Rais Samia awatakia kheri watahiniwa wa Kidato cha Nne 2023

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Rais Samia Suluhu Hassan kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii amewatakia kheri wahitimu wa kidato cha nne wote nchini wanaoanza mitihani yao leo Jumatatu Novemba 13 na kutarajiwa kuimaliza Novemba 30, 2023.

“Nawatakia kila la kheri wanafunzi wote wa Kidato cha Nne mlioanza mtihani wenu (CSEE) leo, katika shule za sekondari 5,371 nchi nzima. Mnaelekea mwisho wa hatua nyingine muhimu katika safari yenu ya elimu na maisha, baada ya kujiandaa kwa miaka minne.

“Mwenyezi Mungu awape utulivu, mkaifanye vyema mitihani yenu na kupata matokeo mazuri. Serikali tayari imeandaa mazingira bora ya kuwapokea katika hatua inayofuata, ikiwemo kufuta ada kwa elimu ya Kidato cha tano na sita,”amesema Rais Samia.

Screenshot 2023-11-13 at 13.06.32.png
 
Na sisi washabaki wa kolwenyo anatutwiti lini asa jama kwa kuchaguliwa kwetu
 
Back
Top Bottom