BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,416
- 8,202
Rais Samia Suluhu Hassan amevunja Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ikiwa ni baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wake, Meja Jenerali Paul Kisesa kuteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uganda.
Kufuatia uamuzi huo, Rais amemteua Dkt. Rhimo Simeon Nyasabo kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo. Dkt. Nyasabo ni Mkurugenzi wa Maendeleao ya Biashara wa Benki ya Azania.
Uteuzi huu unaanza mara moja.