Rais Samia kwanini nawe nakuomba usiyaamini Matokeo ya Jana ya Kidato cha Sita ya nchi nzima?

Hii elimu yetu kweli inahusiana na thinking capacity??

Kukalili kwingi na sio kuelewa, ukiotea gaka pepa unatusua vizuri tu!!.

Na sio mwaka huu tu, ni miaka mingi nyuma elimu yetu ilo hivyo.
Na sio lectureres tu hata walimu wa sekondari hulalamika kupokea wanafuzni wasiojua kusoma vizuri kwa ile mitihani yao ya sasa hivi ya shading!!

Walau wanaoenda form 5 shule za serikali ndio hua na viakili ila kwa sasa private schools zipo kibao, mtu ana ufaulu mdogo tu anazama advance, huko anakalilishwa mwisho anatusua chuo.

Matokeo mimi nayaamini kwa 90%. Ila ni msingi mbovu toka kule chini kabisa primary.
 
Umenena kweli,Kuna wanafunzi watatu nawajua,hata division four hawastahili kupata,eti nao Wana div.one na two.Imenishangaza Sana.Wale hata uwape mtihani wa form one hawatoboi.
 
Uko sahihi sana, kuna shida saana kwenye hii elimu yetu na ukiona matokeo kama hivi basi unabaki kuhuzunika tu.

Wazazi tusishangilie sana matokeo ya hawa vijana wetu baadala yake tutafuta namna binafsi kuwaandaa watoto na mapambano ya dunia inayokwenda kasi sana, Matokeo haya ni kama bomu linalosubiri kulipuka mbeleni huko. Matokeo haya ndio yanafanya watanzania kudharaulika hasa pale kiajana anapoonekana genius kwenye matokeo na kupata GPA kali chuo kikuu halafu kiuhalisia ni kilaza.
 
Watanzania kwa kutojiamini wapo wengi sana...Kila mara hawaoni kama wanaweza kufanya makubwa bali wanadhani majirani na wale wa majuu ndio wenye haki miliki za kufanikiwa lakini sio wao...Ni Ujinga uliopitiliza.

Wanaosema matokeo ya kidato cha sita ya mwaka yana mushkeri watoe data za kuunga mkono madai yao, siyo kuishia kubwabwaja tu kama wapo kwenye kombolela!

Tuthamini na kuenzi vya kwetu kuliko kushadidia vya wenzetu...Tujikomboe kwanza kifikra na mengine yatafuata.
Ita mwanafunzi yeyote, muulize maswali madogo madogo Kama Yale ya Tasker challenge ya chemsha bongo uone., Basic understanding yake..utakubaliana na mm hicho anachosema Gentemycine
 
Hii wizara angepewa Dr Dau,, inatakiwa iongozwe na watu wenye hofu ya mungu na wasio na matamanio ya mambo ya kiduniya
 
1. Ni Matokeo ya Kisiasa ili kukupa Moyo uone Elimu ya Tanzania ni nzuri wakati Mimi GENTAMYCINE kama Mwanataaluma naiona ilikuwa ICU na sasa inaenda kuhifadhiwa Mortuary kwa Maziko.

2. Ni Matokeo ya Kukudanganya ili Watendaji wa Sekta ya Elimu wawe na uhakika na Ajira zao na Mkate wao wa kila Siku.

3. Ni Matokeo ya Kuwahadaa Wazazi wao kuwa Watoto wao wana Akili sana wakati Kiuhalisia na tunavyokaa nao katika Mitaa yetu tunajua kuwa hawana kabisa hizo Akili.

4. Kitaaluma na Kisaikolojia haiwezekani kukawa na above 85% to 85% ya Ufaulu wa Wanafunzi ( tena hawa Goi Goi ) tulionao wa sasa.

5. Rais Samia kungekuwa na Ufaulu huo wa Kimbunga ambao kila mwaka tunatangaziwa basi Wahadhiri wa Vyuo Vikuu wasingekuwa Wanalalamika kuwa Wanafunzi wanaokutana nao huko wana very low thinking capacity hivyo wanawapa Usumbufu wa Kitaaluma.

6. Ni Matokeo ya Kiini Macho tupu tu.

7. Ni Matokeo yanayoonyesha tabia ya Usanii ya Watanzania na jinsi gani Kizazi cha baadae cha Watanzania kitatawaliwa na Wasanii na Goi Goi watupu.

GENTAMYCINE siyaamini hayo Matokeo tena kwa 100% na nijuavyo ni kuwa kama Mdau wa Elimu kwa sasa Elimu ya Tanzania si tu kwamba ipo ICU bali imeshafariki na inasubiria Kuzikwa tu.

Hata Jeshini mkienda Kozi mbalimbali hamuwezi nyote mkamaliza kwa idadi ile ile mliyoanza lazima kuna ambao Wataumia, Watateguka Bandana, Kolomero, Watazimia na hasa Kufa kabisa.

