Mzee Mwinyi ndiye kiongozi pekee aliyewahi kuongoza Tanzania nzima, sio upande mmoja kwa Koti la Muungano

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,503
51,098
Katika dunia hii kuna watu wamebarikiwa sana. Na mamlaka hutoka kwa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu akiamua kukupa mamlaka, kipaji, riziki anakupa tu kwa kupenda yeye mwenyewe bila kujali wewe una nini.

Mzee Mwinyi hakuwa msomi sana kwa viwango vya kisasa (kuwa na digrii), lakini ni dhahiri kwa nyakati zake miaka ya 1950's kabla ya uhuru, mtu kuwa na Diploma basi wewe ulikuwa unahesabika ni msomi haswa maana hata waliokuwa na digrii ndani ya Tanganyika na Zanzibar walikuwa wachache sana.

Katika historia ya nchi zetu mbili, kabla ya mzee Mwinyi hajashika urais Ukiondoa Malkia wa Uingereza aliyeendelea kuwa mkuu wa nchi ya Tanganyika kwa mwaka mmoja kabla hatujawa Jamhuri, tumewahi kuwa na viongozi wakuu wa nchi watano. Yes wakuu wa nchi wa watano na siyo wawili (Nyerere na Karume) kama ilivyozoeleka.

Upande wa Tanganyika
1. Nyerere (kama waziri mkuu wa Tanganyika na baadae Rais wa Tanganyika, then wa muungano)
2.Kawawa kama Waziri mkuu wa Tanganyika (wakati huo Nyerere kajiuzulu uwaziri mkuu)

Upande wa Zanzibar
1. Sultan (naye ni mzanzibari maana alizaliwa Zanzibar)
2. Karume
3. Jumbe

Katika wote hao, hakuna aliyepata kuitawala Tanzania kwa ukamilifu wake. Nyerere alikuwa ni raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini hakuwa na mamlaka ya MAMBO YASIYO YA MUUNGANO kwa upande wa Zanzibar. Ni kweli alikuwa na ushawishi mkubwa kwenye siasa za Zanzibar, lakini hakuwa na powers za kutosha kwenye mambo yasiyo ya Muungano. Hata hivyo aliweza kuongoza Tanganyika iliyovaa koti la Muungano. Yaani aliitumia serikali ya Muungano iifanyie kazi Tanganyika na hivyo kupelekea Wazanzibar kuhoji hata huo muungano wenyewe tangu miaka ya mzee Jumbe.

Lakini tukija kwa Mzee Mwinyi. Yeye ameongoza serikali ya Zanzibar na kisha akaongoza serikali ya Muungano, na hii kumfanya kuwa mtu wa pekee Kuongoza Tanzania nzima katika mambo yote ya Muungano na yasiyo ya Muungano katika pande mbili hizi za nchi katika kipindi cha nyakati tofautitofauti.

Mwinyi amewahi kuwa kamanda mkuu wa vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (Nyerere) hajawahi na Pia Mwinyi amewahi kuwa amiri jeshi mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania (kama maraisi wengine).

Kwa hiyo, Ukiuliza nani amewahi kuwa MTU MWENYE POWER NYINGI ZAIDI katika Tanzania nzima (Tanganyika na Zanzibar), basi ni mzee Mwinyi na wala si Nyerere. Japo Nyerere alikuwa na ushawishi mkubwa zaidi katika masuala ya siasa za Tanzania.

Wakatabahu!
 
Sidhani kama unachokiandika tunaweza tafsri hivyo. Tunataka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awe na mamlaka kamili Kwa wakati mmoja Kwa mambo yote ya Muungano na yasiyo ya Muungano Kwa nchi nzima Kwa wakati mmoja. Mwinyi alipokuwa rais Tanzania alitawala Tanganyika tu hakuwa na mamlaka yoyote upande wa Zanzibar. Alikuwa na nafasi nzuri kuididimiza Tanganyika Kwa sababu siyo mtanganyika.
 
Back
Top Bottom