Rais wetu yuko wapi tena? Kagera hayuko Zambia hajaenda

Rais wetu yuko wapi tena? Kagera hayuko Zambia hajaenda

Watanzania wana yao mambo......wengine wanasema ya ajabu na ya uzushi mpaka Mashetani wanashangaa.
 
Mkuu nadhani umeamua tuu kuandika ila Rais kupitia Ofisi yake ya habari alielezea tukio hilo na kutoa pole kwa wote walofikwa na majanga hayo kupitia Mkuu wa Mkoa wa Kagera na ilikuwa Taarifa rasmi ya Ikulu Mkuu...
Ile ya kutoku testiwa aliinena live live lakin
 
Hopeless
Mwenyekiti CCM JF
Kati yangu na wewe nani hopless?! wewe mwenyekiti hewa ndio hovyo kabisa, umeona nafasi zimjaa hukukumbukwa ukaamua ujipe ya uenyekiti chama chakavu humu jf?! endelea kuwa hewa maana hii ndio sera ya awamu ya tano.
 
Wakati mwingine matatizo tunajiletea wenyewe kwa mambo yasiyo na msingi , haya ngoja hii post isambae kwenye groups za whatsaap , sijui utajibu nini? Mkuu

Tusipende kujitaftia matatizo , kumzushia rais wa nchi ni mgonjwa ni kuleta tension katika nchi
 
Muda utawaumbua wana ccm. Siku akienda mtaanza kutubeza tunaomshauri aende na kusema tumeumbuka. Badala ya ninyi mnaomsifu kwa kujifungia, kama vile rais wetu anaongoza rada hana sababu ya kuonekana
 
Akienda kagera ndo nyumba zitajijenga zenyew..mbona kaenda boss wako chaajabu kaishia kucheka tuu hata mfuko wa cement hajatoa kakimbilia cjui uganda cjui kenya...anaacha msiba wa nyumbani anakwenda msiba wa nje...huyu ndo mnasema atakuwa rais..labda rais wa ufipa
 
Mgonjwa akawa anajiandaa kwenda ZAMBIA?
Ifike wakati uruhusu akili yako kufikiri tofauti na unavyofikiri.... (think outside the box)

Yaani Nenda mbali zaidi ya vile uwazavyo, na kwa kuongeza waza kuwa lile usilolikubali ndio sahihi na lile unalolikubali si sahihi.

Fikiri tofauti ya ufikirivyo.... upe ubongo nafasi ya kuruhusu fikra tofauti na fikra mpya...

Sasa fikiri
Rais haendi Zambia, wewe ndo hujielewi..
Rais aliahirisha kwenda Zambia Kwa Sababu ya maafa hayo, na atawakilishwa na makamu wa rais, hivi Kwanini nyie Lumumba ni totally insanes??!
Na wewe hapo juu, mtoa mada amehoji ukimya wa rais, na hajasema rais ni mgonjwa ila angependa kujua iwapo ukimya wa Rais ni Sababu ya ugonjwa?
Hivi vijana wa ccm huwa mna nini?
 
Amekaa ndani anapitia baadhi ya kauli zake ili kila waziri atoke na tamko kuwa mkuu alikuwa anaongea na watani zake, hata wenye njaa watapewa chakula kwa kuwa aliongea na watani, huyu Mungu huyu?! kweli si athuman wala John.
 
Kati yangu na wewe nani hopless?! wewe mwenyekiti hewa ndio hovyo kabisa, umeona nafasi zimjaa hukukumbukwa ukaamua ujipe ya uenyekiti chama chakavu humu jf?! endelea kuwa hewa maana hii ndio sera ya awamu ya tano.
Sera ya chama tawala.

Mwenyekiti CCM JF
 
Hata mm usiku nimejiuliza sana, mh yuko wapi? Nilidhani jana kwenye hiyo harambe angekuwepo lkn sikumwona.
Kuna nn kimesibu Rais wetu jamani?
 
