Rais Samia asema itungwe Sheria itakayotoa muongozo kuwashughulia viongozi wanaofanya majukumu ambayo sio yao

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa rasmi ya Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai hapa Nchini, kutoka kwa Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman, Mwenyekiti wa Tume hiyo leo tarehe 15 Julai, 2023 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete - Ikulu Dares Salaam.

Tume hiyo iliundwa Jan 2023 na kuanza kazi rasmi Feb 1 2023 lengo likiwa ni kutoa tathmini ya kina ya mfumo wa haki jinai nchini ili ije kufanyiwa maboresho kwenye taasisi za Jeshi la Polisi, Mahakama za Mashtaka, TAKUKURU, Jeshi la Magereza, Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya na Mahakama ya Tanzania, tume hiyo iliundwa watu 11 ikiongozwa na Jaji Mstaafu Mohamed Chande, kwa ujumla tume imegusa taasisi 18.

chande.png

Mwenyekiti Tume ya Haki Jinai - Jaji Mstaafu Mohamed Chande Othmani

Tume imebaini uwepo wa udhaifu mkubwa kwenye mnyororo wa mzima wa Haki Jinai kwenye; kubaini na kuzuia uhalifu, kukamata na kupeleka watuhumiwa vituo vya polisi, uchunguzi wa upelelezi wa makosa ya jinai, undikishaji mashtaka, usikilizaji wa mashauri ya jinai hamakamani, waliotiwa hatiani kutumikia kifungo gerezani au kupewa adhabu mbadala, na maisha ya wafungwa anapomaliza vifungo vyao na kurejea uraiani.

Maeneo Makuu 13 yanayohusu Mnyororo wa Haki Jinai na Mapendekezo yake, kichobainika na mapendekezo ya tume

1/ Kubaini na Kuzuia Uhalifu

Tume imebaini Taifa halina mkakati mahususi wa kuzuia na kubaini uhalifu, jambo linalochangia vyombo vya utekelezaji sheria kujikita zaidi kwenye kwenye ukamataji kutokea, baada ya kutokea kuliko kubaini na kuzuia uhalifu.

Mapendekezo
~ Mamlaka na Wadau wengine wa Haki Jinai waandae na kusimamamia utekelezaji wa Mkakati mahusushi wa kubaini na kuzuia uhalifu Crime Detection and Prevention Policy ikiwemo uhalifu wa Majini na wa Mitandaoni.

~ Mfumo wa nyumba 10 uhuishwe kisheria na kutambulika rasmi katika mfumo wa serikali za mitaa ili kurahisisha wananchi kutambuana kwa lengo la kuwezesha mikakati ya kuzuia uhalifu kuwa endelevu.

~ Mfumo wa huduma za kijamii na kibiashara zifungamanishane na mfumo wa utambuzi w usajili za makazi, RITA na NIDA ili kila mwnanchi awe na namba moja ya utambuzi kwa maisha yake yote.

2/ Ukamataji wa Watuhumiwa
Vyombo vyenye mamlaka ya ukamataji mara kadhaa hutumia nguvu kupita kiasi na kusababisha mateso kwa watuhuimiwa.

Uwepo wa taasisi nyingi zenye mamlaka ya kukamata, ziznazoidhinishiwa kuwa na mahabusu na hivyo kusababisha ugumu kwa wananchi kutambua taasisi ipi inakamata watu, na mahabusu nyingine hazijulikani zilipo.

Mapendekezo
~ Taasisi zenye mamlaka ya ya kukamata watuhumiwa zitekeleze hayo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na maabusu za jeshi la polisi pekee ndio zitumike kuhifadhi watuhumiwa wa makosa yote ya jinai waliokamatwa.

3/ Watuhumiwa kutofikishwa mahakami ndani ya muda

Kuna malalamiko mengi ya muda mrefu kutoka kwa wananchi na wadau kuhusu watuhumiwa kushikiliwa kwa muda mrefu vituo vya polisi na kutofikishwa mahakamani nje ya muda na kinyume cha sheria.

Polisi kuendelea kukamata watuhumiwa kabla ya kukamilisha upepelezi.

Masharti magumu ya dhamana ya polisi.

Mashtaka kuchelewa kuandikwa ofisi ya mashtaka kutokana na uchache wa rasilimali watu na fedha.

Mapendekezo
~ Jeshi la polisi na vyombo vingine vya ukamataji kuwafikisha watuhumiwa mahakamani kwa wakati na kwa mujibu wa sheria na watuhumiwa wasikamatwe kabla ya upepelezi kukamilika isipokuwa kwa makosa makubwa.

4/ Upelelezi kuchukua muda mrefu
Wanachi walalamikia upelelezi kuchukua muda mrefu.

Mapendekezo
~ Sheria ya mwenendo ya Mashauri ya jinai irekebishwe, iweke kikomo wa muda wa upelelezi kwa mashauri yanayosubiri kusikilizwa Mahakama kuu.

5/ Matumizi Mabaya ya Madaraka
Wakuu wa Mikoa na Wakuuwa Wilaya wanalalamikiwa kutumia vibaya yao ya kutoa amri ya kuwakamata na kuwaweka wananchi mahabusu. Tume imependekeza mamlaka haya yafutwe.

