TUKANA UONE
JF-Expert Member
- Jan 3, 2018
- 1,816
- 5,151
Salamu nishamuachia ndugu yangu GENTAMYCINE yeye na ndugu zake wa Butiama & Nyamuswa!
Nimejaribu kutembelea mikoa kadhaa hapa nchini ikiwemo mkoa wa kibiashara wa Dar es Salaam na kila sehemu utakayopita utaona mabango barabarani yakimtambulisha Rais Samia Suluhu Hassan kama ndiye Rais!
Nimekuwa nikishangaa sana hayo mabango si Dar es Salaam pekee bali hadi huko mikoani!
Je, kuna watu hayo mabango yamewalenga? Je, kuna mtu hadi sasa kwenye hii nchi baada ya kifo cha Rais John Pombe Magufuli asiyefahamu Rais ni Samia Suluhu Hassan?
Kwanini hayo mabango serikali kupitia wizara ya utalii isiyatumie kutangaza utalii wa ndani na vivutio tulivyonavyo?
Nilidhani Serikali ingetumia fursa hii kutangaza vivutio ili watalii wa ndani wahamasike kutembelea vivutio vyao hasa kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka!
Naelewa watu watasema pengine hayo mabango yanalipiwa eidha na serikali yenyewe au chama cha mapinduzi ili kumnadi Rais wao?
Je, kama ni kulipia, hatuoni hata Rwanda au Kenya wanaweza wakaja wakaweka mzigo (pesa) ili kuvitangaza vivutio vya nchini kwao?