Rais Samia: Fedha ambazo zingegharamia Sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, zigawanywe sawa

Nguruvi3,

..thank u for tagging me on this thread.

..kwa kweli mimi concern yangu haiko kwenye suala la muungano sasa hivi.

..kinachonifikirisha sasa hivi ni kama ktk utawala wa Mama Samia Suluhu MAUAJI yatakoma au tutaendelea kusumbuliwa na WASIOJULIKANA?

..masuala yote mengine ni secondary, ninachoomba ni Mama Samia Suluhu akomeshe dhuluma na ukatili wa awamu ya 5, arejeshe HAKI kwa kila Mtanzania.
Naunga mkono hoja.
P
 
Hili waliliondoa mapema baada ya kusikia kuna mafuta na gesi. Walichotaka ni kuwa rasilimali zao zisitumike katika muungano. Hapa chini umeeleza vizuri sana

Kwakweli inasikitisha sana. Si hayo tu kuna mengi sana
1. Wametaka 21% ajira za muungano. Katika hiyo 21% ajira wanazopata Wazanzibar hazihusu mambo ya muungano. Kwa mfano, Mzanzibar anaajiriwa TAMISEMI, Wizara ya maji, Mawasiliano, Mifugo n.k. kwa sababu zipi

Lakini pia wanataka waajiriwe katika taasisi zisizo za muungano kama TBS wakati kuna ZBS
Kwa Zanzibar 21% ya ajira za muungano ni nyingi kuliko ajira za SMZ.

Licha ya fadhila hizo za ajira bado wanalipwa na JMT ambayo pesa zake zinatoka hazina Dar.
Hakuna ushahidi wowote wa Zanzibar kuchangia muungano kwa miaka takribani 40 sasa.

Kuna masuala ya gharama za muungano. Hapa hutawasikia Wazanzibar wakieleza nini mchango wao
Mathalani, wanachangia nini katika kuendesha wizara ya mambo ya nje! Lakini utawasiki wanataka nafasi sawa za uteuzi katika ubalozi.

Kuna suala la Wabunge! Ikiwa tunasema asilimia 4% ya mapato ya BoT ambayo ni mapato ya rasilimali na kodi za Watanganyika iende Zanzibar, ni vipi basi SMZ haihudumii wawakilishi wanaokuja Dodoma Bungeni?
Wale Wazanzibar wapo Bungeni kwa ajili ya Zanzibar katika mambo yasiyozidi 7. Kwanini Hazina Tanganyika ibebe mzigo wa kuwahudumia ?

Elimu ya Juu: Hili si suala la muungano. Kuna HESLB na ZHESLB . Kwanini basi HSELB ya bara iwape 'msaada; na si mkopo wanafunzi wa Zanzibar kwa wingi zaidi kuliko mkopo unaotolewa na ZHESLB?

Kuna suala la Akaunti ya pamoja ya fedha. Ukiuliza ni ya nini , Wazanzibar watakwambia ni ya kugawana misaada na fedha. Hakuna Mzanzibar atakayekuambia akaunti hiyo ni ya kuchangia na kutoa! hapana! wao ni kutoa tu

Zanzibar ina watu milioni 1.2 na nusu yao wanaishi Tanganyika. Kwa maana kwamba at anytime Zanzibar inakuwa na approx. watu laki 600. Kwa mwendo huu wa kuchota , sidhani kam wanasababu ya kufanya kazi.

Hawana sababu ya kufanya kazi kwasababu kadri mnavyolipa kodi bara, mnavyotumia rasilimali zenu wao wana mtego wa 4% . Sasa piga hesabu ya 4% ya pato la watu milioni 50 wa Tanganyika!

Suluhu hapa ni moja turejee katika rasimu ya Warioba, mambo 7 tu! mengine kila nchi ijishughulishe

Tanganyika inatoa resources nyingi sana kwenda kuhudumia eneo ambalo kwa Tanganyika ni jimbo moja la uchaguzi, huku tukiacha maeneo yanayochangia sana katika Pato la Taifa bila resources. Ni kwa dividend or return gani? Nani wa kumsemea ''Tanganyika'?

Tunabeba lawama za bure kwa fadhila tunazotoa. Je, haitoshi?

Kwasasa ''Changu ni Chetu, chako ni chako'' na hii ifike mwisho.

