Rais Samia ateua Majaji 9 wa Mahakama ya Rufani

Rais Samia ateua Majaji 9 wa Mahakama ya Rufani

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,115
Reaction score
3,490
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Rufani. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, walioteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani ni:-

(i) Mhe. Abdi Shaaban Kagomba Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma;
(ii) Mhe. Yohane Bokobora Masara Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Arusha;
(iii) Mhe. Immaculata Kajetan Banzi Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kagera;
(iv) Mhe. Rabia Hussein Mohamed - Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar;
(v) Mhe. Cyprian Phocas Mkeha Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Biashara, Dar es Salaam;
(vi) Mhe. Yose Joseph Mlyambina Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi, Dar es Salaam;
(vii) Mhe. Imani Daud Aboud - Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma;
(viii) Mhe. Mzee Ibrahim Ibrahim - Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar; na.
(ix) Mhe. Juliana Laurent Masabo Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma.

Aidha, uapisho wa Majaji wateule wa Mahakama ya Rufani utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.

1779278366439.png

1779278379652.png
 
Halafu.wasifuate maelekezo ahanha ah
 
Kenya ataendelea kukimbiza kila sekta EAC.

Hata wawekezaji wanawekeza Kenya mitaji yao kwa amani bila wasiwasi sababu huwezi kukuta ujinga wa namna hii wa makada wa CCM wapokea maelekezo.

Ndio maana Kenya huwezi kusikia ule ujinga wa kesi za uhaini sababu hakuna simu za maelekezo bali mtu atakuwepo pale kwa taaluma yake.

Huu ni mchakato wa wazi unaorushwa live kwa majaji kuomba kwanza nafasi katika tangazo la wazi , watafanyiwa mchujo na kamati ya kijaji mchakato ni wa wazi kabisa ndio jina libaki mtu akaapishwe.

View: https://www.youtube.com/live/JYE1AdlAlRU?si=Ao2WSezzQ3w02MOJ
images (98).jpeg

images (97).jpeg
 
Daaah najua CCM na Mello mtafuta comment yangu.Nina imani hakuna kitu anainjoi chura aka kizimkazi hapo magogoni kama KUTEUA na KUTENGUA. Na yuko tayri kufanya hata mwaka miaka 5. Na si vinginevyo. Mambo ya wanainchi utamsikia hayo sio mambo yangu.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Mhe. Imani Daud Aboud - Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma;

Imani Daud Aboud - Jaji toka kuwa rais wa Mahakama ya Afrika hadi Jaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania, Kanda ya Dodoma

4 April 2022

"HII ni MAHAKAMA PEKEE INAYOSIKILIZA KESI za HAKI za BINADAMU AFRIKA" - RAIS wa MAHAKAMA ya AFRIKA JAJI IMANI ABOUD

Jaji Imani Daud Aboud rais wa Mahakama ya Afrika anafafanua suala la haki za binadamu na watu, lina uwigo mtambuka mpana sana .

Jaji Imani Aboud anasema kwa mfano hata wafanyabiashara wakifilisiwa na mamlaka za serikali kupitia amri za kufungiwa biashara, masuala ya kodi n.k wanaweza kwenda katika Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu na watu, kwani suala hilo linahusu haki za binadamu kuvunjwa kupitia wenye biashara kukosa kipato na kukabiliwa na madeni ..

1779283208974.jpeg

Lady Justice Imani Daud Aboud is a national of Tanzania. She was first elected as Judge of the African Court on Human and Peoples' Rights in July 2018. She was re-elected for a second and final term of six years in February 2021.

Bio :

Justice Imani Daud Aboud received her Bachelor of Law degree from the University of Dar es Salaam UDSM and her Master of Law degree from the International Maritime Organization.

She is a judge of the Tanzanian High Court and has held several important positions, such as that of the Assistant Director in the President’s Office (Public Service Management), and State Attorney at the Attorney General’s Chambers.

