Magufuli anawanyima raha sana. Kitengo cha Maafa kipo chini ya Waziri Mkuu. Waziri Mkuu ameshafika eneo la tukio na kila kitu kinaenda sawa. Nini kinawawasha?
Hafanyi kazi kama mlivyozoea...Sio mtu wa selfie kama wale wengine!!!
Kwani maandiko yanasema..."na pale mpatwapo na yale yaletayo maafa na njaa ni wakati wa kutulia na kusaidiana" andiko halijasema mfanye selfie na kuutangazia uma.
Aende ili iweje mkuu? Atambue tu tushaachana naye kabisa wala asishindwe kula ugari wake akaiwazia Kagera. Na sahivi tuna gazeti letu la Hamasa, ni bora kulitegemea lile kuliko kutegemea vya wengine, kila mmoja atalingia chake. ....hii ndo Tz.Leo ni siku ya 5 tangu tetemeko la Ardhi litokee mnamo tarehe 10/9/2016 kule Bukoba, Kagera. Nilitegemea Rais JPM wa JMT angelikuwa miongoni wa viongozi wa kwanza kabisa kufika kwenye eneo la tukio lakini mpaka sasa kimyaaaaaaaaaaaa!!! Nini kinaendelea?
Nauliza tu. Kwanza tulisikia ametoa pole kwa Mkuu wa Mkoa wa KAGERA na baadaye kufuatiwa na taarifa kuwa ameahirisha safari ya kuhudhuria kuapishwa kwa Rais Mteule wa Zambia Bwana Edgar Lungu.
Nimekuwa nikifuatilia iwapo nitasikia Rais JPM ametembelea Bukoba kujionea athari za tetemeko pamoja na kuwapa pole Wananchi wa Bukoba mjini na maeneo mengine lakini kimyaaa!
Ukija kwenye media zetu hasa TBC,both TV&Radio nako kimyaaa! Coverage ya matukio ya tetemeko la Kagera haijatetendewa haki na media zetu kabisa. Lakini cha ajabu ukisikiliza BBC wanafuatilia kwa karibu sana na wanatoa update za mara kwa mara.
Wapi TBC, Wapi ITV na hasa StarTV ambao wako jirani na eneo la tukio lakini hakuna wanachoripoti pamoja na kusaidia sana coverage za JPM wakti wa Kampeni 2015 kwa sasa kimyaaaaaa!!!
Nini kinaendelea? Nauliza tu. Je, yawezekana JPM ana ile inaitwa GUILTY CONSCIUONESS ya maneno aliyowatamkia Wasukuma wenzake wa Kahama kuwa Seriklai yake haiwezi kuwajengea Wananchi waliopatwa na maafa ya kungukiwa nyumba zao baada ya mvua kubwa mwaka mwanzoni mwa 2015!
Je, inawezekana ndiyo maana kamtuma Kiranja wake Mkuu Majaliwa wa Majaliwa kutembeza Bakuli kwa Wafanyi biashara ili watafute michango ya kuwajengea Wana Bukoba nyumba kwa hela hiyo maana Serikali yake haitaki kutumia fedha kuwasaidia Wananchi wake?
Nauliza tu.
Akienda mnalalamika eti anaenda sababu ni kwao. Wapuuzi sana nyie
Duh! Huku sasa ni kuchanganyikiwa.Aende ili iweje mkuu? Atambue tu tushaachana naye kabisa wala asishindwe kula ugari wake akaiwazia Kagera. Na sahivi tuna gazeti letu la Hamasa, ni bora kulitegemea lile kuliko kutegemea vya wengine, kila mmoja atalingia chake. ....hii ndo Tz.
Ndio akili yako imefikia hapo? Kweli machadema yote ni kama yamewehuka. Ni mangapi Serikali inafanya kwa ajili ya wana Bukoba? Kama Serikali itaamua kubinya majimbo yenye wapinzani mtapata kitu? Na kwa nini Rais afanye hivyo ilhali amechaguliwa mpaka na wana CHADEMA?Acha ujinga wewe. Lini kumetokea maafa huko kwao akaenda na watu wakalalamika?Mbona mijitu mliolewa maji ya bendera za kijani mnapayuka tu kama walevi?
Ukikubali kuwa Rais lazima uwe na hekima na busara na huwezi kuwa biased na eneo lolote bila kujali unatokea jimbo gani. You must be president of all!
Najua kinachomfanya JPM asifike Bukoba, kisa ni kwa vile BUKOBA NI JIMBO LINALOONGIZWA NA CHADEMA/UKAWA!!!
Ukisha kuwa na Rais mwenye mawazo kama hayo ni janga la kitaifa!!
Mmetuchanganya wenyewe halafu mnageuka kutushangaa kuchanganyikiwa. Kipi hukukielewa?Duh! Huku sasa ni kuchanganyikiwa.
kwani akienda ndio nini kitabadilikaTuliambiwa kaahirisha shughuli na ziara za kimataifa ili ashighulikie janga la tetemeko la ardhi Bukoba na Mwanza, Lakini huku Bukoba Hatujamwona/Hajafika!!
Hivi wazimbabwe wanawasiliana kwa lugha gani vile?Sasa kulikuwa na haja gani kuahirisha safari?
Wataka kusema Obama, na marais wengine dunian wanafika kwenye maafa kama hayo huwa hawana wasaidizi au tz iko tofaut na nchi nyingineUbinadamu upi unaoutaka wewe? Sehemu ya kazi si Waziri Mkuu kamuwakilisha tayari.Madaktari kutoka bugando wameenda kutoa tiba kwa wahanga.Na Serikali bado inatoa mahitaji kwa wahanga.
Kwahiyo Majaliwa ndio akafe kiboya?Taarifa zinasema bado kuna uwezekano wa tetemeko kuendelea kutokea, unataka aende ili likitokea na yeye afe?