Rais Samia: Kamera za Usalama zitaondoa Rushwa na ulazima wa kutumia 'Matrafiki' kila sehemu

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Akizungumza leo Sept. 4, 2023 wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi, Rais Samia amesema wananchi bado wanalalamikia tatizo la Rushwa hasa kwa Askari wa Barabarani.

Amesema “Mfano tukiweka Kamera za Barabarani hakutakuwa na sababu ya Askari kusimama Barabarani kusimamisha Magari, Teknolojia itatoa mwongozo wa kila kitu na Rushwa haitakuwepo,” .

Rais amesema amesema “Wimbo wa Polisi ni mzuri na leo kabla ya kuja hapa nilifungua YouTube nikausikiliza kisha nikaangalia Jeshi langu na kujiuliza ingekuwa yanayoimbwa hapa ndiyo yanayotendeka tungekuwa na Jeshi la Malaika.

=============

Rais Samia Suluhu Hassan amesema licha ya jitihada zinazoendelea kufanyika kuliboresha Jeshi la Polisi bado rushwa imekuwa mfupa mgumu kwa jeshi hilo.

Akizungumza leo Jumatatu Septemba 4, 2023 wakati wa ufunguzi wa kikao cha maofisa waandamizi wa jeshi la polisi Rais Samia amesema wananchi bado wanalalamikia rushwa hasa kwa askari wa barabarani.

“Wimbo wa polisi mzuri na leo kabla ya kuja hapa nilifungua youtube nikausikiliza kisha nikaangalia jeshi langu na kujiuliza ingekuwa yanayoimbwa hapa ndiyo yanayotendeka tungekuwa na jeshi la malaika.

Ukiachana wimbo na slogan yenu nzuri sana lakini je mnayatekeleza? IGP (Mkuu wa Jeshi la Polisi) naomba sana simamia utekelezaji wa wimbo na slogan ili jeshi liwe na sifa ile ya kimataifa,” amesema Rais Samia.

Hata hivyo amebainisha kuwa tatizo la rushwa kwa askari wa barabarani litapatiwa ufumbuzi baada ya uwekezaji kufanyika kwenye teknolojia.

“Wakati mwingine ni vigumu kubadilisha tabia lakini inaweza kurekebishika kukiwa na teknolojia inayolazimisha watu wafuate teknolojia inavyotaka.

“Mfano tukiweka kamera za barabarani hakutakuwa na sababu ya askari kusimama barabarani kusimamisha magari teknolojia itatoa mwongozo wa kila kitu na rushwa haitakuwepo,” amesema.

Rais Samia amefafanua uwekezaji huo ukifanyika kwenye teknolojia itasaidia kupunguza idadi ya askari barabarani na itawezesha kupatikana wa kwenda kwenye maeneo mengine yenye uhitaji.

MWANANCHI
 
Yes kwa makosa ya speed na bima itakuwa ni vuziru kutumia kamera, lakini sidhani kama kamera pekee yake zitaweza fanya inspection ya ubora wa magari, kukagua mizigo na mengineyo, bado watahitajika askari kwaajiri ya ukaguzi wa magari. Labda ukaguzi kama huu pia ufanyike sehemu ambazo zina kamera pia
 
Nimemsikia Rais Samia alisema Serikali itapinguza idadi ya Askari Polisi Barabarani Kwa kutumia teknolojia ya kamera maeneo mbali mbali.

My Take
Ni jambo jema ila Sasa Trafiki watakula wapi?
 
Ni kweli my President, ona kati ya Dar na Morogoro ni 194km,ila kuna check points zaidi ya 27!!!,Kasane hadi Gabbs ni 800km,kuna check points 3 tu,Cpt to joberg ni 1400km ,no check points at all !!!
Aisee...
 
Very true. Wenzetu walifunga miaka 100 iliyopita, sisi bado tupo kwe ass.h. countries. Tujiongeze! Hata pinhole camera hatuna. Go go do it.
1693833323379.png
 
Sidhani kama serikali ya ccm inaweza kuwazuia police kukusanya rushwa. Wenyewe ccm wako madarakani kwa kuiba kura, wanawezaje kuwazuia wenzao kupokea rushwa?
 
Kwanza hata hyo mishahara masikini ya mungu askari wanapewa kid kiduchu sana makazi yao pia ni duni ssa mnapowafungiwa kamera ni kuwakosesha watoto wao njaaaa
Mbona kuna askari kutwa po kaunta na bank au wao hawana watoto? elimu zao ni F4 lakini mishahara yao ni kuanzia 800,000 nje na ration 300,000 unataka nini zaidi ya hapo?
 
Zitakuwa zinaharibika kila siku...na traffic polisi watafanya hivyo ili mchezo uendelee

Na labda zitumie solar, kama ni umeme bado ni tatizo
 
Back
Top Bottom