She was President of the Tanzania Women Judges Association (TAWJA) from 2015 to 2017 but now serves as a trainer in programs such as ‘Sextortion’.

Justice Imani Daud Aboud was one of the founders of the Commission for Human Rights and Good Governance (CHRAGG) in Tanzania and was a member of the Tanzanian task force behind the Local Government reform and Labour Law Reforms.

She has also represented her government in many different human rights conferences and has written reports on Human Rights to the UN and other international monitoring bodies such as the African Commission on Human and Peoples’ Rights.

Justice Aboud has also served as Vice-Chairperson to the Independent Review Electoral Commission in Kenya, a commission created to review the election process in the country.

Justice Iman Daud Aboud represented Africa on the International Association of Women Judges’ (IAWJ) Board of Directors and is a member of the Monitoring Team in the United Nations Mechanism for the International Criminal Tribunal (MICT), where she handled Rwandan genocide cases.

Justice Iman Daud Aboud was a Monitor in two court proceedings related to the Jean Ukwinkindi case in Rwanda in April 2015.

Justice Iman Daud is also on the Advisory Board for the Southern African Development Community’s (SADC) Citizen for Justice branch based in Malawi.

Source : AfCHPR Judges | African Court Coalition
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Rufani. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, walioteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani ni:-

(i) Mhe. Abdi Shaaban Kagomba Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma;
(ii) Mhe. Yohane Bokobora Masara Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Arusha;
(iii) Mhe. Immaculata Kajetan Banzi Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kagera;
(iv) Mhe. Rabia Hussein Mohamed - Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar;
(v) Mhe. Cyprian Phocas Mkeha Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Biashara, Dar es Salaam;
(vi) Mhe. Yose Joseph Mlyambina Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi, Dar es Salaam;
(vii) Mhe. Imani Daud Aboud - Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma;
(viii) Mhe. Mzee Ibrahim Ibrahim - Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar; na.
(ix) Mhe. Juliana Laurent Masabo Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma.

Aidha, uapisho wa Majaji wateule wa Mahakama ya Rufani utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.

Nawatakia kila la kheri kwa majaji wote wateule 🐒
 
20 May 2026
Imani Daud Aboud - Jaji toka kuwa rais wa Mahakama ya Afrika hadi Jaji wa Mahakama Rufani ya Tanzania, Kanda ya Dodoma

1779283837744.jpeg

Mheshimiwa Jaji Imani Daud Aboud ni raia wa Tanzania. Alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Jaji wa Mahakama ya Afrika kuhusu Haki za Kibinadamu na Watu mnamo Julai 2018. Alichaguliwa tena kwa muhula wa pili na wa mwisho wa miaka sita mnamo Februari 2021.

Wasifu:

Jaji Imani Daud Aboud alitunukiwa Shahada ya Kwanza ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM na Shahada ya Uzamili ya Sheria kutoka Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Majini.

Yeye Imani Daud Aboud ni jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na amewahi kushika nyadhifa kadhaa muhimu, kama vile Mkurugenzi Msaidizi katika Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), na Mwanasheria wa Serikali katika Chamber ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Jaji Imani Daud Aboud likuwa Rais wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) kuanzia 2015 hadi 2017 lakini sasa anahudumu kama mkufunzi wa programu kama vile ‘Sextortion’.

Jaji Imani Daud Aboud alikuwa mmoja wa waanzilishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) nchini Tanzania na alikuwa mjumbe wa kikosi kazi cha Tanzania kilichosimamia mageuzi ya Serikali za Mitaa na Maboresho ya Sheria ya Kazi.

Pia amewakilisha serikali yake katika mikutano mingi tofauti ya haki za binadamu na ameandika ripoti kuhusu Haki za Kibinadamu kwa Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa ya ufuatiliaji kama vile Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu.

Jaji Aboud pia amewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Mapitio / Reforms / Review ya Uchaguzi nchini Kenya, tume iliyoundwa kuchunguza mchakato wa uchaguzi nchini humo.

