Sababu kubwa ya Nyerere kumkataa Lowassa asiwe Rais ni utajiri wake uliotokana na urefu wa kamba yake wakati huo!

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Juzi hapa niliweka thread JF iliyosema wengi wa matajiri wa Tanzania ni wanasiasa na sio wafanya biashara, nikiwa na maana kwamba utajiri wao haujatokana na kufanya biashara bali umetokana na nafasi zao za kisiasa au uongozi serikalini kujitajirisha - urefu wa kamba zao. Kwa wengi wetu huo ni ufisadi.

Sasa hili kiongozi wa kisiasa au serikali kujitajrisha kutokana na nafasi yake, Raisi Samia alilihalalisha pale aliposema mtu atakula kwa urefu wa kamba yake. Kila mtu anajua kwamba urefu wa kamba aliousema Samia sio mshahara au marupurupu ya kazini, bali ni nafasi za kipato kisicho rasmi mtu anazopata kutokana na nafasi yake.

Sasa, mara ya kwanza Lowasa alipotaka kugombea uraisi, mwaka 1995, alikuwa tayari ni mtu tajiri sana tu. Aliweza hata kuzunguka nchi nzima kutafuta wadhamini kwa ndege ya kukodi. Na Lowasa hakuwahi kuwa mfanya biashara, na hivyo utajiri wake kwa kiasi kikubwa ulitokana na nafasi za uongozi alizokuwa amekuwa nazo hadi wakati huo - urefu wa kamba yake! Hilo lilimtatiza sana Nyerere, na hakuwa tayari kumruhusu mtu wa namna hiyo kuwa raisi wa Tanzania.

Hali siku hizi ni tofauti sana, hasa chini ya uongozi wa raisi Samia. Kimsingi Samia amehalalisha wanasiasa na viongozi wa serikali kutumia nafasi zao kujitajirisha, na wanapojitajirisha hauwaulizwi maswali yeyote! Katika hizi enzi, utajiri wa Lowasa kuwa ulitokana na nafasi za uongozi serikalini usingekuwa tatizo kwake kuwa raisi wa Tanzania! Hizi sio enzi za Nyerere tena.

Nyerere alijua wazi jambo moja ambalo labda Samia halielewi, kwamba katika nchi zote, watu wenye "kamba" za kuwaruhusu kula huwa si zaidi ya 10% ya raia wote nchini. Yaani wafanyakazi wa mshahara katika nchi huwa hawazidi 10% ya idadi ya raia nchini!

Samia alipotoa kauli ya mtu kula kwa urefu wa kamba yake, kuna watu niliwaambia kauli hiyo kimsingi ilitolewa ili kuhalalisha jambo ambalo Samia mwenyewe aliona anawezwa kusutwa nalo- yeye binafsi kula kwa urefu wa kamba yake ya urais, na hivyo akaona akisema kila mtu afanye hivyo basi hakuna atakaemshangaa yeye akifanya hivyo. Niliwaeleza watu kuwa, Samia anafanya hivi si kwa sababu yeye ni fisadi, bali ni jambo la kawaida katika tamaduni za kiarabu ambazo Samia ana asili nazo - kula kwa urefu wa kamba yako, na hata kuwalisha wanaokuzunguka!

Na of course, hilo pia watu wanapaswa kuelewa kwanini labda Wazanzibari kipindi hiki wamepata nafasi nyingi upande wa bara. Ni kawaida ya "nepotism" ambayo inatokana na tamaduni za kiarabu, kusaidia wale ambao unaona ni ndugu zako zaidi kuliko wengine. Sasa mindset zinazotokana na desturi za society, ni vigumu sana kumbadilisha mtu, na Watanzania wanapaswa kulielewa hilo, na kulivumilia kwa sasa.

Kwa mtu mwenye asili ya tamaduni za kiarabu, ukiwa na nafasi kama ya uraisi, basi utahakikisha watoto wako, wajomba, mashemeji, wakwe zako na ndugu zao, na hata rafiki za watoto wako, nk, wote wanafaidika na hata kutajirika na nafasi yako. "Nepotism" katika culture ya kiarabu, ambayo Samia inamhusu, ni jambo la kawaida, hawalionei aibu! Angalia katika serikali za kiarabu, uone nani wanapewa nafasi za uongozi wa nchi, nani ni matajiri - karibu wote wanakuwa ni wanaukoo!

