Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
Kufuatia mualiko wa kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani na nchi ya Vatican Papa Francis, Rais Samia Hassan atafanya ziara ya kitaifa tarehe 11 hadi 12 Februari, 2024.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amesema lengo la ziara hii ni kukuza ushirikiano kati ya Tanzania na Vatican.

Tanzania na Vatican tangu mwaka wa 1960 zimekuwa zikishirikiana katika masuala ya elimu, afya, masuala ya amani na kiroho.

"Kanisa katoliki linakadiriwa kumiliki zaidi ya shule za chekechea 240, shule za msingi 147, shule za sekondari 245, vyuo vya ufundi 110, na vyuo vikuu 5," inaeleza taarifa iliyotolewa na wizara huku takribani taasisi za afya 473 zikiendeshwa na kanisa katoliki.

Tofauti za udini hazijawafanya viongozi hawa kushindwa kukaa pamoja na kujadili maslahi ya wananchi na uendelezaji wa ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.

=====

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Francis amemualika Rais Samia Suluhu Hassan Mjini Vatican kwa mazungumzo rasmi ya siku mbili baina ya viongozi hao.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amewaambia waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam leo kuwa mazungumzo hayo yatafanyika Februari 11 na 12 Vatican nchini Italia.

Makamba amesema kufuatia mwaliko huo, Rais Samia ameamua kuambatana na waumini wa kawaida wa Katoliki ambao pia wataonana na Papa Francis katika ziara hiyo ya kihistoria.

"Hii ni heshima kubwa kwa nchi yetu na Rais wetu, kwani mazungumzo hayo na Baba Mtakatifu ni ya heshima kubwa na watu wachache sana ndio watapata fursa ya kuhudhuria mazungumzo hayo," amesema Makamba

===
Kujua safari nyingine za Rais Samia, Soma: Safari/Ziara za nje ya Nchi za Rais Samia Suluhu tangu awe Rais wa Tanzania 19 Machi, 2021
 
Kufuatia mualiko wa kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani na nchi ya Vatican Papa Francis, Rais Samia Hassan atafanya ziara ya kitaifa tarehe 11 hadi 12 Februari, 2024.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amesema lengo la ziara hii ni kukuza ushirikiano kati ya Tanzania na Vatican.

Tanzania na Vatican tangu mwaka wa 1960 zimekuwa zikishirikiana katika masuala ya elimu, afya, masuala ya amani na kiroho.

"Kanisa katoliki linakadiriwa kumiliki zaidi ya shule za chekechea 240, shule za msingi 147, shule za sekondari 245, vyuo vya ufundi 110, na vyuo vikuu 5," inaeleza taarifa iliyotolewa na wizara huku takribani taasisi za afya 473 zikiendeshwa na kanisa katoliki.

Tofauti za udini hazijawafanya viongozi hawa kushindwa kukaa pamoja na kujadili maslahi ya wananchi na uendelezaji wa ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.

Source - JamboTv
Kaalikwa na bosi wa maraisi wote duniani
 
Labda papa francis wa chad
 
Uongozi wa kikatoliki duniani umemualika rais wa Tanzania mama Samia kuitembelea Vatican.

Hii itakuwa ni somo murua kabisa kwa ndugu zetu hasa wa hapa jf ambao wanaeneza udini na chuki na uhasama wa uislam na ukristo.

Vatican imemualika rais Samia ambaye ni muislam tena muumini kweli kweli.

Hili ni fundisho kwa watanzania kuwa tisiwe na maneno mengi bila ya kuchunguza na kukitidhisha.

Mungu ameshinda vita kati ya wanao kusudia kuharibu amani ya nchi yetu kupitia kueneza chuki za KIDINI.

Mungu ibariki Tanzania.
1705851226868.jpg
 
IMG_9688.jpeg

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajia kufanya ziara ya kitaifa Vatican kuanzia February 11 – 12, 2024 kufuatia mwaliko wa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Francis.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba akiongea leo Dar es salaam amesema dhumuni la ziara hii ni kuimarisha ushirikiano wa uwili kati ya Tanzania na Vatican “Itakumbukwa mwaka 2016 Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, alimwalika Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, yaani Baba Mtakatifu Francis kutembelea Tanzania hata hivyo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kiafya ziara hiyo haikuwezekana na badala yake kwa wakati huu, Rais Samia amealikwa na Kiongozi huyo kufanya ziara Vatican”

“Akiwa Vatican Rais atakutana kwa mazungumzo na Baba Mtakatifu Francis pamoja na Katibu wa Vatican, Pietro Parolin lakini kabla ya ziara ya Vatican Rais pia atafanya ziara ya Kitaifa nchini Indonesia kuanzia January 24 – 26 kufuatia mwaliko wa Joko Widodo, Rais wa Jamhuri ya Indonesia, ziara hii ya Kitaifa inafuatia ziara ya Kitaifa ya Rais Joko Widodo aliyoifanya Tanzania mwezi Agosti 2023” ——— Waziri Makamba.