JokaKuu Pascal Mayalla Ngongo
Mkuu Nguruvi3 , ratio ya mgao wa Zanzibar ni 4.5% ya mapato ya misaada na mikopo ya kimataifa kwa Tanzania. Pato hili sio unyonyaji, sio hisani, ni deserving kwa Zanzibar kwasababu the status of Zanzibar ndani ya muungano ni equal partners, kufuatia Zanzibar kupoteza it's sovereignty ndani ya muungano, Zanzibar haiwezi kukopa mkopo wowote wa kimataifa, kwa ajili ya maendeleo ya Zanzibar, kwasababu kimataifa Zanzibar sio nchi. Katika kupoteza sovereignty yake, sio Zanzibar tuu iliyopoteza bali Tanganyika nayo sio tuu ilipoteza sovereignty yake bali taifa la Tanganyika lilikufa kabisa na kujikabidhi kwa Tanzania.

Nje ya Muungano, Kimataifa set up ya muungano wetu union, Tanzania ni taifa moja tuu la URT, or JMT chini ya rais mmoja, rais wa JMT, na chini ya serikali moja, serikali ya JMT. Hili ndilo taifa linalotambulika kimataifa, ndilo linalokopeswa na lenye uwezo wa kukopa na ndilo linalopokea misaada yote ya kimataifa.

Ndani ya Muungano Kitaifa, set up ya muungano wetu ni muungano wa federation, ni muungano wa nchi mbili, zenye maeneo mawili tofauti, yaani territories mbili za Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, au Tanzania Zanzibar, zenye serikali mbili ya JMT na SMZ, zenye marais wawili, rais wa JMT na rais wa SMZ wenye hadhi sawa, ndio maana Rais Samia kwenye protocol ya Muungano, anaanza na kumtaja kwanza rais wa Zanzibar, ndipo anakuja kwa makamo wa rais wa JMT.

Kwa vile rais wa JMT, japo ni rais wa muungano, kimataifa, lakini pia ni rais wa Tanganyika kitaifa kwa mambo ambayo sio ya muungano. Sasa miaka yote ya nyuma, mikopo na misaada yote ya kimataifa inayokopwa na Tanzania, au Tanzania tunayopata kama nchi, ilikuwa inaishia upande mmoja tuu wa muungano huku bara. Zanzibar ilikuwa haipati. Ndipo ikaamuliwa kuanzia sasa, mikopo na misaada yote ya kimataifa ya Tanzania, Zanzibar ina mgao wake wa asilimia 4.5%. Na sio asilimia ya pato la taifa!. Mgao ni wa mikopo tuu na misaada ya kimataifa.

Sambamba na mgao huu wa asilimia 4.5%, sasa pia Zanzibar inaruhusiwa kukopa mikopo ya kimaendeleo kutoka ma benki na mashirika ya kimataifa kwa udhamini wa serikali ya JMT, yaani kupata government guarantee.

Tukija kwenye issues za uraia na ajira, kila Mzanzibari, ni Mzanzibari kwanza kisha ni Mtanzania, anazo haki zote za kiraia kama Mtanzania mwingine yoyote, ikiwemo ajira, kumiliki mali, kununua ardhi, na kuajiriwa sehemu yoyote serikalini na sekta binafsi hata wizara ambazo sio za muungano.

Lakini kwa upande wa Watanzania, sii kila Mtanzania ni Mzanzibari!. Hivyo Mtanzania ambaye sio Mzanzibari, hawezi kuajiriwa SMZ wala kumiliki ardhi kule, haki hiyo ni haki kwa Watanzania tuu ambao pia ni Wazanzibari.

Kwenye huu muungano wetu kuna kitu kinaitwa the dominant factor and the minority. Tanganyika ndio dominant na Zanzibar ndio the minority. Tanzania tulipounganisha vyama vya Tanu na ASP ile 1977, tuliendelea na serikali mbili ili kuelekea kuwa na serikali moja, hivyo kukazushwa dhana ya Tanganyika kutaka kuimeza Zanzibar. Sasa tukajijuta tukitumia vigezo sawa, Wanzanzibari watajikuta they just can't compete, hivyo Watanzania bara kujikuta tume dominate muungano, ndipo ikaamuliwa a quotas system ya nafasi za ajira kwenye serikali ya JMT na elimu juu, Wanzanzibari pia watengewe.

Mwisho, Mkuu Nguruvi3, muungano ni kama ndoa, posa imetolewa, ndoa imefungwa, kuna mume na mke, mume anayempenda mkewe kwa dhati, haoni ugumu wowote kumuhudumia mkewe. Mke ni pambo la nyumba. Kama umependa, ukaposa, ukaoa, na mke unampenda kwa dhati, utamuhudumia!.

