Awamu ya Sita na mbuzi kula kwa urefu wa kamba yake

Kiby

JF-Expert Member
Nov 16, 2009
6,899
4,623
Awamu ya jamaa yule hakuna mkuu wa taasisi kitengo au kaya aliyethubutu kutengeneza mkao wa kula jasho la wengine kupitia ofisi ya umma.

Leo hii katika hii awamu ya sita kila mbuzi kwenye ofisi ya umma anatafuta urefu wa kamba yake ni mrefu kiasi gani ili ajipimie ulaji wa kula bila kunawa mikono.

Elimu serikali ilitangaza kuwa ni bure lakini kiuhalisia ni zile ada zimebadilishwa jina kuitwa michango kama vile leo kodi ya mara mbili inaitwa tozo.

Shule za serikali zililipia ada ya elfu 70 wakati ule ila leo haiitwi ada bali michango na ni mara tano au hata mara kumi ya ile ada ya elfu sabini kwa mwaka.

Huo ukarabati na hiyo ujenzi wa ukuta ni lugha ya ulaghai au ni mimi sielewi?

Ni vema wizara ya elimu iondolewe ofisi ya rais sasa na irudi ofisi ya waziri mkuu maana raisi wa sasa ndiye mwenye falsafa ya mbuzi kula kwa urefu wa kamba.

Waziri mkuu yeye anatembea na falsafa ya rais wa awamu ya tano.
View attachment 2739586
 
Wahenga wanasema baada ya kauli ile inaonekana wengi wetu tuliridhika na kipenyo cha kamba zetu,ila kama kawaida kuna wale jamaa huwa hawaridhiki wakaamua kukata kamba kabisa.
 
Back
Top Bottom