Rais wetu yuko wapi tena? Kagera hayuko Zambia hajaenda

Rais wetu yuko wapi tena? Kagera hayuko Zambia hajaenda

mkuu utatumbukizwa kisimani...
unywe maji mpaka ushibe [emoji12]
 
Mkuu nadhani umeamua tuu kuandika ila Rais kupitia Ofisi yake ya habari alielezea tukio hilo na kutoa pole kwa wote walofikwa na majanga hayo kupitia Mkuu wa Mkoa wa Kagera na ilikuwa Taarifa rasmi ya Ikulu Mkuu...
Hiyo ilikuwa hata kabla ya safari ya Zambia. Sasa baada ya kuahirisha wanananchi walitegemea awe kafika kule kwenye tukio na kauli yake kama mkuu wa nchi ilikuwa muhimu. Kablaya kuanza kuchangisha watu ilikuwa bora serikali ianze kupitia bajeti ya maafa unless waseme imeisha lakini majuzi aliwaambia wakazi pale magomeni kuwa serikali yake ni tajiri!
 
Kwenye kupatwa kwa jua Habari Leo waliandika, KUPATWA KWA JUA NI ISHARA YA MUNGU KUMKUBALI RAIS Sasa kwenye hili tetemeko sijui watasema ni ishara ya nini?
Nukuu:
Katibu wa Mila wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, Mwanasimtwa Mwagongo, amesema tukio la kupatwa kwa jua linalotarajiwa kutokea Alhamisi hii katika Kijiji cha Rujewa wilaya ya Mbarali, ni ishara ya Mwenyezi Mungu kuukubali uongozi wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli.

Akizungumza jana na waandishi wa habari, habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) nyumbani kwake katika Kata ya Isisi, Mwagongo alisema tukio hilo la kupatwa kwa jua nchini si mkosi, bali ni sawa na taa iliyokuwa imezimika na sasa imewashwa na kuongeza, hii ishara kuwa Mungu ameukubali utawala uliopo madarakani na ndiyo sababu ametoa giza na kuleta nuru.

“Hapo zamani watoto walikuwa hawaruhusiwi kutoka nje siku ya tukio hili, Wazee waliamini ni ajali ya kugongana jua na mwezi na wanaoumia ni wanadamu hasa watoto kwa kusababishiwa milipuko ya magonjwa mbalimbali,” alisema.

“Lakini kwa sasa tunatambua kuwa ni tukio la kisayansi na kutokea kwenye eneo letu ni neema kutoka kwa Mungu. Kupitia tukio hili dunia itaijua Tanzania, itaijua Mbarali na itaijua Rujewa. Ni tukio ambalo limetutangaza”.

Aidha Mwagogo alisema baada ya tukio hilo, wazee wa kimila watachinja ng’ombe kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa neema ya tukio hilo na pia kumwomba aiepushe jamii na madhara yoyote yanayoweza kujitokeza.

Aliwaasa viongozi wa dini zote kote nchini kuliombea tukio hilo ili lifanyike na kupita kwa amani na pasiwepo na uvunjifu wa amani utakaosababisha jamii kutoa tafsiri ya tofauti baada ya tukio hili la kihistoria ambalo litafanyika kati ya saa 4.15 asubuhi hadi saa 8.00 mchana.

Chanzo: Habari leo
 
Rais John Pombe Magufuli alighairi safari ya zambia ili aende Kagera kwenye maafa ya tetemeko. Lakini sijaona akiongea na taifa wala sijamwona live katika tukio hilo. Je mikakati ya kuwasaidia waathirika inafanywa kimya kimya, kama katuma wawakilishi kulikua na haja gani kuahirisha safari ya Zambia?

Lile tukio kubwa sana halikuwa la kiongozi mkuu kukaa kimya. Zaidi sana aliacha shughuli zingine ili ashughulikie maafa haya, yuko wap? Ikulu sio sehemu ya maafa yampasa afike eneo la tukio. Vingenevyo tutaamini alisitisha safari ya Zambia kwa kazi zingine na sio kuhudumia wahanga. Timu ya kupanga utendaji wa maafa ipo, sijui yeye mikakati ganu inamfanya ajifungie.

