Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,380
- 18,750
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemshukuru na kumpongeza Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mstaafu Prof. Ibrahim Hamis Juma, kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kukuza ushirikiano wa Mahakama na mihimili mingine ya Dola ikiwemo Serikali na Bungeni ambapo Rais Samia amesema sio dhambi kwa Serikali kushirikiana na Mahakama kama baadhi ya Watu wanavyodhani.
Akiongea Jijini Dodoma leo June 15,2025 wakati akimuapisha George Masaju kuwa Jaji Mkuu mpya wa Tanzania, Rais Samia amesema "Jaji unayemaliza muda wako wa utumishi umefanya kazi kubwa sana ya kuendeleza na kuleta mageuzi ndani ya Mahakama pamoja na kushikwa mkono na Serikali lakini uongozi wako ndani ya Mahakama ndio umeleta mageuzi yale, umeandika historia na umeacha legacy kubwa na kutokana na hayo umekuza imani ya Watanzania kwa Mahakama yao, najua katika miaka mitatu mfululizo kila tukifanyiwa tathmini Duniani imani ya Watanzania kwa Mahakama yao imekuwa ikipanda ikipanda ikipanda kwahiyo tunakushukuru sana"
"Lakini pia kama ulivyosema hapa umekuza ushirikiano na mihimili mingine ya Dola, Dola inaundwa na mihimili mitatu kwa Katiba yetu Tanzania Mahakama, Bunge na Serikali sasa mihimili hii ili Dola iende vizuri mihimili hii lazima ishirikiane, sasa wale wenye tafsiri kwamba Serikali kushirikiana na Serikali ni dhambi, hapana, Mahakama haitoweza kufanya kazi zake kama haikushirikiana na Serikali"
"Nikuombee ukapumzike kwa furaha na kama alivyosema Waziri Mkuu Serikali tukihitaji kukutumia wakati wowotw turuhusu tukutumie, umestaafu ukiwa na nguvu, tusingependa kutotumia hiyo brain unayoitoa kwenye mhimili kwahiyo turuhusu tukutumie wakati wowote tukikuhitaji"
Soma, Pia