Wakuu wa wilaya na mikoa kuongozana na wajumbe wa kamati za usalama hata katika ziara ambazo hazistahili uwepo wa kamati hizo.

wakuu wa mikoa na wilaya kujitambulisha kama Wenyeviti wa Kamati za Ulinzi na Usalama kinyume na sheria.

Mapendekezo
~ Wakuu wa mikoa na wilaya wakiwa anatekeleza mamlaka ya ukamataji ni muhimu kufata kifungu cha 7 na 15.

~ Kiongozi yoyote atakayekiuka maagizo awajibishwe.

~ Wakuu wa mikoa na wilaya wasijitambulishe kama wenyekiti wa kamati za ulinzi na usalama badala yake wajitambulishe kama Wenyeviti wa Kamati za usalama wakiwa wanaongoza vikao vya baraza la usalama.

~ Mamlaka ya kumkamata na kumuweka mtuhumiwa kizuizini waliyonayo wakurugenzi wa halmashauri na maafisa watendaji wa kata yaondolewe na yaache mikononi mwa jeshi la polisi, na mahakimu ambao ni walinzi wa amani waondolewe pia mamlaka hayo.

~ Baadhi ya viongozi wa juu wa kisisasa wamekuwa wakitoa matamko na amri kwa vyombo vya dola kukamata na kuweka ndani wananchi wakati mamlaka hayo hawana; Viongozi hao walekezwe kuzingatia sheria.

6/ Upelelzi na Uchunguzi
Kutotenganishwa kwa idara ya upelelezi wa jeshi la polisi na shughuli zingine za jeshi hilo limesababisha ucheleweshaji wa upelelezi, ukosefu wa ubobezi, ufanisi mdogo katika upelelezi, na upelelezi wa jeshi la polisi wakati mwingine kupangiwa shunguli nyingine ambazo hazihusiani na upelelezi.

Idara ya upelelezi ya jeshi la polisi inategemea bajeti ya jeshi la polisi na hivyo kuwa na bajeti ambayo haikidhi mahitaji.

TAKUKURU inakabiriwa na ukosefu wa wachubguzi wabobezi na wenye weledi wa kutosha kuhusu masuala ya rushwa, ufinyu wa bajeti, ukosefu wa vitendea kazi na kukosa ushirikiano kutoka taasisi nyingine.

Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za Kuvya inakabiliwa na changamato kadhaa ikiwemo mamlaka hii kutokuwa chombo cha muungano na kuwa katika maeneo machache nchini.

Changamoto ya uhalifu kuungamana mfano uhalifu wa kusafirisha dawa za kulevya kuhusiha utakatishati wa fedha na rushwa.

Mapendekezo
~ Serikali iunganishe nguvu ya upelelezi na uchunguzi iliyopo sasa ya vyombo vyote hivi kwa kuanzisha mamlaka upya huru ya upelelezi itakayojulikana na itakayijitegemea kama ofisi ya taifa ya upelelezi - National Bureau of Investigation itakayokuwa na jukumu la kupepeleza makosa yote makubwa ya jinai yakiwemo Rushwa na Dawa za Kulevya.

7/ Makubaliano ya kukiri kosa
Mapendekezo

~ Elimu zaidi itolewe kuhusu makubaliano ya kukiri kosa.

~ Malalamiko ya washtakiwa kulazimishwa kukiri kosa ambao wanasema hawakukiri kosa kwa hiari washaghulikie kwa kufata utaratibu mfano njiaya mahakama kutengua uamuzi huo.

~ Iundwe timu maalumu ya kuchunguza utata katika baadhi ya mali zilizotaifishwa katika utaratibu wa kukiri kosa na utendaji wa kikosi kazi ili kuishauri serikali.

8/ Uhuru wa kufuta mashauri mahakamani aliyonayo Mkurugenzi wa Mashtaka bila kutoa sababu na mahakama kutoweza kuingilia uamuzi huo
Uwepo wa malalamiko ya matumizi mabaya ya fursa hii - sheria ilirekebishwa (kifungu cha 31 (3)).

Mapendekezo
~ Mamlaka ya DPP kufuta kesi kwa uhuru wake ilendelee lakini kama kutaendelea kuwa na changamoto ya matumizi mabaya ya uhuru huu marekebisho ya sheria yanaweza kufanyika kama ilivyo kwa nchi nyingine ili uhuru huo utolewe kwa ridhaa ya mahakama.

~ Maafisa wa mahakama na waendesha mashtaka watakaoshindwa kuzingatia matakwa ya sheria wanatakiwa kuwajibika.

9/ Dhamana
Wadau mbalimbali wamekuwa na mtazamo tofauti kuhusu sheria zinazoruhusu dhamana kwa baadhi ya makosa, kwa sasa mamkosa ambayo yanakosa dhamana ni takribani 50.

Mapendekezo
~ Bila kuathiri mikataba ya kimataifa ya makosa ya udhibiti uchumi na mengine tafsiri ya makosa tangulizi ya utakatishaji fedha haramu irekebishwa ili kupunguza washtakiwa wengi kukosa dhamana kutokana na tafsiri hiyo pana.

