Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,814
- 11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizindua Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai chini Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 31 Januari, 2023
Katibu Mkuu kiongozi Moses Kusiluka
Jukumu kubwa la tume ni kufanya tathmini ya kina ya mfumo wa haki jinai kwa lengo la kufanya maboresho makubwa ili kukidhi matakwa ya serikali na jamii ya Tanzania kwa ujumla.
Taasisi za haki jinai zitakazofanyiwa kazi na tume ni;
~ Jeshi la Polisi
~ Ofisi ya Taifa ya Mashtaka
~ TAKUKURU
~ Jeshi la Magereza
~ Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya
Tume ina jumla ya Wajumbe 11 ambao ni;
Sekretariat ya kuisaidia tume yenye Wajumbe watano ambao ni;
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango
Kumekuwa na manung'uniko mengi kutoka kwa wanachi ambayo yanaonesha kuwa mfumo wa haki jinai una changamoto nyingi kama vile kwenye ukamataji, wananchi kujua haki zao, ucheleweshwaji wa upepelezi nk.
Rais Samia Suluhu Hassan
Katika kipindi cha miongoo kadhaa mfumo wa kudai haki jinai nchini imeharibika kwa kupuuza mifumo ya maadili.
Mifumo ipitiwe upya kuangalia wapi pana makosa na kufanya marekebisho ili mambo yaende vizuri.
Tume imeundwa na watu ambao wametoka kwenye taasisi ambazo zinakwenda kuchunguzwa, mfano kutoka TAKUKURU, Rais wa Tanganyika Law Society, IGP wawili kutoka Jeshi la Polisi, Mwanasheria Mkuu, sababu wanajua wapi kuna matatizo na walipotetereka na itakuwa rahisi kuonesha penye matatizo na wapi pa kuboresha.
Kutokana na ukubwa wa kazi tume itakuwa na muda wa miezi minne kuwanzia tar 1/2/2023 hadi 30/5/2023 kupeleka ripoti (kamili au ya kwanza kutokana na muda utakavyokuwa) kwa Rais Samia.
Taasisi hizo zinazoenda kufanyiwa kazi na tume zina malalamiko mengi na zinatakiwa kwenda kuangaliwa, ili kubainisha matatizo hayo na yaweze kufanyiwa kazi.
Hakuna kitu kibaya kukichepusha Duniani kama kuchepusha kama haki ya mtu, kama wewe hutaki kunyang'anya haki yako basi unatakiwa kutengeneza mfumo ambao kwa kiasi kikubwa angalau inalinda haki za watu.
Baadhi ya mambo kadhaa yanayohitaji kuangaliwa kwenye taasisi hizo ni;
~ Utendaji wa taasisi hizo.
~ Masuala ya mafunzo ya ajira.
~ Mifumo ya ajira.
~ Upandishwaji wa vyeo katika taasisi hizo.
~ Matumizi ya TEHAMA na Ubunifu.
~ Fikra za kiutendaji na mahusiano kati ya taasisi hizo na raia.
Kwenye tatizo lolote zitaundwa timu, kwakuwa wataalamu wapo; kuchunguza kuna matatizo gani katika sekta mbalimbali.
Tume zimekuwa zikiundwa lakini mapendekezo yao yamekuwa hayafanyiwi kazi, hivyo tume hii inatakiwa kwenda na mapendekezo wa ya jinsi ya kuboresha kutokana na changamoto zitakazoibuliwa ambapo itarahisisha matatizo kushughulikiwa haraka.

- Mwenyekiti wa Tume Jaji Mkuu Mstaafu - Mohamed Othman Chande
- Makamu Mwenyekiti - Balozi Ombeni Sefue
- Laurean Vilomena Ndumbaro
- Jaji Eliezer Feleshi
- Dkt. Edward Kamanywa Hoseah
- Balozi Ernest Jumbe Mangu
- Saada Ibrahimu Makungu
- Omary Issa
- Yahya Khamis Hamad
- Baraka Leonard
- IGP Mstaafu Said Mwema
Sekretariat ya kuisaidia tume yenye Wajumbe watano ambao ni;
- Ramadhani Kailima
- Evata Mushi
- James Kilabuko
- Benjamin Mwakisongole
- Ally Mirza