Rais William Ruto (Kenya) Amjibu Rais Samia Suluhu Hassan (Tanzania) baada ya kutoa kauli ya kuwabagaza na kuwadharau Wakenya..

The Palm Beach

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2015
Posts
3,611
Reaction score
9,269

View: https://youtu.be/tarwA0cZbcI?si=Wizm2OyFYriZzJzg
View: https://youtu.be/LI58lCwODxQ?si=3O5x8UYnDDmWtSL7
#Kwa wachunguzi wa mambo, wanaona moja kwa moja kuwa kauli hiI ya Rais Ruto imemlenga kumjibu Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania baada ya kauli yake ya wiki hii iliyoonekana kuwalenga wakenya kusema kuwa;

".....wameshindikana kwao, wameharibu amani ya nchi yao na hivyo wasije huku Tanzania kutuvuruga na kuvuruga amani yetu..." Rais Samia Suluhu Hassan
#Lakini Rais William Ruto akiwa so calm, carefully and diplomatically ktk matamshi yake anajibu kusema"

"...Taifa letu la Kenya ni taifa zuri sana, taifa la ajabu, taifa kuu hapa duniani. Hebu asitokee yeyote kuwaambia juu ya mambo hasi (negative things) kuhusu ninyi na taifa/nchi yenu..."; Rais William Ruto​
 
Mama alichemka, hatuwezi mtetea kwa kauli ile. Akili ndogo sana ilitumika kuwakabili akina Mwangi. Hakuna Rais atafurahia raia wake apigwe na aje atupwe mpakani.
Wala hakuna Raisi ataambiwa mchi yake imeharibiwa, akakenua meno tuu.
 
Mama alichemka, hatuwezi mtetea kwa kauli ile. Akili ndogo sana ilitumika kuwakabili akina Mwangi. Hakuna Rais atafurahia raia wake apigwe na aje atupwe mpakani.
Wala hakuna Raisi ataambiwa mchi yake imeharibiwa, akakenua meno tuu.
Kwani wangewaacha waudhurie mahakamani na kuondoka kwani kungetokea madhara yeyote?
 
Kwahio WA kwetu karopokwa? Hana diplomatic language?
 
Havina uhusiano. Hiyo kauli ni ya siku ya jamhuri December 12, 2024.
Imeunganishwa tu kwa dhumuni maalum.
 
Tulisema hapa JF, ile kauli ya Samia haikuwa kauli sahihi kuhusu wakenya, kidiplomasia ilikuwa ni kauli ya kulishambulia taifa nzima la Kenya. Hakupaswa kufanya vile. Mama yetu aliteleza.
Yes ilikuwa na dharau ndani yake.
Ila hiyo hapo juu ni ya December
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…