~ Jedwali la 1 linaloainisha makosa ya uhujumu uchumi katika sheria ya kudhibiti makosa ya uhujumu uchumi na uhalifu wa kupangwa lipitiwe upya ili kuona iwapo kama kuna umuhimu wa makosa yote yaliyobainishwa kwenye sheria hii kuendelea kuwa ya uhujumu uchumi.

~ Makosa kwenye sheria ya kudhibiti uchumi irekebishwe kjuipa maamuzi ya dhamana mahakama ya Tanzania.

~ Sheria ya mwenendo ya mashauri ya jinai irekebishwe ili masharti ya makosa yasiyo na dhmana yaanze kusikilizwa ndani ya muda maalum na ikiwa mashauri hayo hayajasikilizwa ndani ya kipindi maalum basi mtuhumiwa anaweza kupewa dhamana.

~ Itungwe sheria moja ambayo itabeba kila kitu kuhusu dhamana.

10/ Utitiri wa vyombo wenye taswira ya kijeshi
Uwepo wa vyombo vya haki jinai vinavyotekeleza majukumu yake kwa taswira ya kijeshi jeshi la zima moto na uokoaji, jeshi la uhamiaji, jeshi usu la uhifadhi hali inayosababisha matumizi ya nguvu kupita kiasi kwa watuhumiwa katika ukamataji, upekuzi na mahojiano.

Uvaaji wa vyeo vinavyoshahabiana na jeshi la ulinzi na usalama la Tanzania.

Baadhi ya Taasisi hizo kujilinganisha hadhi na Jeshi la Ulinzi na Usalama.

Taasisi za haki jinai kukosa ushirikiano.

Malalamiko ya wananchi ya kunyanyaswa na kuteswa na taasisi zenye taswira ya kijeshi.

Kuwepo kwa uwezekanao wa kusambaa silaha zikiwemo za kivita suala ambalo linaweza kutishia amani ya nchi

Mapendekezo
~ Taasisi zinazotekelza majukumu ya Haki Jinai au zinazotoa huduma kwa wanachi zenye taswira ya kijeshi zirejee na kujikita zaidi kwenye majukumu yake ya awali ya utoaji huduma kwa wananchi.

~ Huduma za zima moto na uokoaji zirejeshwe na kutekelezwa kwenye ngazi ya halmashauri hasa ikizingatiwa shughuli za kuzima moto zina uingiliano mkubwa na shughuli nyingina za halmashauri katika mipango miji.

~ Mafunzo ya askiri misitu, uhifadhi na nyamapori yatolewe yatolewe na polisi kwa kuzingatia misingi ya haki jinai, binadamu na utawala sheria.

~ Waziri wa Maliasili na Utalii warejeshee watumishi wote raia katika vyombo vyao vya ajira ya awali na kuwaondolea mavazi ya vyeo ya kijeshi isipokuwa tu mavazi yavaliwe na watumishi walioko kwenye idara inayohisana na majukumu yakupambana na ujangili.

11/ upelelezi binafsi
Mapendekezo

~ Tume itunge sheria mahususi itakayoruhusu na kusimamia upelelezi binafsi ambapo itaainisha mamlaka itakayosimamia na kuratibu upelelezi binafsi, masharti ya usaili, aina ya upelelezi, mipaka ya upelelezi binafsi, maadili na nidhamu, wajibu wao wa jeshi la polisi na vyombo vingine vya uchunguzi.

12/ Adhabu ya kifungo cha maisha
Maoni na malalamiko ya kifungo cha maisha hakiwapi wafungwa nafasi ya kujirekebisha na kuendelea kulitumikia taifa na kwamba wakati umefika kifungu hiki kiwe na ukomo ili kuhakikisha wafungwa wanaotumikia kifungo cha maisha kuwa na matumaini.

Mapendekezo
~ Tume inapendekeza kwa sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 irekebishwe ili kuweka tafsiri ya kifungo cha maisha kwa kuonesha muda maalum wa kifungo.

13/ Adhabu ya kifo
Kuna maoni mbalimbali juu ya adhabu ya kifo, baadhi wanasema adhabu ya kifo isiondolewe kwakuwa ni stahiki kwa makosa yaliyotendwa na muhusika na ni funzo kwa jamii kutotenda makosa ambayo adhabu yao ni kifo. Wengine wanapendekeza adhabu ya kifo iondolewe kwakuwa ni ya kikatili isiyozingatia haki ya kuishi na haki za binadamu.

Adhabu hiyo imekuwa haitekelezwi kwa miaka mingi na kusababisha waliopewa adhabu hiyo kuishi maisha ya hofu huku wakisubiri utekelezaji wa adhabu hiyo, takwimu zinaonesha hadi Mei 2023 kuna watuhumiwa 691 wanasubiria kutekelezwa kwa adhabu hii, Tanzania haijatekeleza adhabu hii kwa miaka zaidi ya 28.

Mapendekezo
~ Sheria ya kanuni za adhabu, sura ya i6 ifanyiwe marekebisho ili adhabu ya kifo isiwe adhabu pekee ya kosa la mauaji.

