Kwa wale ambao wamefika chuo kikuu na kupata angalau shahada moja, hemu tuwe mstari wa mbele kusaidia wale ambao hawakupata elimu.
Ndugu zangu, katika kukusanya maoni ya watu, kuna njia mbalimbali hutumika, na matumizi ya njia hizo ndio zitapelekea uhalali wa data zilizopatikana na hivyo matokeo ya tafiti.
Kwa njia alizotumia Warioba na vibaraka wake, ni wazi kuwa "data" zake hazina uhalali wowote kwa kuwa sio data za kisayansi.
Mtafiti hawezi kukusanya maoni ya kajikundi fulani cha wananchi (ambacho labda kanataka serikali 3) halafu aje ahitimishe kuwa wananchi wanataka serikali tatu. Huo ni wendawazimu.
Yeye kama mwenyekiti wa tume akupaswa ku-generalize, angesema tu kwa mujibu wa data, idadi hii ilitaka hivi, hiyo ilitosha. Ila sio kudanganyana kuwa Watanzania tunataka serikali tatu kwa kutumia maoni ya watu 30,000.
Hata standards za sampling pekee zinatosha kuikataa rasimu ya Warioba.