Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942
📍 Jimbo la Ushetu: Wananchi wa Ukune, Ushetu Wampongeza Rais Samia Suluhu Hassan

🏥🚑🤰🏽🧑🏽‍🍼

▪️Wananchi wa Ukune,Ushetu Wampongeza Rais Samia Suluhu Hassan

▪️Mbunge wa Ushetu Mhe. Emmanuel Cherehani azidi kukonga nyoyo wananchi wa Ushetu

Wananchi wa Kata ya Ukune katika Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga, wameishukuru Serikali pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia gari jipya la kubebea wagonjwa(Ambulance).

Akizungumza kwa niaba ya wananchi hao mara baada ya kukabidhiwa gari hilo, Fabiani James na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wilaya ya Kahama Theresphora Saria wamesema gari hilo litasaidia kupunguza vifo vya wajawazito na watoto na kwamba awali walikuwa wanalazimika kutumia usafiri wa pikipiki kuwasafirisha wagonjwa kwenda kwenye hospitali wilayani Kahama

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Ukune Dr. Elikana Lubango, amesema gari hilo litatumika kubeba wagonjwa wakati wote litakapohitajika.

Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani akisema Serikali imetoa magari hayo ukiwa ni mpango wa kuwaondolea Wananchi adha ya kuwasafirisha wagonjwa kwenda kupata matibabu kwenye Hospitali kubwa.

GAFPdtLXwAAyCG3.jpg
GAFPdtKWgAARq9l.jpg
GAFPdtNWoAAXorX.jpg
GAFPe9sWUAAWJSH.jpg
 
Back
Top Bottom