Kwangu mimi sio ugumu wowote kwenye hili, tafadhalini sana, tusilete mambo ya upare katika muungano. Japo the Articles of Union, zilisema muungano utahudumiwa na pande zote kwa kuanzishwa mfuko maalum wa kuhudumia muungano. Zanzibar alichangia kidogo gharama za uendeshaji wa muungano pale mwanzo, baadaye alipogindua kuwa serikali ya muungano pia ndio serikali ya Tanzania bara kwa mambo ambayo sio ya muungano, akajikuta anagharimia kitu asichokijua, hivyo akasitisha kuchangia na toka hapo ni bara ndio pekee imekuwa iki gharimia kuendesha muungano. Zanzibar wao ni kula kulala tuu!. Hivyo msharika mmoja wa muungano kuonekana kama mume, akigharimika, huku msharika mwingine yeye akilala amebweteka, kula kulala!. Jee kuna shida gani kwa mkeo unaempenda akiwa kula kulala?.

Kwa hali hii unkubaliana na wanaosema eti Muungano umebakiza kero chache ndogo ndogo?
 
Yes, Muungano ni ndoa, hakuna ndoa isiyo na kero. Kwenye kero za muungano, mifumo tayari imeishajengwa iko in place umebaki utekelezaji tuu wa kutatua kero ndogo ndogo.

Ila kuna kero fulani kubwa mpya haitajwi, hii ni kero ya Katiba ya Zanzibar. Katiba ya JMT inasema Tanzania ni nchi moja ya JMT, Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani. Katiba ya Zanzibar inasema Tanzania ni Jamhuri ya Muungano wa nchi mbili , wa nchi iliyokuwa Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, na kuendelea kuitaja mipaka ya Zanzibar, wimbo wake wa taifa, bendera na vyombo vyake vya ulinzi na Vikosi vya SMZ.

Katiba hiyo ya Zanzibar, katiba ya JMT haitambui, hivyo ni ama katiba ya JMT iitambue katiba ya Zanzibar, au Katiba ya Zanzibar Ibadilishwe iendane na Katiba ya JMT.

P
 
Muliidhulumu sana Zanzibar tokea uhuru at least mama aonyeshe kwamba nchi 2 ziliungana hivo faida iwe 50-50
Nawe unabwabwaja hapa hata aibu huna, Zanzibar ilidhulumiwa kipi?. Kati ya Zanzibar na Tanganyika nani anadhulumiwa kama uko mkweli.Hakuna mzanzibari aliyewahi ongoza nchi ya Tanzania ikawa na maendeleo, mama akifanikiwa atakuwa wa kwanza ila kwa mwendo wake ni wale wale kila kitu ruksa, ruksa yakhe.
 
Television ya kwanza ilitazamwa Zanzibar kuliko nchi nyingi za Africa ikiwemo Afrika kusini, kusema zanzibar hakuna kiongozi wa aliyeleta maendeleo ni kiburi chako tu, umesahau kwaba Tanganyika wamepeleka ofisi za TRA kule Zanzibar zinakusanya kodi kwa ajili ya Maendeleo ya Tanganyika tu pamoja na mishahara yenu inatoka humo humo lakini nikukumbushe zaidi BOT ilianzishwa Wazanzibari wakiwa wachangiaji wakubwa walitoa fedha zao za kigeni nyingi kuliko Tanganyika lakini leo BOT inafanywa kama ni zao la Tanganyika pekee.,

Ndio mana Lukuvi alisema waziwazi Tanganyika haitaweza kuicha na kuikalia kimabavu zanzibar sababu ni ile ile tu ndio inayokupeni maendeleo yenu huko na hizo fly over zote mnapata hela kutoka Zanzibar.,

Watanganyika walioko zanzibar hawazalishi mali yoyote wanauza dawa za panya, viroboto na kulima viazi vitamu tu hawana kodi wanayolipa mahali popote., Wazanzibari wamewafadhili majumba ya kukaa bila ya kulipa kodi, wanaishi bure na kila leo wanapigiana simu wanaendelea kuja kuishi zanzibar na familia zao.

Sasa unapokuja na hoja kuhusu Zanzibar tambua ndio wanakufanya wewe leo uwe na kiburi kiasi hicho, hamna shukurani.
 
