Rais Samia: Dunia kwa sasa inakabiliwa na tatizo jipya la Usalama (Ugaidi)

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Rais Samia amesema Dunia kwa sasa inakabiliwa na tatizo jipya la Usalama (Ugaidi). Ameeleza hayo katika Ufunguzi wa Kikao cha Mkuu wa Majeshi kinachofanyika Ngome ya Lugalo

Ameeleza, "Kwa hulka ya Ugaidi, Mtu yeyote bila kujali Rangi, Dini, Umri, Itikadi, Kipato au Uraia anaweza kuwa mhanga wa Ugaidi. Mifano ipo nanyi mnaijua"

Rais ameongeza kuwa, "Mapambano dhidi ya tishio la Ugaidi si suala la Vyombo vya Ulinzi na Usalama peke yenu, bali linahitaji ushirikiano kutoka Taasisi mbalimbali ikiwemo Vyombo vya Habari na Asasi za Kiraia"

photo_2021-11-15_12-52-46.jpg
 
Haya wale wapiga Zumari wasema hili nalo kapitiwa! Huyu sio Mwislam ila kajificha kwenye kivuli cha Uislam. Ninavyowajua Waislam ni wapenda haki sana and I admire hii spirit yao ila hawa akina Mahita na Kingai na Hang'hire
 
Kwani Samia ndio Mahakama au hakimu? Unalinganishaje Uislam wa Samia na Kesi ya Mbowe ambayo huyo unayemlalamikia hana mamlaka nayo?
 
Mboe na Genge lake la Kihalifu wamesha pata salamu.
Mnyika anapaswa awakataze viongozi wenzake na wana chama wake baadhi wenye tabia za kigaidi waache tabia za kihalifu kama vile;
kuiombea mambo mabaya nchi, kuvurunga amani, kuto kutii sheria, ujambazi, uzaji madawa, kupanga njama za kuwauwa viongozi wa serikali au kufurahia vifo vyao n.k waache.
 
Rais Samia amesema Dunia kwa sasa inakabiliwa na tatizo jipya la Usalama (Ugaidi). Ameeleza hayo katika Ufunguzi wa Kikao cha Mkuu wa Majeshi kinachofanyika Ngome ya Lugalo

Ameeleza, "Kwa hulka ya Ugaidi, Mtu yeyote bila kujali Rangi, Dini, Umri, Itikadi, Kipato au Uraia anaweza kuwa mhanga wa Ugaidi. Mifano ipo nanyi mnaijua"

Rais ameongeza kuwa, "Mapambano dhidi ya tishio la Ugaidi si suala la Vyombo vya Ulinzi na Usalama peke yenu, bali linahitaji ushirikiano kutoka Taasisi mbalimbali ikiwemo Vyombo vya Habari na Asasi za Kiraia"

View attachment 2011253
Kumbe maisha bila hijabu yanawezekana. Hongera sana Madam President kwa muonekano wa vazi la kijeshi.
 
Back
Top Bottom