Chalamila: Sijaona Rais Samia ukielekeza Ukatoliki au Ulutherani wa mtu kufanya mambo unayoyataka

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akishiriki ufunguzi wa Kikao kazi cha Maafisa waandamizi wa Jeshi la Polisi, Oystebay, leo Septemba 4, 2023.

View: https://www.youtube.com/live/Ft4BQNhtlHE?si=wnu_34cmAx82c_0X
70fcf6fb-05b7-47a1-9f09-143d8f7abca3.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan akikagua kikosi cha gwaride mara baada ya kuwasili kwenye Bwalo la Maafisa wa Polisi (Police Officer’s Mess) Oysterbay Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Septemba, 2023.

CHALAMILA: SIJAONA RAIS UKIELEKEZA UKATOLIKI AU ULUTHERANI WA MTU KUFANYA MAMBO UNAYOYATAKA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema “Sijawahi kuona Rais ukielekeza Ukatoliki wetu au Ulutherani wa mtu mwingine kufanya mambo ambayo unayataka, ungesimama na kuanza kutuelekeza tungekuwa tumepoteza mwelekeo.

Kama kuna mtu yeyote atasimama kukuelekeza wewe na Serikali yako kufanya vitu ambavyo wanataka iwe hivyo, naomba usimame na unyooshe kamba kwa kuwa utapimwa kwa matokeo.

Simama katika mstari, hatuko tayari kuona Rais ukitukanwa na kurushiwa mawe, Polisi wameimba wakikuvaa tutawavaa, na mimi kama Mkuu wa Mkoa wa Dar naahidi wakikuvaa nitawavaa.
d3b5f0ec-0660-4f00-9160-1fe53e5c9457.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi. Hamad Masauni wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Maafisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi, Makamanda wa Polisi wa Mikoa pamoja na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa Polisi (Police Officer’s Mess) Oysterbay Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Septemba, 2023.​
2f91824f-4127-4c25-b372-f63254094620.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi, Samia Suluhu Hassan akihutubia kabla ya kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, Makamanda wa Polisi wa Mikoa pamoja na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa Polisi (Police Officer’s Mess) Oysterbay Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Septemba, 2023.

Rais Samia anazungumza
Rais Samia amepongeza jeshi la polisi kwa kupunguza uhalifu nchini, amewaomba kuimarisha dhana ya ulinzi shirikishi, wananchi wawe huru kufanya shughuli zao bila hofu ya kuvamiwa na majambazi.

“Bado napokea vikaratasi vya tatizo la kubambikwa kesi kwenye vituo vya polisi ambalo nalo naomba sana mlitupie macho, ili wale wanaopelekwa basi wawe na makosa ya kweli na sio ya kukomoana. Wananchi pia wanalalamika nasi tunayasikia hatuna budi kuyaleta kwenu ili yaweze kufanyiwa kazi” -Rais Samia

Kuhusu tabia ya kuomba rushwa hasa kwa Polisi wa usalama Barabarani, Rais Samia amesema teknolojia inaweza kusaidia kuondoa rushwa hizi na Serikali itaendelea kutumia teknolojia ili pia namba ya askari hao itumike kwa kazi zingine.

Amelipongeza pia jeshi hilo kwa kutambua na kuwapongeza askari wanaofanya vizuri ili kuwatia ari ya kufanya vizuri na wale wanaofanya vibaya waathibiwe au kuambiwa ili watambue tabia zao.

"Kuna magari mabovu yanayotembea barabarani, tunakuja na mfumo wa ukaguzi wa lazima wa TEHAMA, ukaguzi wa magari kwa lazima. Mtu akitaka atalikagua gari lake hataki atalipeleka likaguliwe kwa mfumo tu, itabidi lazima likaguliwe" amesema Rais Samia.

Aidha, Serikali inakuja na mfumo wa utambuzi na uchakataji wa taarifa za wahalifu ili kama inavyofanyika Ulaya, Sura ya mhalifu ikiwekwa taarifa zake zote zinapatikana.

Akizungumzia kuhusu kikokotoo, Rais Samia amesema Serikali inafanyia kazi.

"Tupo tunakifanyia kazi na kuona jinsi tutakavyoenda vizuri kwa sababu masuala ya kikokotoo haya si tu matakwa ya Serikali kutaka kuja na kikokotoo, ni hali ya uchumi na hali ya mifuko yenu ilivyo. Ni hali ya mifuko ilivyo. Tukisema kila anayetoka boom lako hilo hapo, boom lako hilo hapo, miaka 2 tu mifuko ile imekauka."

