Nimemsikia Rais Mama Samia anasema kila mbuzi hula kutokana na urefu wa kamba yake akiwambia kikao na Mawaziri wake, sijuwi amemaanisha nini kwamba mawaziri sasa wataanza kugawana rasilimali na mapato?
Embu tujielekeze hapa kidogo wale watu wenye taaluma fasihi, Mama kila siku anatoa kamsemo mpya mpya.
Natanguliza shukurani.
"Mara moja nilisema kwenye baraza la mawaziri nikasema mimi najua kila mbuzi hula urefu wa kamba yake, jinsi kamba yako inavyokuruhusu ndivyo unavyokula lakini nikawaambia mbona mnakula sana? Mnavimbiwa! Si kweli kwamba hampati kwenye maeneo yenu, mnapata, lakini jipimie, jipimieni.
"Kuna mambo yanafanyika ni kufuru, kwa mfano lile nililosema kwa ujenzi wa meli. Meli moja kuna ki wakala huko pembeni kinalipwa dola milioni 2 kwa kila meli. Hiyo ni nini? Hiyo sio sawa, sijui kuna ujenzi wa barabara pesa itagaiwa kwanza weeee, barabara ikijengwa viwango vinakuwa compromised.
"Na sio barabara peke yake na mambo mengine, pesa inagawiwa kwanza kabla mradi haujafanywa, matokeo yake mradi unakuwa compromised. Na ndio maana sekta inakuwa ya mtu mmoja kuna mradi mkubwa basi serikali yote wanakuwa wasemaji wa ile sekta, ukiangalia kwa undani kila mmoja ameshakwenda kumuona aliyepata tenda hiyo kwa wakati wake kwahiyo maneno yanakuwa mengi kwa wakati mmoja, kwahiyo ndugu zangu lizingatieni hilo." - Rais Samia akiongea na Mawaziri na Manaibu Waziri