~ Adhabu ya kifo isiporidhiwa na Rais kwa mamlaka aliyonayo kikatiba kwa kipindi cha miaka mitatu adhabu hiyo itengulike kuwa kifungo cha maisha.

Screenshot 2023-06-02 095942.png

Samia Suluhu Hassan - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

~ Mageuzi makubwa yaliyopendekezwa na Tume ya Haki Jinai yanaanza kwanza kwa kubadilisha mtazamo wetu sisi wenyewe kabla ya kwenda kwenye maboresho ya kiutawala na kiufundi.

~ Itungwe sheria kwa vingozi wanaoingia kwenye maeneo ambayo sio yao washughulikiwe.

~ Vyombo vya Haki Jinai visomane ili kupunguza watu kutotendewa haki.

~ Jeshi la Polisi litizamwe na kurebishwa, lisimame vizuri pamoja na stahiki zao kufanyiwa kazi ili lifanye kazi zao vizuri.

~ Nguvu za kupiga vita madwa ya kulevya na rushwa itiliwe mkazo kwa pande zote mbili Bara na Zanzibar.

~ Liandikwe concept paper ya marekebisho ya demokrasia, utawala bora na haki za binadamu Tanzania na kuwashirikisha wadau wengine wanaotaka kusaidia kwenye maeneo hayo.

~ TBC iite wataalam kuchambua Ripoti ya Tume ya Haki Jinai ili watu wasikie na waone mwelekeo wa serikali inapoelekea.
 
Attachments

  • MUHTASARI HAKI JINAI.pdf
    503.4 KB · Views: 12
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajia kupokea Taarifa Rasmi ya Tume ya Haki Jinai, leo Julai 15, 2023.

Matukio yote yanayojiri yatapatikana hapa. Endelea kufuatilia.

View attachment 2688626
 
Hawa wazee ni hazina ya taifa wasikilizwe.

Wakiongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu leo wametoa ripoti nzuri.

Hawamungunyi maneno na baadhi yao walipata kuyasema haya haya mbele ya Rais John Pombe Joseph Magufuli na leo 2023 kupitia ripoti kamili wanarudia mbele ya mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan.

Serikali iifanyie kazi haraka ripoti hii, kutengeneza framework ya utekelezaji wa mapendekezo haya na kupeleka muswaada wa dharura bungeni sheria kusapoti haya mapendekezo ili wale wote walio ktk kamati za ulinzi na usalama kuanzia ma- DC, wanasiasa na polisi wapewe vijitabu vikae ktk meza ofisini kwao na pia wakati wa vikao vyao vya ulinzi na usalama wavibebe.

Rais wa awamu ya tano Rais John Pombe Magufuli mwaka 2018 wazee hawa walimwambia 'live' mapungufu haya lakini hayakufanyiwa kazi awamu ya 5 ya serikali ya CCM.

Leo hii tena baadhi ya wazee haohao 2023 wamepata nafasi nyingine wamefika ikulu wanamuambia mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan mambo yaleyale.

Ni matumaini sasa ni wakati wa kutekeleza mapendekezo haya muhimu kwani serikali inaongozwa na chama kilekile, ilani ile ile na viongozi walewale wa kisiasa na kiserikali na wa mfumo wa utumishi katika taasisi za haki jamii waliokuwepo mwaka 2018 na leo bado wapo ktk utumishi mwaka 2023.

Kutoka maktaba:

Ni kweli kabisa mfumo wa Haki Jamii na taasisi zake nyingi haupo huru

Mfumo wa Haki Jamii unapaswa sasa kuanza kuacha kutumiwa na dola, ili ufanye kazi kwa haki ndiyo utakuwa mfumo Haki Jamii unaosimamia sheria na katiba bila kupokea amri toka mhimili wa executive (wanasiasa / serikali)

Kwa mfano Jaji Mkuu mstaafu jaji Barnabas A . Samatta ameandika kitabu kinachogusa sehemu ya mfumo wa haki jamii kuhusu uhuru wa mahakama na hakika inatakiwa raia wote ikiwemo jaji mkuu aliyepo ofisini, majaji, mahakimu kukisoma na kuwa rejea kuhusu umuhimu wa mhimili wa Mahakama katika nchi hususan yetu ya Tanzania