Jaji Iman Daud Aboud aliiwakilisha Afrika katika Bodi ya Wakurugenzi ya Chama cha Kimataifa cha Majaji Wanawake (IAWJ) na ni mjumbe wa Timu ya Ufuatiliaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya Umoja wa Mataifa (MICT), ambapo alishughulikia kesi za mauaji ya kimbari ya Rwanda.

Jaji Iman Daud Aboud alikuwa Mfuatiliaji katika kesi mbili za mahakama zinazohusiana na kesi ya Jean Ukwinkindi nchini Rwanda mwezi Aprili 2015.

Jaji Imani Daud Aboud pia yuko katika Bodi ya Ushauri ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) tawi la Haki yenye makao yake nchini Malawi
Source: AfCHPR Judges | African Court Coalition
 
Abdi Shaaban Kagomba Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma;

Jaji Abdi Shaaban Kagomba aitupilia mbali kesi ya Kaiza Bubelwa

The High Court, presided over by Judge Abdi Shaaban Kagomba, has dismissed a petition challenging the 2025 Electoral Code of Conduct. In the ruling issued on July 11, 2025, the court states that only political parties, candidates, the government, and the National Electoral Commission are the primary stakeholders with the legal standing to contest the regulation.

The petition was filed by two citizens, Kumbusho Kagine and Bubelwa Kaiza, who had requested the court to temporarily suspend the implementation of the code until a full judicial review
 
Majaji wa Tanzania ni kama mahouseboy wa Rais tu anawafinyanga anavyotaka, hakuna mahakama Tanzania
Hukumu za mahakama hazitekelezeki chini ya utawala wa chama doka kongwe CCM

TOKA MAKTABA:

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Masijala Kuu Dodoma imeamuru Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kutoa fursa kwa mgombea urais kupitia tiketi ya ACT Wazalendo, Luhaga Mpina kurudisha fomu na mchakato wa kupokea uendelee pale ulipoishia Agosti 27, mwaka huu.

View: https://m.youtube.com/watch?v=AxTT0QN_li0
Uamuzi huo umetolewa mahakamani hapo na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Abdi Kagomba, Jaji Evaristo Longopa na Jaji John Kahyoza lilipopelekwa kwa ajili ya hukumu.

Katika kesi hiyo walalamikaji ni Bodi ya Wadhamini waliosajiliwa wa ACT Wazalendo na wa pili ni Mpina dhidi ya INEC na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Msingi wa kesi hiyo ilidaiwa kuwa chama hicho kilichukua hatua kutokana na uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa kubatilisha uteuzi wa Mpina kuomba kuteuliwa na INEC kuwa mgombea urais wa chama hicho, na wa INEC kumzuia kurejesha fomu yake ya kuomba uteuzi aliyokabidhiwa awali kuijaza.

SOMA: Mpina aenguliwa kugombea urais

Awali, akisoma uamuzi huo, Jaji Kagomba amesema wapeleka maombi waliwasilisha maombi tisa ambayo mahakama iliangalia katika viini vitatu, cha kwanza kikiwa ni iwapo INEC ilivunja Ibara ya 74 (11) ya Katiba ya Tanzania kwa kumzuia Mpina kurudisha fomu.

Waombaji pia waliiomba mahakama itoe tamko kwamba kitendo cha INEC kufanya hivyo baada ya kupokea barua ya msajili ni kupoteza uhuru wake kwa kufuata kifungu tajwa ambacho kinaitaka ifanye kazi na majukumu yake bila kupangiwa na taasisi au chama chochote.

Jaji Kagomba amesema kiini cha pili ni mahakama iangalie kitendo cha INEC kumzuia Mpina kurudisha fomu bila kupewa nafasi ya kusikilizwa kilivunja haki ya msingi ya wapeleka maombi kusikilizwa.