Rais Samia pia atafanya ziara ya Kitaifa nchini Norway, February 13-14, 2024, kufuatia mwaliko kutoka kwa Mfalme Herald wa Norway na Malkia Sonja ikiwa ni miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Nchi hiyo.
 
Uongozi wa kikatoliki duniani umemualika rais wa Tanzania mama Samia kuitembelea Vatican.

Hii itakuwa ni somo murua kabisa kwa ndugu zetu hasa wa hapa jf ambao wanaeneza udini na chuki na uhasama wa uislam na ukristo.

Vatican imemualika rais Samia ambaye ni muislam tena muumini kweli kweli.

Hili ni fundisho kwa watanzania kuwa tisiwe na maneno mengi bila ya kuchunguza na kukitidhisha.

Mungu ameshinda vita kati ya wanao kusudia kuharibu amani ya nchi yetu kupitia kueneza chuki za KIDINI.

Mungu ibariki Tanzania.View attachment 2878752

Amemualika kama Muislamu au kama Rais wa Tanzania?
 
Tutege Mee heshima na kuheshimika nawatu fake wenye lengo la kutunyonyanya na kuya futa maadiri yetu watu weusi

Kwakifupi rabda niseme tutegemee kuwa heshimu na kuzifuata amri za watu wenye Nia mbaya na kizazi chetu/dunia yetu

Nimalizie kwa kusema Tuombe mungu amuongezee busara raisi wetu machaguo yake yasiwe ya kibinafsi,yakibinadamu, na yaki raisi zaidi Bari yawe ya kiutu, kimira,kidesturi, na yanayo zingatia maisha endelevu yakibinadamu kinyume na hapo tuta vuna aibu kubwa sana
 
Kufuatia mualiko wa kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani na nchi ya Vatican Papa Francis, Rais Samia Hassan atafanya ziara ya kitaifa tarehe 11 hadi 12 Februari, 2024.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amesema lengo la ziara hii ni kukuza ushirikiano kati ya Tanzania na Vatican.

Tanzania na Vatican tangu mwaka wa 1960 zimekuwa zikishirikiana katika masuala ya elimu, afya, masuala ya amani na kiroho.

"Kanisa katoliki linakadiriwa kumiliki zaidi ya shule za chekechea 240, shule za msingi 147, shule za sekondari 245, vyuo vya ufundi 110, na vyuo vikuu 5," inaeleza taarifa iliyotolewa na wizara huku takribani taasisi za afya 473 zikiendeshwa na kanisa katoliki.

Tofauti za udini hazijawafanya viongozi hawa kushindwa kukaa pamoja na kujadili maslahi ya wananchi na uendelezaji wa ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.

=====

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Matakatifu Francis amemualika Rais Samia Suluhu Hassan Mjini Vatican kwa mazungumzo rasmi ya siku mbili baina ya viongozi hao.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amewaambia waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam leo kuwa mazungumzo hayo yatafanyika Februari 11 na 12 Vatican nchini Italia.

Makamba amesema kufuatia mwaliko huo, Rais Samia ameamua kuambatana na waumini wa kawaida wa Katoliki ambao pia wataonana na Papa Francis katika ziara hiyo ya kihistoria.

"Hii ni heshima kubwa kwa nchi yetu na Rais wetu, kwani mazungumzo hayo na Baba Mtakatifu ni ya heshima kubwa na watu wachache sana ndio watapata fursa ya kuhudhuria mazungumzo hayo," amesema Makamba
Amealikwa au amejialika ,tuwekane sawa hapa , kama vipi leta ushahidi wa mwaliko , why mnachukulia watz wapumbavu sana nchi hii, kumbuka

Kikwete alijialika
Mkapa alijialika n.k ,so kipi cha msingi sana Papa amwalike ,Tueshimiane mtoa mada hauijui Dunia
 
TUNA PASWA KUJIULIZA MASWALI HAYA

Kwanza
hongera kwa tz,

Pili nikwanini Tanzania?

Tatu

tujitafakari tunaishi maisha gani je! nimaisha ya kujifrahisha au kuwa frahisha wengine?

Dunia Haina kitu Cha bure hivyo tuende tukijua si bure Bari ni kwasababu na hiyo sababu ni ipi?

Tusije ruhusu Yale yasiyo takiwa yakawa ya mhimu kuya fanya huku tukiwa tunajiangamiza wenyewe 🙏🙏
 
Back
Top Bottom