1689411904522.png

Barnabas A. Samatta, Jaji Barnabas A. Samatta, alikuwa Jaji Mkuu wa Tanzania kutoka 2000 hadi 2007. Huko nyuma, 1984-1987, alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zimbabwe. Yeye ni mjumbe mwanzilishi wa Judicial Integrity Group (Kikundi cha Uadilifu wa Mahakama), chombo huru cha cha kimataifa kinacho jishughulisha na ukuzaji wa uadilifu wa mahakama duniani na ambacho kilitunga Kanuni za Bangalore za Mwenendo wa Mahakama. Kwa wakati huu, yeye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Bodi ya Kampuni ya Earth, Energy and Environment Mediation Limited yenye makao makuu yake London, Uingereza, ambayo inashughulikia njia bora za kuzuia au kutatua migogoro barani Afrika inayohusiana na ardhi, mafuta, madini, maji au mazingira. Vilevile, Jaji Samatta ni Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe. Katika baadhi ya hukumu, makala na hotuba zake amesisitiza sana juu ya umuhimu wa uhuru wa mahakama, usawa mbele ya sheria na upatikanaji wa haki kwa unafuu na wepesi kwa kila mtu katika jamii. Katika kitabu hiki, anazungumzia kwa ufasaha, lakini kwa lugha nyepesi kuelewa, na kwa namna isiyomchosha msomaji, masuala mengi muhimu sana katika uwanja wa utoaji wa haki. Miongoni mwake ni uhuru wa mahakama; rushwa; ugumu wa kazi na maisha ya jaji; mikwaruzano baina ya mihimili ya dola na utumiaji wa kiuonevu wa mamlaka ya dola. Hiki ni kitabu kwa mwanasheria na kwa mlei. Ni kitabu kwa mtawala na mtawaliwa. Kwa kweli, ni kitabu kwa kila mtu.

5 July 2018
Ikulu mbele ya John Pombe Magufuli

Umuhimu wa utawala wa sheria - Jaji Barnabas A. Samatta

Sheria zinazopelekwa mbele ya bunge (bills) lazima kwanza zichunguzwe kwanza kama zinakiuka katiba, sheria na haki anasisitiza jaji mstaafu B.A Samatta na kusisitiza kila mmoja ktk ngazi za maamuzi wasisitize haki ikiwemo maDC, maRC n.k maana nikusikiliza radio au kutazama TV amri wanazotoa watendaji zingine zina kukakasi mkubwa anamalizia jaji mstaafu B. A Samatta almaarufu "B.A.S" anavyojulikana na washikaji wenzie wa karibu.
 
Hawa wazee wasikilizwe wastaafu wakiongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu leo wametoa ripoti nzuri. Hawamungunyi maneno walisema mbele ya Rais John Pombe Magufuli na leo 2023 kupitia ripoti kamili wanarudia mbele ya mheshimiwa rais Samia Hassan.

Serikali iifanyie kazi haraka ripoti hii, kutengeneza framework ya utekelezaji wa mapendekezo haya na kupeleka muswaada bungeni sheria kusapoti haya mapendekezo ili wale wote walio ktk kamati za ulinzi na usalama kuanzia DC, wanasiasa na polisi wapewe vijitabu vikaa ktk meza ofisini na wakati wa vikao vyao vya ulinzi na usalama.

Rais wa awamu ya tano Rais John Pombe Magufuli mwaka 2018 wazee hawa walimwambia 'live' mapungufu haya lakini hayakufanyiwa kazi.

Leo hii tena baadhi ya wazee haohao 2023 ikulu wanamuambia mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan mambo yaleyale sasa. Ni matumaini sasa ni wakati wa kutekeleza mapendekezo haya muhimu kwani serikali inaongozwa na chama kilekile, ilani ile ile na viongozi walewale wa kisiasa na kiserikali na wa mfumo wa utumishi katika taasisi za haki jamii waliokuwepo mwaka 2018 na leo bado wapo ktk utumishi mwaka 2023.

Kutoka maktaba:

Ni kweli kabisa mfumo wa Haki Jamii na taasisi zake nyingi haupo huru

Mfumo wa Haki Jamii unapaswa sasa kuanza kuacha kutumiwa na dola, ili ufanye kazi kwa haki ndiyo utakuwa mfumo Haki Jamii unaosimamia sheria na katiba bila kupokea amri toka mhimili wa executive (wanasiasa / serikali)

Kwa mfano Jaji Mkuu mstaafu jaji Barnabas A . Samatta ameandika kitabu kinachogusa sehemu ya mfumo wa haki jamii kuhusu uhuru wa mahakama na hakika inatakiwa raia wote ikiwemo jaji mkuu aliyepo ofisini, majaji, mahakimu kukisoma na kuwa rejea kuhusu umuhimu wa mhimili wa Mahakama katika nchi hususan yetu ya Tanzania

View attachment 2688692

5 July 2018
Ikulu mbele ya John Pombe Magufuli

Umuhimu wa utawala wa sheria - Jaji Barnabas A. Samatta

Sheria zinazopelekwa mbele ya bunge (bills) lazima kwanza zichunguzwe kwanza kama zinakiuka katiba, sheria na haki anasisitiza jaji mstaafu B.A Samatta na kusisitiza kila mmoja ktk ngazi za maamuzi wasisitize haki ikiwemo maDC, maRC n.k maana nikusikiliza radio au kutazama TV amri wanazotoa watendaji zingine zina kukakasi mkubwa anamalizia jaji mstaafu B. A Samatta almaarufu "B.A.S" anavyojulikana na washikaji wenzie wa karibu.

Hii kumbukumbu nzuri sana.
 
Hii kumbukumbu nzuri sana.