Please rais wetu nenda kawahudumie wahanga.

Rais wangu uko wapi Zambia, Magogoni au kagera?
Mara mmekwishammiss eeh! Anafanya mikakati ya kuhudumia wahanga wa tetemeko la ardhi.
 
Dah, urais ni mzigo, sielewi kwa nini ENL alikuwa anaukimbilia kwa nguvu zote, sasa hapa kila afanyalo JPM lazima akosolewe na kuulizwa maswali.

Rais wa mioyo yenu yuko kenya, hivi toka wiki sasa hajafika bukoba,??
Nakumbuka yeye ndiye aliyeanza kwenda kisha akaenda Kenya
 
Ila taifa silina viongozi wakuu watatu?w/mkuu ameshaiwakilisha serikali
 
Yaani hata hujui idara ya maafa IPO chino ya ofisi ya nani. Jiongeze kabla ya kukoment mkuu.


Kwani nchi nyingine maafa yanapotokea na rais kuchukua jukumu la kuyashughulikia au hata kutembelea wahanga unadhani nchi hzo hazina idara ya maafa???we ndo unatakiwa kujiongeza na kujua kuwa Mkuu wa nchi wajibu wake ni nn???kitu ambacho hujui na yeye inaelekea hajui...neo moja tu la faraja kwa wahanga Kutoka jwa rais wao linatosha sana..
 
Hiyo ilikuwa hata kabla ya safari ya Zambia. Sasa baada ya kuahirisha wanananchi walitegemea awe kafika kule kwenye tukio na kauli yake kama mkuu wa nchi ilikuwa muhimu. Kablaya kuanza kuchangisha watu ilikuwa bora serikali ianze kupitia bajeti ya maafa unless waseme imeisha lakini majuzi aliwaambia wakazi pale magomeni kuwa serikali yake ni tajiri!
Sawa Mkuu amesikia ataenda
 
Akiiongea mnamsema ya kuwa anaongea SANA na apunguze, akikaa KIMYA napo mnamsema pia mbona haongei...!

Afanye nini mridhike?!

Watanzania bhana!

Kwa issue ya Tetemeko nafikiri amemwagiza W/mkuu achukue hatua.

Sio lazima atoke kwenye media. Nafikiri ataenda Kagera soon..!
Kagera soon ndio wapi?
 
Ana kazi nyingi za kulitumikia taifa,wacha uchochezi
 
Tikatika wewe ni mchochezi unataka kujua Mkulu yupo wapi ili iweje? Kama ni Kagera Si MAJA alienda sasa shida iko wapi? Zambia hakuenda ndio we inakuhusu nini? Je kama kaishiwa anatafuta za kuja kutaftia kiki.
 
Rais John Pombe Magufuli alighairi safari ya zambia ili aende Kagera kwenye maafa ya tetemeko. Lakini sijaona akiongea na taifa wala sijamwona live katika tukio hilo. Je mikakati ya kuwasaidia waathirika inafanywa kimya kimya, kama katuma wawakilishi kulikua na haja gani kuahirisha safari ya Zambia?

Lile tukio kubwa sana halikuwa la kiongozi mkuu kukaa kimya. Zaidi sana aliacha shughuli zingine ili ashughulikie maafa haya, yuko wap? Ikulu sio sehemu ya maafa yampasa afike eneo la tukio. Vingenevyo tutaamini alisitisha safari ya Zambia kwa kazi zingine na sio kuhudumia wahanga. Timu ya kupanga utendaji wa maafa ipo, sijui yeye mikakati ganu inamfanya ajifungie.

Please rais wetu nenda kawahudumie wahanga.

Rais wangu uko wapi Zambia, Magogoni au kagera?
Kama hujamuona LIVE basi itakuwa ni kubana matumizi subiri saa tano!!!
 
The president is busy with national issues. Earthquake is an international issue.
 
Back
Top Bottom