Rais John Pombe Magufuli alighairi safari ya zambia ili aende Kagera kwenye maafa ya tetemeko. Lakini sijaona akiongea na taifa wala sijamwona live katika tukio hilo. Je mikakati ya kuwasaidia waathirika inafanywa kimya kimya, kama katuma wawakilishi kulikua na haja gani kuahirisha safari ya Zambia?

Lile tukio kubwa sana halikuwa la kiongozi mkuu kukaa kimya. Zaidi sana aliacha shughuli zingine ili ashughulikie maafa haya, yuko wap? Ikulu sio sehemu ya maafa yampasa afike eneo la tukio. Vingenevyo tutaamini alisitisha safari ya Zambia kwa kazi zingine na sio kuhudumia wahanga. Timu ya kupanga utendaji wa maafa ipo, sijui yeye mikakati ganu inamfanya ajifungie.

Please rais wetu nenda kawahudumie wahanga.

Rais wangu uko wapi Zambia, Magogoni au kagera?
Dah, urais ni mzigo, sielewi kwa nini ENL alikuwa anaukimbilia kwa nguvu zote, sasa hapa kila afanyalo JPM lazima akosolewe na kuulizwa maswali.
 
kuna siku mtataka Rais apite kila nyumba kuwasalimia sasa mnakoenda
Ni kweli sjawahi muona hata siku moja anapita kusalimia miji yetu huku mitaani kwetu, kama hivyo yaani,
Ukipishana nae njiani anataka wewe ndo ukae pembeni apite, mkiwa mezani mnakula akimaliza vya kwake anachukua vya wengine bila kuomba, pia akiwakuta mahali anasimama hasalimii hadi mumsalimie yeye halaf hawajibu anaendelea na safari zake, tena anaweza kuwajibu kwa kufyonza tu.
Kali zaidi mkiwa kwenye mazishi wakati wengine mnapokezana majembe na makoleo kufukia kaburi yeye husogea kaburini na kusogeza mchanga kidogo kwa mguu mara moja huku mikono kaweka mifkoni ktk mkoti af akitoka hapo anajikung'uta mikono kana kwamba amefanya kazi kubwa.
'watanzania tunatamani kumsema na kumchongea vibaya hivi rais wetu, uzalendo ziro'
 
Ebu watanzania tuache unafiki,Rais akiongea mnamponda mnasema anaibua hasira,akikaa kimya mnamtafuta ili aongee,ila ninegundua kitu kimoja kua kua hao wanaomponda huwa pia wanampenda kimya kimya ndo maana asipo ongea au akipotea kwenye media wana muulizia sana..
 
Mmemchoka kiasi hicho? Si mmeshaambiwa baada ya tetemeko lile kubwa yatafata mengine madogomadogo kwa ufupi ile sehem bado sio salama kwa sasa.
Sio salama kwa rais pekee au? Kuna walioenda na wakarudi na wengine wanaendelea kwenda
 
Ndugu yangu acha kuanzisha thread za majungu unataka kufitinisha tu yani hiyo ndo kazi yenu.

Mwenyekiti CCM JF
Mbona kauliza swali zuri tu mkuu, rais aliahirisha ziara yake Zambia kwa ajili ya tetemeko, ila hajaonekana wala hajasikika kuhusu tetemeko, sasa hapo kuna majungu gani?
wakihoji chochote kuhusu rais basi ni majungu au uchochezi au hawana akili?
 
Ndugu yangu acha kuanzisha thread za majungu unataka kufitinisha tu yani hiyo ndo kazi yenu.

Mwenyekiti CCM JF
Sasa na wewe hapa ndio unaongea nini? Yani watanzania tunauliza rais yuko wapi katika kipindi hili kigumu wenzetu wamepoteza maisha, wengine hawana chakula wala sehemu za kulala wewe unaita ni majungu. Mkuu hata Kama una mahaba yaliyopitiliza ni upumbavu kutetea jambo ambao lipo wazi kama hili.funua huo ubongo wako.
 
Back
Top Bottom