Tatizo, Je? hawa viongozi wa serikali na chama tawala watakuwa na utashi wa kisiasa kusimamia zoezi la kufumuliwa kwa mfumo Haki Jamii ulio tepevu unaowabeba bila haki kwa manufaa ya wao kubaki madarakani na wawezeshe mabadiliko ili mfumo Haki Jinai thabiti wa kufuata haki utamalaki nchini Tanzania ?
 
Tatizo hawa viongozi wa serikali na chama tawala watakuwa na utashi wa kisiasa kusimamia zoezi la kufumuliwa kwa mfumo Haki Jamii ulio tepevu unaowabeba bila haki kwa manufaa ya wao kubaki madarakani na wawezeshe mabadiliko ili mfumo Haki Jinai thabiti wa kufuata haki utamalaki nchini Tanzania ?
Wao ndio wanufaika wakubwa wa matendo hayo ya uminywaji wa haki.
 
Hawa wazee hawa hazina ya taifa wasikilizwe.

Wakiongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu leo wametoa ripoti nzuri.

Hawamungunyi maneno walipata kuyasema haya haya mbele ya Rais John Pombe Joseph Magufuli na leo 2023 kupitia ripoti kamili wanarudia mbele ya mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan.

Serikali iifanyie kazi haraka ripoti hii, kutengeneza framework ya utekelezaji wa mapendekezo haya na kupeleka muswaada wa dharura bungeni sheria kusapoti haya mapendekezo ili wale wote walio ktk kamati za ulinzi na usalama kuanzia ma- DC, wanasiasa na polisi wapewe vijitabu vikae ktk meza ofisini kwao na pia wakati wa vikao vyao vya ulinzi na usalama wavibebe.

Rais wa awamu ya tano Rais John Pombe Magufuli mwaka 2018 wazee hawa walimwambia 'live' mapungufu haya lakini hayakufanyiwa kazi.

Leo hii tena baadhi ya wazee haohao 2023 ikulu wanamuambia mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan mambo yaleyale sasa. Ni matumaini sasa ni wakati wa kutekeleza mapendekezo haya muhimu kwani serikali inaongozwa na chama kilekile, ilani ile ile na viongozi walewale wa kisiasa na kiserikali na wa mfumo wa utumishi katika taasisi za haki jamii waliokuwepo mwaka 2018 na leo bado wapo ktk utumishi mwaka 2023.

Kutoka maktaba:

Ni kweli kabisa mfumo wa Haki Jamii na taasisi zake nyingi haupo huru

Mfumo wa Haki Jamii unapaswa sasa kuanza kuacha kutumiwa na dola, ili ufanye kazi kwa haki ndiyo utakuwa mfumo Haki Jamii unaosimamia sheria na katiba bila kupokea amri toka mhimili wa executive (wanasiasa / serikali)

Kwa mfano Jaji Mkuu mstaafu jaji Barnabas A . Samatta ameandika kitabu kinachogusa sehemu ya mfumo wa haki jamii kuhusu uhuru wa mahakama na hakika inatakiwa raia wote ikiwemo jaji mkuu aliyepo ofisini, majaji, mahakimu kukisoma na kuwa rejea kuhusu umuhimu wa mhimili wa Mahakama katika nchi hususan yetu ya Tanzania

View attachment 2688692

5 July 2018
Ikulu mbele ya John Pombe Magufuli

Umuhimu wa utawala wa sheria - Jaji Barnabas A. Samatta

Sheria zinazopelekwa mbele ya bunge (bills) lazima kwanza zichunguzwe kwanza kama zinakiuka katiba, sheria na haki anasisitiza jaji mstaafu B.A Samatta na kusisitiza kila mmoja ktk ngazi za maamuzi wasisitize haki ikiwemo maDC, maRC n.k maana nikusikiliza radio au kutazama TV amri wanazotoa watendaji zingine zina kukakasi mkubwa anamalizia jaji mstaafu B. A Samatta almaarufu "B.A.S" anavyojulikana na washikaji wenzie wa karibu.

Pdf!?
 
Tume imebaini uwepo wa udhaifu mkubwa kwenye mnyororo wa mzima wa Haki Jinai kwenye;

Tume hiyo inaongozwa na Mhe. Mohammed Othman Chande ambaye ni mwenyekiti,
  • Balozi Omben Sefue Makamu Mwenyekiti, na huku wajumbe wakiwa ni :
  • Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali,
  • Profesa Edward Hosea,
  • Said Ally Mwema IGP mstaafu,
  • Balozi Ernest Magu IGP mstaafu,
  • Dkt. Laurean Ndumbaro
  • na Bw. Omary Issa
Source : Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AGCTZ) | TUME YA RAIS YA KUBORESHA HAKI JINAI YAKUTANA NA WADAU MKOANI MWANZA
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa rasmi ya Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai hapa Nchini, kutoka kwa Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman, Mwenyekiti wa Tume hiyo leo tarehe 15 Julai, 2023 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete - Ikulu Dares Salaam.

Tume hiyo iliundwa Jan 2023 na kuanza kazi rasmi Feb 1 2023 lengo likiwa ni kutoa tathmini ya kina ya mfumo wa haki jinai nchini ili ije kufanyiwa maboresho kwenye taasisi za Jeshi la Polisi, Mahakama za Mashtaka, TAKUKURU, Jeshi la Magereza, Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya na Mahakama ya Tanzania, tume hiyo iliundwa watu 11 ikiongozwa na Jaji Mstaafu Mohamed Chande, kwa ujumla tume imegusa taasisi 18.

