Rais wetu yuko wapi tena? Kagera hayuko Zambia hajaenda

Rais wetu yuko wapi tena? Kagera hayuko Zambia hajaenda

Kwi kwi kwi kwi kwi lol! Ungekuwa kama si mpumba.vu usingeandika pumba na kujibaraguza kwamba unanifahamu wakati hunijui sikujui. Achana na tabia ya kudandia dandia watu mitandaoni. Mind your own business.

I can't argue with a fool
 
Hafanyi kazi kama mlivyozoea...Sio mtu wa selfie kama wale wengine!!!
Kwani maandiko yanasema..."na pale mpatwapo na yale yaletayo maafa na njaa ni wakati wa kutulia na kusaidiana" andiko halijasema mfanye selfie na kuutangazia uma.
 
Hafanyi kazi kama mlivyozoea...Sio mtu wa selfie kama wale wengine!!!
Kwani maandiko yanasema..."na pale mpatwapo na yale yaletayo maafa na njaa ni wakati wa kutulia na kusaidiana" andiko halijasema mfanye selfie na kuutangazia uma.
Ni kweli, na sasa janga limetupata, U-WAPI MSAADA?
 
Umesahau tuliambiwa kuna watu wameficha pesa?
Huwezi jua anafanya nini sasa!
 
Hivi kwani ameshamaliza kuteua? naona tangu jana sioni taarifa kutoka kwa msigwa khs uteuzi
 
Ebu watanzania tuache unafiki,Rais akiongea mnamponda mnasema anaibua hasira,akikaa kimya mnamtafuta ili aongee,ila ninegundua kitu kimoja kua kua hao wanaomponda huwa pia wanampenda kimya kimya ndo maana asipo ongea au akipotea kwenye media wana muulizia sana..
Mkuu Akade,upinzani sio huo,ni kufuatilia kwa karibu weakness za mtawala na serikali yake na kumsemelea kwa wananchi hilo ndilo jambo kubwa kupita yote akifanya mazuri haituhusu anatimiza alichoahidi wa wananchi.Hili la kuhoji uwepo wake BK ndio fitna za siasa zenyewe si aliahirisha safari??yuko wapi we rudi kwa JK likitokea jambo kubwa kama hilo utamwona huyu hapa.Hao wote chama kimoja ilani ya chama moja.
 
Ndugu yangu acha kuanzisha thread za majungu unataka kufitinisha tu yani hiyo ndo kazi yenu.

Mwenyekiti CCM JF
Mnapeana vyeo tu kisa posho za buku 7 punguzeni njaa vijana fanyeni kazi
 
JPM ni kiongozi wa action. Huwezi enda sema poleni huku watu wamelala njaa na wengine wamelala nje ya nyumba zao kwa hofu ya kuangukiwa. Ngosha akiingia hapo mahema yote tupa kule, JKT wanapewa saa saba tu nyumba za gharama nafuu ziote ka uyoga. Mark ma words. Shule si zimefungwa mpaka 26 Sept?? Wadhani muda huomkandarasi wa kurepea atalala usingizi?? Kazi ka mchwa tu.
Hatutaki ngonjera, twataka Hapa Kazi Tu. Ngonjera 2020
Safi sana umemaliza Mkuu! Sio watu wanaenda kupiga selfie tu huko hamna la maana!
 
Tuliambiwa kaahirisha shughuli na ziara za kimataifa ili ashighulikie janga la tetemeko la ardhi Bukoba na Mwanza, Lakini huku Bukoba Hatujamwona/Hajafika!!
Subiri kidogo anakuja Kwa njia ya barabara atafika tu!! Hapa kazi tu ebo!!
 
Nimeshasema tangu asubuhi, katika hili tunaiona tofauti ya wazi ya JK na JPM kiuongozi! JK anahuruma sana yule baba, na anauwezo mkubwa wa kumobilize resource kwa haraka! hakuwa mtu wa kujifungia ndani

Alitukanwa akaitwa 'Vasco Dagama' kwa kutojifungia ndani.
 
Leo ni siku ya 5 tangu tetemeko la Ardhi litokee mnamo tarehe 10/9/2016 kule Bukoba, Kagera. Nilitegemea Rais JPM wa JMT angelikuwa miongoni wa viongozi wa kwanza kabisa kufika kwenye eneo la tukio lakini mpaka sasa kimyaaaaaaaaaaaa!!! Nini kinaendelea?

Nauliza tu. Kwanza tulisikia ametoa pole kwa Mkuu wa Mkoa wa KAGERA na baadaye kufuatiwa na taarifa kuwa ameahirisha safari ya kuhudhuria kuapishwa kwa Rais Mteule wa Zambia Bwana Edgar Lungu.

Nimekuwa nikifuatilia iwapo nitasikia Rais JPM ametembelea Bukoba kujionea athari za tetemeko pamoja na kuwapa pole Wananchi wa Bukoba mjini na maeneo mengine lakini kimyaaa!

Ukija kwenye media zetu hasa TBC,both TV&Radio nako kimyaaa! Coverage ya matukio ya tetemeko la Kagera haijatetendewa haki na media zetu kabisa. Lakini cha ajabu ukisikiliza BBC wanafuatilia kwa karibu sana na wanatoa update za mara kwa mara.

Wapi TBC, Wapi ITV na hasa StarTV ambao wako jirani na eneo la tukio lakini hakuna wanachoripoti pamoja na kusaidia sana coverage za JPM wakti wa Kampeni 2015 kwa sasa kimyaaaaaa!!!

Nini kinaendelea? Nauliza tu. Je, yawezekana JPM ana ile inaitwa GUILTY CONSCIUONESS ya maneno aliyowatamkia Wasukuma wenzake wa Kahama kuwa Seriklai yake haiwezi kuwajengea Wananchi waliopatwa na maafa ya kungukiwa nyumba zao baada ya mvua kubwa mwaka mwanzoni mwa 2015!

Je, inawezekana ndiyo maana kamtuma Kiranja wake Mkuu Majaliwa wa Majaliwa kutembeza Bakuli kwa Wafanyi biashara ili watafute michango ya kuwajengea Wana Bukoba nyumba kwa hela hiyo maana Serikali yake haitaki kutumia fedha kuwasaidia Wananchi wake?

Nauliza tu.
 
Magufuli anawanyima raha sana. Kitengo cha Maafa kipo chini ya Waziri Mkuu. Waziri Mkuu ameshafika eneo la tukio na kila kitu kinaenda sawa. Nini kinawawasha?
 
Back
Top Bottom