Rais Samia ateua Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Bodi za TMA, Mkonge na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,111
12,574
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Bodi kama ifuatavyo:

i) Amemteua Jaji Mshibe Ali Bakari kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (Tanzania Meteorological Authority - TMA) na amemteua Dkt. Emmanuel Jonathan Mpeta kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo.

ії) Amemteua Balozi Adadi Mohamed Rajab kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa binafsi na amemteua Bi. Fatma Mohamed Ali kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo.

iii) Amemteua Bw. Theobald Maingu Sabi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mkonge, Tanzania.

Uteuzi huu umeanza tarehe 10 Desemba, 2023.
IMG_9329.jpeg
 
Back
Top Bottom