mshale21
JF-Expert Member
- Apr 8, 2021
- 2,050
- 4,903
Dodoma!
Akizungumza Leo katika kongamano la Muungano jijini Dodoma, Makamu wa Raisi Dr . Philip Mpango amesema Raisi Samia Suluhu Hassan ameelekeza Fedha zilizotakiwa kutumika katika shughuli za maadhimisho ya miaka 57 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zigawanywe pande hizo mbili (Tanganyika na Zanzibar) ili zikafanye shughuli za maendeleo!
Dk. Philip Mpango ametumia takribani dakika 20 kuhutubia wanakongamano na Kisha kuondoka ili aendelee na shughuli zake za Kila siku za kulijenga taifa!
TAREHE 26 Aprili, 1964 Mataifa mawili haya ya Jamuhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar yalioungana na kuunda Taifa jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo badae ikabadilishwa na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hivyo kila mwaka ifikapo Aprili 26, tunakumbuka siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ambapo mwaka huu Muungano huu unatimiza miaka 57, huku ukiwa ni Muungano wa mfano na imara katika Bara la Afrika na ulimwenguni pote.