Naionea Huruma Elimu ya Nchini.
Upo sahihi. Walianza kwa kupanua magoli, A ikashushwa ikaanzia marks 75. Sasa kila mwaka ufaulu unapanda, umeshafika 99.8%. Walivyo weupe kichwani kidogo watavuka 100%!
 
shida yetu ni vijana kufaulu tu, hatujui na wala kukumbuka kama kuna "standard and quality" tuliyoweka kwa mhitimu wa kila daraja tunaishia kuwapima tu na mtihani wa siku moja..

Hivi tunajua kweli dunia inataka nini na wahitimu wetu wanamaliza na nini kichwani.

Wengine wanapamban kufuta mitihani, sisi tunapambana vijana wetu kufaulu mitihani.
 
simple test, tunawatahini vijana wetu kwa mitihani iliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza na tuliwafundisha kwa kutumia mitaala ya kiingereza.

Ni wahitimu wangapi wa kidato cha sita wanaiongea hiyo lugha walioyosomea?.
 
Kinachofanyika,
Ni walimu wanaohusika kuandaa Continuous Assesment (CA) huongezea alama wanafunzi.
Ipo hivi mtihan wa Taifa NECTA kwa O &A level huw na alama 75,
Alama 25 hutokana na CA.
Hivyo mbali na Janja nyingine ya watendaji idara ya elimu kupika matokeo,
Chanzo kingine ni hicho.
Wakuu wa shule hucheza sana hiyo michezo ili kutft sifa na kulinda vitu vyao kw style hiyo.
 
1. Ni Matokeo ya Kisiasa ili kukupa Moyo uone Elimu ya Tanzania ni nzuri wakati Mimi GENTAMYCINE kama Mwanataaluma naiona ilikuwa ICU na sasa inaenda kuhifadhiwa Mortuary kwa Maziko.

2. Ni Matokeo ya Kukudanganya ili Watendaji wa Sekta ya Elimu wawe na uhakika na Ajira zao na Mkate wao wa kila Siku.

3. Ni Matokeo ya Kuwahadaa Wazazi wao kuwa Watoto wao wana Akili sana wakati Kiuhalisia na tunavyokaa nao katika Mitaa yetu tunajua kuwa hawana kabisa hizo Akili.

4. Kitaaluma na Kisaikolojia haiwezekani kukawa na above 85% to 85% ya Ufaulu wa Wanafunzi ( tena hawa Goi Goi ) tulionao wa sasa.

5. Rais Samia kungekuwa na Ufaulu huo wa Kimbunga ambao kila mwaka tunatangaziwa basi Wahadhiri wa Vyuo Vikuu wasingekuwa Wanalalamika kuwa Wanafunzi wanaokutana nao huko wana very low thinking capacity hivyo wanawapa Usumbufu wa Kitaaluma.

6. Ni Matokeo ya Kiini Macho tupu tu.

7. Ni Matokeo yanayoonyesha tabia ya Usanii ya Watanzania na jinsi gani Kizazi cha baadae cha Watanzania kitatawaliwa na Wasanii na Goi Goi watupu.

GENTAMYCINE siyaamini hayo Matokeo tena kwa 100% na nijuavyo ni kuwa kama Mdau wa Elimu kwa sasa Elimu ya Tanzania si tu kwamba ipo ICU bali imeshafariki na inasubiria Kuzikwa tu.

Hata Jeshini mkienda Kozi mbalimbali hamuwezi nyote mkamaliza kwa idadi ile ile mliyoanza lazima kuna ambao Wataumia, Watateguka Bandana, Kolomero, Watazimia na hasa Kufa kabisa.

Naionea Huruma Elimu ya Nchini.
GENTAMYCINE et al. Suluhisho ni wanasiasa kuacha kutoa comments kwenye mambo ya ufaulu kwa wanafunzi. Vyuoni kwenyewe kipindi nasoma eti mkifeli mnataka muandamane. Enzi za mkoloni hat Mwl Nyerere hapakuwa na siasa kwenye Elimu. Tulishuhudia awamu ya 5 eti wasahishaji wanaambiwa wakaze mkono kwa shule za private, walegeze kwa shule za serikali. Yaani kama taifa tunaanda generation yenye elimu ya mchongo halafu tutegemee watu waadilifu? It’ll take generations nchi yetu kupata maendeleo.
 
Upo sahihi. Walianza kwa kupanua magoli, A ikashushwa ikaanzia marks 75. Sasa kila mwaka ufaulu unapanda, umeshafika 99.8%. Walivyo weupe kichwani kidogo watavuka 100%!
O level A ndio 75% A level inaanzia 80% kitu kama hiko.
 
Kama lile toto la swahiba wangu limepata division one, basi maajabu mapya ya dunia yamepatikana....
 
Nauliza tu sio kwa ubaya nia njema. Hiv ile shule ya chato iliyokuwa inaongoza mwaka huu imekuwa ya ngapi?
 
Back
Top Bottom