Rais wetu yuko wapi tena? Kagera hayuko Zambia hajaenda

BEHOLD

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2013
Posts
5,071
Reaction score
10,741
Tuliambiwa kaahirisha shughuli na ziara za kimataifa ili ashighulikie janga la tetemeko la ardhi Bukoba na Mwanza, Lakini huku Bukoba Hatujamwona/Hajafika!!

Rais John Pombe Magufuli alighairi safari ya zambia ili aende Kagera kwenye maafa ya tetemeko. Lakini sijaona akiongea na taifa wala sijamwona live katika tukio hilo. Je mikakati ya kuwasaidia waathirika inafanywa kimya kimya, kama katuma wawakilishi kulikua na haja gani kuahirisha safari ya Zambia?

Lile tukio kubwa sana halikuwa la kiongozi mkuu kukaa kimya. Zaidi sana aliacha shughuli zingine ili ashughulikie maafa haya, yuko wap? Ikulu sio sehemu ya maafa yampasa afike eneo la tukio. Vingenevyo tutaamini alisitisha safari ya Zambia kwa kazi zingine na sio kuhudumia wahanga. Timu ya kupanga utendaji wa maafa ipo, sijui yeye mikakati ganu inamfanya ajifungie.

Please rais wetu nenda kawahudumie wahanga.

Rais wangu uko wapi Zambia, Magogoni au kagera?
 
Akienda huko Bukoba na Mwanza mtaanza kumhesabia safari za kwenda kwake. Hamna maana ninyi. Bora aendelee kuratibu maafa akiwa Ikulu kwa vile kule kuna wakuu wa mikoa na wilaya wanaweza kufanya vema
 
Hiyo haitakuwa ziara bali safari ya dharula kwenda msibani!!
 
Yupo analishughulikia, analishughulikiaje? Usitake kujua maana itakuwa ni uchochezi.

Huo uchochezi uaujua wewe. Lkn Kufika kwa Raisi in person na kuwajulia wahanga hali kuna tofauti sana na kutuma watu!
 
Tuliambiwa kaahirisha shughuli na ziara za kimataifa ili ashighulikie janga la tetemeko la ardhi Bukoba na Mwanza, Lakini huku Bukoba Hatujamwona/Hajafika!!

Anasubiria zile ndege, ndio zinawasili wiki hiii
 
Akienda huko Bukoba na Mwanza mtaanza kumhesabia safari za kwenda kwake. Hamna maana ninyi. Bora aendelee kuratibu maafa akiwa Ikulu kwa vile kule kuna wakuu wa mikoa na wilaya wanaweza kufanya vema
Team TUSIONAJEMA
 
Huo uchochezi uaujua wewe. Lkn Kufika kwa Raisi in person na kuwajulia wahanga hali kuna tofauti sana na kutuma watu!
Nimeshasema tangu asubuhi, katika hili tunaiona tofauti ya wazi ya JK na JPM kiuongozi! JK anahuruma sana yule baba, na anauwezo mkubwa wa kumobilize resource kwa haraka! hakuwa mtu wa kujifungia ndani
 
Akiwa mwanza alisema Mwanza sina namna ya kuikwepa madiwan, wabunge na meya ni wa ccm sasa kwa bukoba utajaza mwenyewe......
 
Akienda huko Bukoba na Mwanza mtaanza kumhesabia safari za kwenda kwake. Hamna maana ninyi. Bora aendelee kuratibu maafa akiwa Ikulu kwa vile kule kuna wakuu wa mikoa na wilaya wanaweza kufanya vema
wewe acha sifa za ovyo jibu hoja
 
Back
Top Bottom