Kwa mfano, ni rahisi sana kwa upande wa Zanzibar watoto wa maraisi waliopita nao pia kuja kuwa maraisi - na tumeliona hili tayari. Sintashangaa huko mbele mtu kutoka familia ya raisi Samia kuja kuwa raisi wa Zanzibar. Hii ni sehemu ya tamaduni za kiarabu, kurithishana au kupeana madaraka ndani ya ukoo. Nimeona baadhi ya Watanzania bara kuanza kuiga hii culture, kuwaandaa watoto wao kuja kuwa viongozi upande wa bara. Niwaonye mapema, huenda hili linakubalika upande wa Zanzibar kutokana na silka za kiarabu, lakini kwa bara litatuletea matatizo!
 
Kosa la Lowassa, lawama kwa Samia; Kivipi?
Samia alimaanisha mtu utapata ujira kulingana na ulipo usiwe na kijicho kwa nafasi ya mtu mwingine! Kwa fursa za kihalali kabisa zinatofautiana kati ya wizara na wizara na hii ni kawaida kabisa!

Sasa ukwasi usioeleweka wa Lowassa watu mnauhalalisha kwa kusema "aliuchukia umaskini kwa vitendo'! Shenziy kabisa hii inatofauti gani na trafiki anayeuchukia umaskini kwa vitendo kwa kuchukua rushwa?
 
Hakuna niliposema kosa la Lowasa lawama kwa Samia. Nimelinganisha hali ya wakati huo na sasa, kwa sababu wapo wanaoona Lowasa wakati huo alionewa, kwa sababu tu wanai-reflect hali ya wakati huo chini ya influence ya Nyerere wakitumia context ya sasa chini ya influence ya Samia. Inabidi uolewe uandishi katika comparative contexts

Na pia uelewe kwamba wewe unachoona ni rushwa labda aliyofanya Lowasa wakati huo, kwa sasa ndio kile kimehalalishwa kuwa ni kula kwa urefu wa kamba yako, na hili limehalalishwa na mamlaka ya juu kabisa nchini - raisi, bila kutolewa ufafanuzi. So anything goes.
 
Sio tamaduni za kiarabu tu.

Ni kwa nchi zote ambazo bado zimeng’ang’ana kubakia kwenye mfumo wa uchumi-jamii wa kikabaila.

Ila kama kweli maza ni memba wa royal family ya Oman basi mapinduzi ya Zanzibar ya 1964 yatakuwa yamezunguka full mduara.

Btw wapo wengi wanao argue kuwa mfumo wa ukabaila(feudalism), ndio bora zaidi ya mifumo mingine ya uchumi jamii iliyoibuka hapa duniani.

Bila shaka kwa wanufaika.
 
Juzi hapa niliweka thread JF iliyosema wengi wa matajiri wa Tanzania ni wanasiasa na sio wafanya biashara, nikiwa na maana kwamba utajiri wao haujatokana na kufanya biashara bali umetokana na nafasi zao za kisiasa au uongozi serikalini kujitajirisha - urefu wa kamba zao. Kwa wengi wetu huo ni ufisadi.

Sasa hili kiongozi wa kisiasa au serikali kujitajrisha kutokana na nafasi yake, Raisi Samia alilihalalisha pale aliposema mtu atakula kwa urefu wa kamba yake. Kila mtu anajua kwamba urefu wa kamba aliousema Samia sio mashahara, basi ni nafasi mtu anazopata kutokana na nafasi yake.

Sasa, mara ya kwanza Lowasa alipotaka kugombea uraisi, mwaka 1995, alikuwa tayari ni mtu tajiri sana tu. Aliweza hata kuzunguka nchi nzima kutafuta wadhamini kwa ndege ya kukodi. Na Lowasa hakuwahi kuwa mfanya biashara, na hivyo utajiri wake kwa kiasi kikubwa ulitokana na nafasi za uongozi alizokuwa amekuwa nazo hadi wakati huo - urefu wa kamba yake! Hilo lilimtatiza sana Nyerere, na hakuwa tayari kumruhusu mtu wa namna hiyo kuwa raisi wa Tanzania.

Hali siku hizi ni tofauti sana, hasa chini ya uongozi wa raisi Samia. Kimsingi Samia amehalalisha wanasiasa na viongozi wa serikali kutumia nafasi zao kujitajirisha, na wanapojitajirisha hauwaulizwi maswali yeyote! Katika hizi enzi, utajiri wa Lowasa kuwa ulitokana na nafasi za uongozi serikalini usingekuwa tatizo kwake kuwa raisi wa Tanzania! Hizi sio enzi za Nyerere tena.