Mwenyekiti Tume ya Haki Jinai - Jaji Mstaafu Mohamed Chande

Tume imebaini uwepo wa udhaifu mkubwa kwenye mnyororo wa mzima wa Haki Jinai kwenye; kubaini na kuzuia uhalifu, kukamata na kupeleka watuhumiwa vituo vya polisi, uchunguzi wa upelelezi wa makosa ya jinai, undikishaji mashtaka, usikilizaji wa mashauri ya jinai hamakamani, waliotiwa hatiani kutumikia kifungo gerezani au kupewa adhabu mbadala, na maisha ya wafungwa anapomaliza vifungo vyao na kurejea uraiani.

Maeneo Makuu 13 yanayohusu Mnyororo wa Haki Jinai na Mapendekezo yake, kichobainika na mapendekezo ya tume

1/Kubaini na Kuzuia Uhalifu

Tume imebaini Taifa halina mkakati mahususi wa kuzuia na kubaini uhalifu, jambo linalochangia vyombo vya utekelezaji sheria kujikita zaidi kwenye kwenye ukamataji kutokea, baada ya kutokea kuliko kubaini na kuzuia uhalifu.

Mapendekezo
Mamlaka na Wadau wengine wa Haki Jinai waandae na kusimamamia utekelezaji wa Mkakati mahusushi wa kubaini na kuzuia uhalifu Crime Detection and Prevention Policy ikiwemo uhalifu wa Majini na wa Mitandaoni

Mfumo wa nyumba 10 uhuishwe kisheria na kutambulika rasmi katika mfumo wa serikali za mitaa ili kurahisisha wananchi kutambuana kwa lengo la kuwezesha mikakati ya kuzuia uhalifu kuwa endelevu

Mfumo wa huduma za kijamii na kibiashara zifungamanishane na mfumo wa utambuzi w usajili za makazi, RITA na NIDA ili kila mwnanchi awe na namba moja ya utambuzi kwa maisha yake yote

2/ Ukamataji wa Watuhumiwa
Vyombo vyenye mamlaka ya ukamataji mara kadhaa hutumia nguvu kupita kiasi na kusababisha mateso kwa watuhuimiwa

Uwepo wa taasisi nyingi zenye mamlaka ya kukamata, ziznazoidhinishiwa kuwa na mahabusu na hivyo kusababisha ugumu kwa wananchi kutambua taasisi ipi inakamata watu, na mahabusu nyingine hazijulikani zilipo

Mapendekezo
~ Taasisi zenye mamlaka ya ya kukamata watuhumiwa zitekeleze hayo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na maabusu za jeshi la polisi pekee ndio zitumike kuhifadhi watuhumiwa wa makosa yote ya jinai waliokamatwa

3/ Watuhumiwa kutofikishwa mahakami ndani ya muda

Kuna malalamiko mengi ya muda mrefu kutoka kwa wananchi na wadau kuhusu watuhumiwa kushikiliwa kwa muda mrefu vituo vya polisi na kutofikishwa mahakamani nje ya muda na kinyume cha sheria

Polisi kuendelea kukamata watuhumiwa kabla ya kukamilisha upepelezi

Masharti magumu ya dhamana ya polisi.

Mashtaka kuchelewa kuandikwa ofisi ya mashtaka kutokana na uchache wa rasilimali watu na fedha

Mapendekezo
~ Jeshi la polisi na vyombo vingine vya ukamataji kuwafikisha watuhumiwa mahakamani kwa wakati na kwa mujibu wa sheria na watuhumiwa wasikamatwe kabla ya upepelezi kukamilika isipokuwa kwa makosa makubwa.

4/ Upelelezi kuchukua muda mrefu
Wanachi walalamikia upelelezi kuchukua muda mrefu

Mapendekezo
Sheria ya mwenendo ya Mashauri ya jinai irekebishwe, iweke kikomo wa muda wa upelelezi kwa mashauri yanayosubiri kusikilizwa Mahakama kuu

5/ Matumizi Mabaya ya Madaraka
Wakuu wa Mikoa na Wakuuwa Wilaya wanalalamikiwa kutumia vibaya yao ya kutoa amri ya kuwakamata na kuwaweka wananchi mahabusu. Tume imependekeza mamlaka haya yafutwe

Wakuu wa wilaya na mikoa kuongozana na wajumbe wa kamati za usalama hata katika ziara ambazo hazistahili uwepo wa kamati hizo

wakuu wa mikoa na wilaya kujitambulisha kama Wenyeviti wa Kamati za Ulinzi na Usalama kinyume na sheria

Mapendekezo
Wakuu wa mikoa na wilaya wakiwa anatekeleza mamlaka ya ukamataji ni muhimu kufata kifungu cha 7 na 15

Kiongozi yoyote atakayekiuka maagizo awajibishwe

Wakuu wa mikoa na wilaya wasijitambulishe kama wenyekiti wa kamati za ulinzi na usalama badala yake wajitambulishe kama Wenyeviti wa Kamati za usalama wakiwa wanaongoza vikao vya baraza la usalama

Mamlaka ya kumkamata na kumuweka mtuhumiwa kizuizini waliyonayo wakurugenzi wa halmashauri na maafisa watendaji wa kata yaondolewe na yaache mikononi mwa jeshi la polisi, na mahakimu ambao ni walinzi wa amani waondolewe pia mamlaka hayo

Baadhi ya viongozi wa juu wa kisisasa wamekuwa wakitoa matamko na amri kwa vyombo vya dola kukamata na kuweka ndani wananchi wakati mamlaka hayo hawana; Viongozi hao walekezwe kuzingatia sheria.