Ameongeza, "Tuliweka hivi ili kuweka sustainability ya mfuko, sasa kwa sababu imepigiwa kelele sana sio tu na jeshi la polisi lakini na wengine, tutakwenda kuangalia sababu tunasema siku zote Serikali yenu ni sikivu. Tutakwenda tuangalie njia nzuri tunayoweza kufanya ili kikokotoo kisilete maneno mengi."
1ff9c022-beb8-4f08-aa31-60bf309079b3.jpg

bd5ba713-a683-48be-9415-f9b23d0cd4df.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan akipokea taarifa ya Jeshi la Polisi kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Camillus Wambura mara baada ya kuwasili kwenye Bwalo la Maafisa wa Polisi (Police Officer’s Mess) Oysterbay Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Septemba, 2023.
f3afa6eb-c8f5-4433-9898-e043a54bddc3.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi wa Jeshi la Polisi mara baada ya kuwasili kwenye Bwalo la Maafisa wa Polisi (Police Officer’s Mess) Oysterbay Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Septemba, 2023.
 
Acha kukariri wewe, angalia Rais wa Zambia, lazima uishi kulingana na uwezo wako, umewahi kuona Waziri wa Uingereza ana V8 kama hawa wa kwetu?
Sasa ya Zambia na uingereza yanashabiana Vipi na mambo ya Tz??yaani wewe Kwa mf:Wewe Mzee shirima huwezi ishi Kwa kumuiga Mzee Urassa!!
Acha kukariri wewe, angalia Rais wa Zambia, lazima uishi kulingana na uwezo wako, umewahi kuona Waziri wa Uingereza ana V8 kama hawa wa kwetu?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akishiriki ufunguzi wa Kikao kazi cha Maafisa waandamizi wa Jeshi la Polisi, Oystebay, leo Septemba 4, 2023.

CHALAMILA: SIJAONA RAIS UKIELEKEZA UKATOLIKI AU ULUTHERANI WA MTU KUFANYA MAMBO UNAYOYATAKA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema “Sijawahi kuona Rais ukielekeza Ukatoliki wetu au Ulutherani wa mtu mwingine kufanya mambo ambayo unayataka, ungesimama na kuanza kutuelekeza tungekuwa tumepoteza mwelekeo.

Kama kuna mtu yeyote atasimama kukuelekeza wewe na Serikali yako kufanya vitu ambavyo wanataka iwe hivyo, naomba usimame na unyooshe kamba kwa kuwa utapimwa kwa matokeo.

Simama katika mstari, hatuko tayari kuona Rais ukitukanwa na kurushiwa mawe, Polisi wameimba wakikuvaa tutawavaa, na mimi kama Mkuu wa Mkoa wa Dar naahidi wakikuvaa nitawavaa.

Huyu ndio chawa wa mama Sasa

View: https://www.instagram.com/p/Cww7wz9q6g4/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akishiriki ufunguzi wa Kikao kazi cha Maafisa waandamizi wa Jeshi la Polisi, Oystebay, leo Septemba 4, 2023.

CHALAMILA: SIJAONA RAIS UKIELEKEZA UKATOLIKI AU ULUTHERANI WA MTU KUFANYA MAMBO UNAYOYATAKA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema “Sijawahi kuona Rais ukielekeza Ukatoliki wetu au Ulutherani wa mtu mwingine kufanya mambo ambayo unayataka, ungesimama na kuanza kutuelekeza tungekuwa tumepoteza mwelekeo.

Kama kuna mtu yeyote atasimama kukuelekeza wewe na Serikali yako kufanya vitu ambavyo wanataka iwe hivyo, naomba usimame na unyooshe kamba kwa kuwa utapimwa kwa matokeo.

Simama katika mstari, hatuko tayari kuona Rais ukitukanwa na kurushiwa mawe, Polisi wameimba wakikuvaa tutawavaa, na mimi kama Mkuu wa Mkoa wa Dar naahidi wakikuvaa nitawavaa.

Asiyemfahamu huyo CHAWA na bendera fuata upepo, ndiye pekee atakayepata shida. Huyo jamaa akili yake siku zote huwa anaihifadhi tumboni, badala ya kichwani.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akishiriki ufunguzi wa Kikao kazi cha Maafisa waandamizi wa Jeshi la Polisi, Oystebay, leo Septemba 4, 2023.

CHALAMILA: SIJAONA RAIS UKIELEKEZA UKATOLIKI AU ULUTHERANI WA MTU KUFANYA MAMBO UNAYOYATAKA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema “Sijawahi kuona Rais ukielekeza Ukatoliki wetu au Ulutherani wa mtu mwingine kufanya mambo ambayo unayataka, ungesimama na kuanza kutuelekeza tungekuwa tumepoteza mwelekeo.

Kama kuna mtu yeyote atasimama kukuelekeza wewe na Serikali yako kufanya vitu ambavyo wanataka iwe hivyo, naomba usimame na unyooshe kamba kwa kuwa utapimwa kwa matokeo.

Simama katika mstari, hatuko tayari kuona Rais ukitukanwa na kurushiwa mawe, Polisi wameimba wakikuvaa tutawavaa, na mimi kama Mkuu wa Mkoa wa Dar naahidi wakikuvaa nitawavaa.

Hivi siku anaapishwa anakumbuka alitamkanini?
 
Back
Top Bottom