Yes, Muungano ni ndoa, hakuna ndoa isiyo na kero. Kwenye kero za muungano, mifumo tayari imeishajengwa iko in place umebaki utekelezaji tuu wa kutatua kero ndogo ndogo.

Ila kuna kero fulani kubwa mpya haitajwi, hii ni kero ya Katiba ya Zanzibar. Katiba ya JMT inasema Tanzania ni nchi moja ya JMT, Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani. Katiba ya Zanzibar inasema Tanzania ni Jamhuri ya Muungano wa nchi mbili , wa nchi iliyokuwa Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, na kuendelea kuitaja mipaka ya Zanzibar, wimbo wake wa taifa, bendera na vyombo vyake vya ulinzi na Vikosi vya SMZ.

Katiba hiyo ya Zanzibar, katiba ya JMT haitambui, hivyo ni ama katiba ya JMT iitambue katiba ya Zanzibar, au Katiba ya Zanzibar Ibadilishwe iendane na Katiba ya JMT.

P
Mpaka hapa sijui ni ipi kubwa kati ya Katiba ya Zanzibar na Katiba ya Tanzania.
1.Ukiwa Zanzibar wanafuata kwanza Katiba ya Zanzibar kisha Katiba ya Tanzania, na hata usipoizingatia Katiba ya Tanzania wala huna kosa maana wewe ni Mzanzibari kwanza.
2.Ukiwa bara hata kama kwenu ni Zanzibar unatawaliwa na Katiba ya Tanzania pekee na hata ukiitukana katiba ya Zanzibar haihusu.
Katiba moja hsiitambui wala kuitaja nyingine, Katiba ya Zanzibar haiitaji wala kusema chochote kuhusu katiba ya Tanzania na kinyume chake.

Nisaidie kujua ipi kubwa kati ya Katiba ya Zanzibar na Katiba ya Tanzania?
 
Hili waliliondoa mapema baada ya kusikia kuna mafuta na gesi. Walichotaka ni kuwa rasilimali zao zisitumike katika muungano. Hapa chini umeeleza vizuri sana

Kwakweli inasikitisha sana. Si hayo tu kuna mengi sana
1. Wametaka 21% ajira za muungano. Katika hiyo 21% ajira wanazopata Wazanzibar hazihusu mambo ya muungano. Kwa mfano, Mzanzibar anaajiriwa TAMISEMI, Wizara ya maji, Mawasiliano, Mifugo n.k. kwa sababu zipi

Lakini pia wanataka waajiriwe katika taasisi zisizo za muungano kama TBS wakati kuna ZBS
Kwa Zanzibar 21% ya ajira za muungano ni nyingi kuliko ajira za SMZ.

Licha ya fadhila hizo za ajira bado wanalipwa na JMT ambayo pesa zake zinatoka hazina Dar.
Hakuna ushahidi wowote wa Zanzibar kuchangia muungano kwa miaka takribani 40 sasa.

Kuna masuala ya gharama za muungano. Hapa hutawasikia Wazanzibar wakieleza nini mchango wao
Mathalani, wanachangia nini katika kuendesha wizara ya mambo ya nje! Lakini utawasiki wanataka nafasi sawa za uteuzi katika ubalozi.

Kuna suala la Wabunge! Ikiwa tunasema asilimia 4% ya mapato ya BoT ambayo ni mapato ya rasilimali na kodi za Watanganyika iende Zanzibar, ni vipi basi SMZ haihudumii wawakilishi wanaokuja Dodoma Bungeni?
Wale Wazanzibar wapo Bungeni kwa ajili ya Zanzibar katika mambo yasiyozidi 7. Kwanini Hazina Tanganyika ibebe mzigo wa kuwahudumia ?

Elimu ya Juu: Hili si suala la muungano. Kuna HESLB na ZHESLB . Kwanini basi HSELB ya bara iwape 'msaada; na si mkopo wanafunzi wa Zanzibar kwa wingi zaidi kuliko mkopo unaotolewa na ZHESLB?

Kuna suala la Akaunti ya pamoja ya fedha. Ukiuliza ni ya nini , Wazanzibar watakwambia ni ya kugawana misaada na fedha. Hakuna Mzanzibar atakayekuambia akaunti hiyo ni ya kuchangia na kutoa! hapana! wao ni kutoa tu

Zanzibar ina watu milioni 1.2 na nusu yao wanaishi Tanganyika. Kwa maana kwamba at anytime Zanzibar inakuwa na approx. watu laki 600. Kwa mwendo huu wa kuchota , sidhani kam wanasababu ya kufanya kazi.