Nyerere alijua wazi jambo moja ambalo labda Samia halielewi, kwamba katika nchi zote, watu wenye "kamba" za kuwaruhusu kula huwa si zaidi ya 10% ya raia wote nchini. Yaani wafanyakazi wa mshahara katika nchi huwa hawazidi 10% ya idadi ya raia nchini!

Samia alipotoa kauli ya mtu kula kwa urefu wa kamba yake, kuna watu niliwaambia kauli hiyo kimsingi ilitolewa ili kuhalalisha jambo ambalo Samia mwenyewe aliona anawezwa kusutwa nalo- yeye binafsi kula kwa urefu wa kamba yake ya uraisi, na hivyo akaona akisema kila mtu afanye hivyo basi hakuna atakaemshangaa yeye akifanya hivyo. Niliwaeleza watu kuwa, Samia anafanya hivi si kwa sababu yeye ni fisadi, bali ni jambo la kawaida katika tamaduni za kiarabu ambazo Samia ana asili nazo - kula kwa urefu wa kamba yako, na hata kuwalisha wanaokuzunguka!

Na of course, hilo pia watu wanapaswa kuelewa kwa nini labda Wazanzibari kipindi hiki wamepata nafasi nyingi upande wa bara. Ni kawaida ya "nepotism" ambayo inatokana na tamaduni za kiarabu, kusaidia wale ambao unaona ni ndugu zako zaidi kuliko wengine. Sasa mindset zinazotokana na desturi za society, ni vigumu sana kumbadilisha mtu, na Watanzania wanapaswa kulielewa hilo, na kulivumilia kwa sasa.

Kwa mtu mwenye asili ya tamaduni za kiarabu, ukiwa na nafasi kama ya uraisi, basi utahakikisha watoto wako, wajomba, mashemeji, wakwe zako na ndugu zao, na hata rafiki za watoto wako, nk, wote wanafaidika na hata kutajirika na nafasi yake. "Nepotism" katika culture ya kiarabu, ambayo Samia inamhusu, ni jambo la kawaida, hawalionei aibu! Angalia katika serikali za kiarabu, uone nani wanapewa nafasi za uongozi wa nchi, nani ni matajiri - karibu wote wanakuwa ni wanaukoo!

Kwa mfano, ni rahisi sana kwa upande wa Zanzibar watoto wa maraisi waliopita nao pia kuja kuwa maraisi - na tumeliona hili tayari. Sintashangaa huko mbele mtu kutoka familia ya raisi Samia kuja kuwa raisi wa Zanzibar. Hii ni sehemu ya tamaduni za kiarabu, kurithishana au kupeana madaraka ndani ya ukoo. Nimeona baadhi ya Watanzania bara kuanza kuiga hii culture, kuwaandaa watoto wao kuja kuwa viongozi upande wa bara. Niwaonye mapema, huenda hili linakubalika upande wa Zanzibar kutokana na silka za kiarabu, lakini kwa bara litatuletea matatizo!
Kurithishana madaraka kulingana na koo zao,huo ni upumbavu.
 
Ilikuwa ni Wivu tu wa mwalimu baada ya kuambiwa Lowassa ana kibanda pale SA

Edward hakuwa na Utajiri wowote ila hakuwa na mawazo ya Kimaskini
Hivi ulimfahamu Nyerere wewe, yule ambae aliimbisha watu kiongozi asiwe na nyumba ya kupangisha, asiwe na mishahara miwili, ungetegemea aruhusu tajiri Lowasa awe raisi, na akijua utajiri wa Lowasa haukutokana na biashara? Kumbuka tunaongelea 1995, ambapo matajiri Tanzania walikuwa watu kama Lowasa
 
Kurithishana madaraka kulingana na koo zao,huo ni upumbavu.
Nakubaliana nawe 100% Watu wanasema Mbona George Bush alikuwa raisi kama baba yake? Context ni tofauti sana. George Bush alijiwezesha, alienda through the ranks, hakuwa raisi kwa sababu ya mgongo wa baba yake. Na USA hutaungwa mkono kwa sababu wewe ni mtoto wa raisi, tofauti na huku kwetu
 
Hivi ulimfahamu Nyerere wewe, yule ambae aliimbisha watu kiongozi asiwe na nymba ya kupangisha, asiwe na mishahara miwili, ungetegemea aruhusu tajiri Lowasa awe raisi, na akijua utajiri wa Lowasa haukutokana na biashara? Kumbuka tunaongelea 1995, ambapo matajiri Tanzania walikuwa watu kama Lowasa
1995 Lowassa hakuwa miongoni mwa matajiri kwa Taarifa Yako

Ni kama leo Mbowe ana kibanda pale Dubai basi ndio iwe Nongwa

Ndio sababu Kenyatta alisema Nyerere anaongoza Maiti, ndio Nyie 🐼
 
Safi mlianza lazima watu wamalize ,msingeiba na kupeleka barabara mpaka kweny migomba wakati huo mkaacha miji ya kimkakati .