Tume na ripoti za kupotezeana muda maana hakuna utekelezaji wowote. Iwapo ccm itaendelea kukaa madarakani kwa shuruti, tusitegemee utekelezaji wowote wa hayo mapendekezo hayo, maana zaidi ya 80% ya hayo malalamiko na mapendekezo ni athari za uwepo wao madarakani.
 
N.B
Kesi ya mheshimiwa Freeman Mbowe na wenzie watatu kwa niaba wa watuhumiwa wa kesi nyingine nyingi waliopo rumande, iliweka wazi jinsi mfumo wa Haki Jinai unavyoweza kutumika vibaya.

Majina ya watuhumiwa kutokuwepo ktk rejista ya kitabu cha waliopo rumande. Ndugu kunyimwa taarifa ndugu zao ambao ni watuhumiwa wamewekwa kituo gani cha polisi rumande, mawakili kushindwa kuwafikia wateja wao walio watuhumiwa ambao wapo rumande n.k

Toka maktaba :

KESI YA UGAIDI NAMBA 16 YA MWAKA 2021 INAYOMTUHUMU MBOWE NA WENZIE WATATU, IMEFIKIA PATAMU.

Kesi ya Freeman Mbowe inashabiana na kesi ya maarufu ya Nelson Mandela iliyojulikana kama kesi ya Rivonia, ambapo ilipelekea dunia nzima kufahamu maovu ya utawala wa kibaguzi wa Afrika ya Kusini na ulimwengu kuanza kuingalia Afrika ya Kusini kama nchi yenye matatizo.

Tanzania nayo kesi hii namba 16 ya mwaka 2021 ya ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzie watatu tayari imekuwa gumzo jinsi vyombo vya dola vinavyofanya kazi inayozua maswali mengi sana, tuendelee kusikiliza kesi hii mpaka tamati yake na je itaifanya Tanzania mpya kuzaliwa kama Afrika ya Kusini mpya The Rivonia Trial: The Landmark Event that Changed South Africa Forever - Google Arts & Culture kupatikana kwa rais Frederik Willem de Klerk kuongoza mabadiliko na Afrika ya Kusini mwaka 1994 kumpata kiongozi wa utawala mpya usio na ubaguzi chini ya rais Nelson Mandela huku aliyekuwa rais wa mwisho wa utawala wa wachache weupe Frederik Willem de Klerk akiwa makamu wa rais ?
Under the interim constitution (valid from 1994 to 1996), there was a Government of National Unity, in which a member of parliament from the largest opposition party was entitled to a position as deputy president. Along with Mbeki, the previous state president, F. W. de Klerk also served as deputy president in his capacity as the leader of the National Party, then the second-largest party in the new Parliament. De Klerk later resigned and went into opposition with his party. A voluntary coalition government continues to exist under the new constitution (adopted in 1996), although there have been no appointments of opposition politicians to the post of deputy president.

Rivonia Trial 1963 - 1964, the trial that changed South Africa

Shot of the Palace of Justice during a lunch recess, seen from the supporters’ point of view. Rivonia Trial. © PTA News LibrarySource: Pretoria

In the Rivonia Trial, the ‘accused’ addressed this problem by using the courts as a site of struggle. They argued that the law was drawn up without the consent of the majority; it was enforced to ensure the perpetuation of an unjust system, and therefore the struggle would be waged to establish a new system, including a legal system that would embody the values of a non-racial constitution that protected human rights.

For the accused, the courtroom became a new site of struggle. The defendants’ daily appearances in court drew large crowds that filled up the courtroom and streets outside the court. Many supporters were in violation of numerous influx control regulations, and the courts for them too, became new sites of struggle.

In presenting the prosecution’s case, Yutar claimed that the accused were all members of what he considered ‘a cabinet of the government soon after the overthrow of the state’. In this cabinet, Mandela was Deputy Minister and Minister of Defence, while Govan Mbeki was Minister of European Affairs. The rest of the accused each had a cabinet portfolio.

Often referred to as "the trial that changed South Africa,” in October 1963, ten leading opponents of apartheid went on trial for their lives on charges of sabotage.

READ MORE Rivonia Trial 1963 - 1964 | South African History Online

Nelson Mandela: The Rivonia Trial​

The story of Nelson Mandela and the other Rivonia Trialists, from the series "Have You Heard From Johannesburg."
Source : Clarity films
 
Back
Top Bottom