Hawana sababu ya kufanya kazi kwasababu kadri mnavyolipa kodi bara, mnavyotumia rasilimali zenu wao wana mtego wa 4% . Sasa piga hesabu ya 4% ya pato la watu milioni 50 wa Tanganyika!

Suluhu hapa ni moja turejee katika rasimu ya Warioba, mambo 7 tu! mengine kila nchi ijishughulishe

Tanganyika inatoa resources nyingi sana kwenda kuhudumia eneo ambalo kwa Tanganyika ni jimbo moja la uchaguzi, huku tukiacha maeneo yanayochangia sana katika Pato la Taifa bila resources. Ni kwa dividend or return gani? Nani wa kumsemea ''Tanganyika'?

Tunabeba lawama za bure kwa fadhila tunazotoa. Je, haitoshi?

Kwasasa ''Changu ni Chetu, chako ni chako'' na hii ifike mwisho.

JokaKuu Pascal Mayalla Ngongo
Swala la kushangaza zaidi wakitokea watu au kikundi cha watu mfano hai Uwamsho, swala la kusema wanataka Zanzibar huru wanawekwa ndani, hii imekaaje nayo?
 
Television ya kwanza ilitazamwa Zanzibar kuliko nchi nyingi za Africa ikiwemo Afrika kusini, kusema zanzibar hakuna kiongozi wa aliyeleta maendeleo ni kiburi chako tu, umesahau kwaba Tanganyika wamepeleka ofisi za TRA kule Zanzibar zinakusanya kodi kwa ajili ya Maendeleo ya Tanganyika tu pamoja na mishahara yenu inatoka humo humo lakini nikukumbushe zaidi BOT ilianzishwa Wazanzibari wakiwa wachangiaji wakubwa walitoa fedha zao za kigeni nyingi kuliko Tanganyika lakini leo BOT inafanywa kama ni zao la Tanganyika pekee.,

Ndio mana Lukuvi alisema waziwazi Tanganyika haitaweza kuicha na kuikalia kimabavu zanzibar sababu ni ile ile tu ndio inayokupeni maendeleo yenu huko na hizo fly over zote mnapata hela kutoka Zanzibar.,

Watanganyika walioko zanzibar hawazalishi mali yoyote wanauza dawa za panya, viroboto na kulima viazi vitamu tu hawana kodi wanayolipa mahali popote., Wazanzibari wamewafadhili majumba ya kukaa bila ya kulipa kodi, wanaishi bure na kila leo wanapigiana simu wanaendelea kuja kuishi zanzibar na familia zao.

Sasa unapokuja na hoja kuhusu Zanzibar tambua ndio wanakufanya wewe leo uwe na kiburi kiasi hicho, hamna shukurani.
We mdada hebu kalale, naona unatokka povu sana, usijeharibu swaum yako!
 
Ila kama Serikali haina mpango wa kuadhimisha Sherehe za Muungano, kwanini wanatenga bajeti yake kila mwaka?

Kwanini fedha hizo in a first place zisipangiwe shughuli za maendeleo badala ya kuja kuzibadilishia gia angani ilhali kuna vifungu vingi tu vya muhimu vinakosa bajeti katika wakati wa kupanga.
Ndiyo taabu ya siasa mkuu, hapo kuna wajumbe walikaa kumshauri mama na walilipwa posho na ni posho nene
 
Sasa mnashindwa nini!! Miaka yote hii tunawalea tu! Ni watoto gani nyinyi msio kua? Yaani huwa inanikera sana niwaonapo wabunge wa Zanzibar kwenye bunge letu la Tanganyika wakitafuna kodi zetu kinyume kabisa cha utaratibu!
Weka utaratibu wako wewe basi tuufate maana huo ulikuwepo ndio ushauwona sio ati ni kinyume na utaratibu ...btw umetokea wapi unaonekana kama sio Mtanzania.
 
Asante sana Mkuu kwa ufafanuzi wako ufafanuzi wako kupitia mabandiko yako mawili. Nimeyasoma kwa makini sana. Na nikayarudia kuyasoma zaidi ya mara nne. Kisa cha haya ni mkanganyiko huu ulioueleza.
===
Nje ya Muungano, Kimataifa set up ya muungano wetu union, Tanzania ni taifa moja tuu la URT, or JMT chini ya rais mmoja, rais wa JMT, na chini ya serikali moja, serikali ya JMT. Hili ndilo taifa linalotambulika kimataifa, ndilo linalokopeswa na lenye uwezo wa kukopa na ndilo linalopokea misaada yote ya kimataifa.

