapi leo?Naye tuseme muda wake wa kuishi umefika?

Ni asiye na akili tu anauwezo wa kuongea haya aliyoongea kama kweli ameongea,kwani hakuna mtu aijuaye siku wala saa yake ya kuondoka si kijana,mtoto,mzee na hata mgonjwa.

Pole zake lakini,msamehe pia NAFASI aliyonayo ndiyo inamfanya aseme hayo aliyosema.
 
Acha umbeya wako;
Kwani kasema uongo?

Haya, sema wewe kasema kweli? Yawezekana Warioba pia anapenda serikali mbili, ila wananchi wanataka serikali tatu. Kuna ubaya gani Warioba akisema maoni ya watu. Na huyu RizMoko ni nani mpaka apewe attention namna hii? haka karedio kumbe nako ka kisengenye, ndo nimejua leo.
 
Siamini kama maneno hayo yametoka kinywani wa mtoto wa rais, kama ni kweli basi kuna kakikundi kadogo kamefanya nchi hii ka familia yao! Inazewekanaje mtoto amabaye ni Warioba ni kama babu yake aseme anpayuka? Nani kampa kiburi cha kuropoka na kutukana waasisi wa nchi hii? Anadhani baba yake ataishi Ikulu milele? Mbona hatujawhi kumuona Dr Hussein Mwinyi akikosa adabu namna hii?
 
Na huyu RizMoko ni nani mpaka apewe attention namna hii? .
tatizo la nchi za kiafrika, baba akiwa Rais basi mtoto naye ni Rais mama pia ni Rais - kazi tunayo.
 
Haya, sema wewe kasema kweli? Yawezekana Warioba pia anapenda serikali mbili, ila wananchi wanataka serikali tatu. Kuna ubaya gani Warioba akisema maoni ya watu. Na huyu RizMoko ni nani mpaka apewe attention namna hii? haka karedio kumbe nako ka kisengenye, ndo nimejua leo.

Amesema ndoto zake ni kuwa Katibu mkuu wa Ccm Taifa…
So amesema kama katibu mkuu mtarajiwa! Ha haaa ha ha
 
ccm hakuna mtu mzima hata mmoja,kuna mwingine karipotiwa kuleofm kuwa ni shoga na inavyoelekea kwa akili zao kuna tatizo zaidi ya tujuavyo.
 
Kwenye waraka wa Mwalimu Nyerere "TUJISAHIHISHE" alioutoa Dar es Salaam May 1962 akiwalenga viongozi na wanachama wa TANU mojawapo wa maelekezo yake namnukuu ...." haifai kuchagua kiongozi kwa sababu ni mjomba, au ni binamu au ana sauti au ana sura nzuri.....jambo kubwa ni kuchagua kiongozi mwenye tabia nzuri na anayeiweza kazi..." Nafikiri viongozi wa serikali na chama cha mapinduzi wamelifumbia macho hili ndiyo maana wanateua hata girlfriends zao kwenye nafasi ambazo si kutokuziweza tu bali ni kuwafanya walioteuliwa kubainika ujuha wao! Quote me!
 
Back
Top Bottom