Pumbavu nchi mliharibu mnajimilikisha mpaka vijijini ili mfuge mifugo ...
 
Samia alimaanisha mtu utapata ujira kulingana na ulipo usiwe na kijicho kwa nafasi ya mtu mwingine! Kwa fursa za kihalali kabisa zinatofautiana kati ya wizara na wizara na hii ni kawaida kabisa!
Nukuu "Msile hadi mkavimbiwa".
Akili yangu inakataa ufafanuzi wako.
 
1995 Lowassa hakuwa miongoni mwa matajiri kwa Taarifa Yako

Ni kama leo Mbowe ana kibanda pale Dubai basi ndio iwe Nongwa

Ndio sababu Kenyatta alisema Nyerere anaongoza Maiti, ndio Nyie 🐼
Huenda nabishana na mtu ambae 1995 alikuwa hata hajazaliwa. Kwa standard ya Tanzania, 1995 mtu naepanda ndege kwa hela yake mwenyewe alikuwa tajiri.Mtu aliekodi ndege kuzunguka mikoa yote ya Tanzania alikuwa tajiri sana.

Leo unawafahamu wafanya kazi wangapi Tanzania wanaoweza kukodi ndege wakazungukia mikoa yote Tanzania? Je hutawaita matajiri hata kwa standard ya leo? Kwanza wewe bado unapanda basi kwenda mikoani halafu unataka kuniambia huoni wanajikatia tiketi za ndege ni matajiri kwako
 
Wanaopanda ndege ni wachache sn
 
Kwa Taarifa Yako ile ndege walikodi Temu na Mataka na walikuwa wanaitumia kila weekend kwenda Nairobi kula bata 😂😂

Haya mambo naweza kuongea na Mrangi tu Wakati huo nilikuwa NCCR mageuzi 😂😂🔥
 
Kosa la Lowassa, lawama kwa Samia; Kivipi?
Samia alimaanisha mtu utapata ujira kulingana na ulipo usiwe na kijicho kwa nafasi ya mtu mwingine! Kwa fursa za kihalali kabisa zinatofautiana kati ya wizara na wizara na hii ni kawaida kabisa!

Sasa ukwasi usioeleweka wa Lowassa watu mnauhalalisha kwa kusema "aliuchukia umaskini kwa vitendo'! Shenziy kabisa hii inatofauti gani na trafiki anayeuchukia umaskini kwa vitendo kwa kuchukua rushwa?
Umesema sawa ila hili la samia kusema vigogo wale kwa urefu wa kamba halina mashaka. Alimaanisha wale rushwa. Mwenyewe alisema anajua wanakula ila wale kwa kiasi. Kwa lugha yetu tanzania ukisikia mtumishi wa umma anakula ina maana anakula rushwa na kuiba mali ya umma. Kwa hili samia alionyesha hafai kua rais wa jamhuri. Ingekua kwa hizi nchi za magharibi zinajidai za kidemokrasia kwa kauli ile wangemwandama wapinzani wake hadi ajiuzulu. Kwa hiyo kauli alifungua mlango wa ulaji rushwa aliyokua amefanya kazi kubwa jpm kuufunga kwa watumishi wa umma. Kwa kauli hiyo aliwatoa hofu wala rushwa.
Samia wanamapinduzi ndani ya chama cha mapinduzi na nje ya chama cha mapinduzi hawana imani naye. Heshima yake itakua kuhakikisha nchi inapata kiongozi aina ya jpm 2025.
 
Sio tamaduni za kiarabu tu.

Ni kwa nchi zote ambazo bado zimeng’ang’ana kubakia kwenye mfumo wa uchumi-jamii wa kikabaila.

Ila kama kweli maza ni memba wa royal family ya Oman basi mapinduzi ya Zanzibar ya 1964 yatakuwa yamezunguka full mduara.

Btw wapo wengi wanao argue kuwa mfumo wa ukabaila(feudalism), ndio bora zaidi ya mifumo mingine ya uchumi jamii iliyoibuka hapa duniani.

Bila shaka kwa wanufaika.
Najiuliza mama akienda Oman wanaongeleaje nafasi yake ya kuwa raisi wa Tanzania? Maana kimsingi wale ndio waliopinduliwa, na leo mtoto wao amekuwa raisi wa nchi iliyowapindua!
 
Back
Top Bottom