Ndani ya Muungano Kitaifa, set up ya muungano wetu ni muungano wa federation, ni muungano wa nchi mbili, zenye maeneo mawili tofauti, yaani territories mbili za Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, au Tanzania Zanzibar, zenye serikali mbili ya JMT na SMZ, zenye marais wawili, rais wa JMT na rais wa SMZ wenye hadhi sawa, ndio maana Rais Samia kwenye protocol ya Muungano, anaanza na kumtaja kwanza rais wa Zanzibar, ndipo anakuja kwa makamo wa rais wa JMT.

Katiba hiyo ya Zanzibar, katiba ya JMT haitambui, hivyo ni ama katiba ya JMT iitambue katiba ya Zanzibar, au Katiba ya Zanzibar Ibadilishwe iendane na Katiba ya JMT.
=====
Sasa baada ya kutulia nikaanza kujiuliza haya:
1. Rais wa jamhuri wa Tanzania anapaswa kutumia katiba ipi kuongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(JMT) kati ya katiba JMT na ile ya katiba ya Zanzibar?

2. Je. Rais wa JMT ameapa kuilinda katiba ya JMT au katiba ya Zanzibar au kuzilinda katiba zote?

3. Kama jibu la swali namba 2. ni kulinda katiba zote; je, hili linawezekana wakati kuna mkanganyiko wa kile kinachoelezwa kwenye katiba hizi mbili juu ya tafsiri ya JMT?

3. Kama majibu ya maswali namba 1. na 2. ni anatumia katiba ya JMT na ali'h'apa kuilinda katiba JMT ni kwa namna gani Makamu wa Rais wa JMT au chukuliwe kuwa yupo chini ya Rais wa Zanzibar tena kwa misingi ya mnasema ya 'kiplotokali'?

4. Kwenye maelezo yako kuna sehemu umesema watanzani waliozaliwa ama wenye haki ya kuitwa wazanzibari wana haki mbili za kiraia, moja haki ya uraia wa Zanzibar (ambayo umesisitiza ndiyo hasa inapaswa kutambulika kwanza) na uraia wa Tanzania. Lakini Watanzania waliozaliwa ama wenye haki ya kuitwa iliyokuwa Tanganyika yaani watanganyika wao wana haki moja ya kiraia. Yaani wao ni Watanzinia tu, hivyo mambo ya uzanzibari wayasike redioni na kwenye 'l'uninga tu!.

Sasa, Mkuu; je, unaniruhusu nipinge mfano wako wa kusema Tanzania ndiye anamlisha Zanzibar kama mke (hili neno lina ukakasi) kwa kutumia mfano unaoelekea kuwa halisia kuwa Eneo la iliyokuwa Tanganyika kwa sasa ndilo koloni la Zanzibar kwa kuzingatia faida nyingi wazipatazo watanzania wenye kujitambulisha wazanzibari kutoka JMT kwa kuzingatia maelezo ya Mkuu(Mwalimu wangu) Nguruvi3, achilia mbali wao kuwa na uraia wa "nchi mbili", jambo linalokatazwa na katiba ya JMT? Ndiyo wana uraia wa nchi mbili uraia wa Zanzibar na uraia wa JMT.

5....
Maswali yako mengi, ila Mkuu Pascal, ama yeyote naomba anisaidie majibu haya kwanza.
 
Labda niulize kuwa pesa za gharama za Muungano huwa zinatoka wapi au kwa utaratibu gani.

Pili, je Zanzibar kuna pesa ambayo wanachangia kwenye Muungano kusema sasa warudishiwe sehemu?

Kinyume na hapo Tanganyika haipaswi iendelee kuifadhili Zanzibar. Otherwise tuambiwe kuwa nao Zanzibar kuna pesa huwa wanachangia huku kwetu.

Mh Rais asitake sasa kuwa nyonya wabara kwa jasho lao kupafaidisha kwao. Haya ndo madhara ya kuwa na Rais kutoka Zanzibar. Kama kuna sehemu anaona Zanzibar wananyonywa aseme wazi na hiyo mianya izibwe.

Lakini siyo sisi huku tupigike halafu jamaa wawe wanakula tende na urojo tu mwisho wa siku wapate pesa zetu.
💪
 
Back
Top Bottom