Amesema pia mahakama inaangalia wadaiwa wana haki gani, akizingatia ombi la mpeleka maombi namba mbili la kuitaka INEC kumlipa Sh milioni 100 kama fidia ya athari waliyosababisha kwa Mpina.

Amesema pia wapeleka maombi katika mawasilisho yao walidai zuio lilifanyika kinyume cha sheria kabla ya muda wa kufanya hivyo haujafika, pia waliomba mahakama itoe amri ya kuendelea na mchakato.

Kwa upande wa wajibu maombi ambao ni INEC ulidai ulifanya uamuzi baada ya kubaini mgombea alikuwa hana sifa, hivyo kusema ilipokea maelekezo hayo ni maoni na hisia tu, pia walitupa wenyewe haki yao ya kusikilizwa kwa kutopinga uamuzi wa INEC.

Baada ya hayo, Jaji Kagomba amesema mahakama imeona baada ya kupitia barua iliyotoka kwa msajili hawakuona neno lolote lililokuwa linatoa amri kwa INEC, hivyo mahakama haiwezi kutumia maoni na hisia kufanya maamuzi.

“Na sisi tunaona jaji mwenzetu kwenye kesi tulizotumia kwamba kwa kuwa barua haikutoa maelekezo au amri tunashindwa kuamua kuwa INEC iliamua kwa kufuata yale yaliyoandikwa na Msajili yalikuwa ni maelekezo na si amri hivyo tume ilikuwa na uhuru,” amesema Jaji Kagomba.

Katika suala la walalamikaji kudai kutosikilizwa mahakama ilisema inakubaliana na hilo kuwa maamuzi yalifanywa bila walalamikaji kupewa fursa ya kusikilizwa, INEC ilifanya uamuzi ambao umeathiri waombaji, hivyo ilifanya uamuzi kinyume cha katiba inavyoelekeza.

Kwa kuzingatia hilo, mahakama imetoa amri kwa kuwapa waombaji fursa ya kuwasilisha fomu za mgombea huyo na mchakato wa kuzipokea uendelee pale mchakato ulipoishia Agosti 27, mwaka huu.

Kuhusu gharama, amesema zitabebwa na kila upande, hivyo kuhusu hoja ya muombaji wa pili kulipwa Sh milioni 100 mahakama imelikataa.

Akizungumzia hukumu hiyo, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji Jacobs Mwambegele amesema watafuata uamuzi wa mahakama.

“Labda kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali akikata rufaa tutasubiri, lakini kwa sasa tutafuata uamuzi wa mahakama,” amesema.

Kwa upande wake, Naibu Mwenezi Taifa wa ACT Wazalendo, Shangwe Ayo amesema, “Baada ya kupata taarifa
rasmi ya hukumu tutaipeleka tume na wao watatupangia tarehe ya kurudisha fomu kwa mgombea wetu wa urais
na tutaanza kampeni”.
Na Ramla HamiduSeptember 12, 2025
 
umetolewa mahakamani hapo na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Abdi Kagomba, Jaji Evaristo Longopa na Jaji John Kahyoza lilipopelekwa kwa ajili ya hukumu.

Maamuzi kutoka juu kwa kupitia simu yana nguvu kuliko hukumu za majaji wa Mahakama za Juu

Sep 11 2025
🔴#Live: KESI ya LUHAGA MPINA na ACT WAZALENDO VS INEC na AG - ASHINDA KESI ya KUGOMBEA URAIS...

View: https://m.youtube.com/watch?v=-nnosWtsWa8
Uamuzi huo umetolewa mahakamani hapo na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Abdi Kagomba, Jaji Evaristo Longopa na Jaji John Kahyoza lilipopelekwa kwa ajili ya hukumu.
 
Taratibu gani na vigezo gani huwa vinatumika kuteuwa hawa majaji?
Lissu aliwahi kusema majalj wetu hawana vigezo vya kua Jaji aliongea miaka hiyo wakati Kikwete ameteua majaji
 
Back
Top Bottom