Serikali Yaanza Ufungaji Camera Magerezani

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,909
946
Serikali imeanza Ufungaji wa Kamera maalumu(CCTV) katika maeneo mbalimbali yanayozunguka magereza lengo ikiwa ni Uboreshaji wa Huduma za ulinzi na usalama pamoja na kwenda na dhana nzima ya sayansi na teknolojia katika utoaji na ufuatiliaji wa huduma kwa wadau mbalimbali wanaoshilikiana na Jeshi la Magereza ikiwemo Jeshi la Polisi na Mahakama.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Kamishna wa Jeshi la Magereza, Jeremia Katungu wakati akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo wakati wa mkutano uliohusisha Uongozi wa juu wa jeshi hilo, Maafisa, Askari na watumishi raia huku akitaja baadhi ya mikoa ambapo kamera hizo zimefungwa.

‘Tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuliwezesha jeshi katika maeneo mbalimbali ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake, baadhi ya maeneo hayo ni ununuzi wa vifaa vya ulinzi na usalama katika maeneo yanayozunguka magereza kwa nje ambapo kwa sasa zoezi la usimikaji wa vifaa hivyo kwa sasa unaendelea katika maeneo ya magereza ya Maweni, Karanga, Moshi, Lwanda na Tabora’.alisema

Ameyataja maeneo mengine yaliyoboreshwa na serikali ya awamu ya sita kuwa ni vyombo vya usafiri,ajira,upandishwaji vyeo kwa askari na maafisa ambapo hadi sasa jumla ya ajira 662 ziko katika mchakato wa usaili huku upandishwaji vyeo mpaka sasa askari na maafisa 4111 wamepandishwa vyeo.

Akizungumza katika kikao hicho, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Daniel Sillo amewataka Askari wa Jeshi la Magereza kuwa ni nidhamu katika utendaji wao wa kazi ili kujiepusha na tuhuma mbalimbali ambazo zitalichafua jeshi huku akimpongeza Rais Daktari Samia Suluhu Hassani kwa msaada anaotoa kwa vyombo vya ulinzi na Usalama likiwemo Jeshi la Magereza.

GLEhojFWMAAhjSL.jpg
GLEhoi-XsAELpiR.jpg
GLEhoi-WAAAyFQw.jpg
WhatsApp Image 2024-04-13 at 21.17.02.jpeg
 
View attachment 2962679View attachment 2962680View attachment 2962681View attachment 2962682
Hizo kamera ni kwa ajili ya kuwaona wafungwa wanao toroka au watu wanaotaka kuvamia magereza? Mimi nadhani zingefungwa ndani ya magereza ili kuhakikisha usalama wa wafungwa na askari wanaowahudumia. Pamoja ni rahisi zaidi kuzuia utoro kabla haujatokea kuliko ukishatokea.

Amandla...
 
Ehh kumbe miaka yote hiyo camera cctv zilikuwa hakuna

Ova
 
Back
Top Bottom