Rais Samia atoa msamaha kwa wafungwa 1,036

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,480
Reaction score
14,825
Katika kuadhimisha Miaka 64 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo Desemba 9, 2025 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa msamaha kwa wafungwa elfu moja na thelathini na sita (1,036)

Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. George Simbachawene imeeleza kuwa wafungwa ishirini na mbili (22) kati y ao

wameachiliwa huru leo tarehe 09 Disemba, 2025 na wafungwa elfu moja na kumi na nne (1,014) wamepunguziwa adhabu zao na watabaki gerezani na kuendelea kutumikia sehemu ya vifungo vilivyobaki.

"Ni matarajio ya Serikali kuwa wafungwa walioachiliwa huru leo tarehe 09 Disemba, 2025 watarejea tena katika jamii kushirikiana na wananchi wenzao katika ujenzi wa Taifa letu na kwamba watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani." - Waziri Simbachawene

1765260709819.jpeg

1765260723571.jpeg

1765260738357.jpeg

1765260753272.jpeg
 
View attachment 3513334
View attachment 3513335
View attachment 3513336
View attachment 3513337
Pongezi kwako mama Samia
 
cha maana akomeshe utekaji ukamataji wa watu holela na askari kanzu.wasiojulikana wakomeshwe na wachukuliwe hatua
 
Ndugu zangu Watanzania,

Tuwe tunaeleweka vyema na vizuri sana tunaposema kuwa Rais Samia ni Mama na kiongozi Mwenye moyo wa Huruma na Upendo mkubwa kwa watu wote bila ubaguzi na kumbagua mtu yeyote yule.

Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan kwa kutambua kuwa binadamu wote hukosea na kwamba hakuna aliyekamilika chini ya jua. Ameweza katika siku ya leo kwa moyo wa upendo na huruma kubwa sana kutoa msamaha pamoja na kuwapunguzia Adhabu Wafungwa takribani 1036.

Ambapo Rais wetu Mpendwa amewapa tabasamu na furaha mamia ya wafungwa hao katika siku hii Adhimu na ya kipekee kabisa kwa Taifa letu. Ambayo ni kumbukumbu ya Uhuru wa Taifa letu tulipojinasua kutoka katika makucha ya wakoloni na ukoloni.

Hii ni katika kutambua ya kuwa binadamu hujifunza kutokana na makosa na kwamba kupitia vifungo vyao walivyo vitumikia katika muda waliokuwa magerezani. watakuwa wamejifunza na kuwa Raia wema na wa mfano na kuigwa kitabia pale watakapokuwa wakirejea mitaani na kuungana na Familia zao.

Kwa hakika Rais Samia anastahili pongezi kubwa sana na kuendelea kuungwa mkono na watanzania wote kwa nguvu zetu zote. Tusikubali kuchonganishwa na Rais wetu Mpendwa pamoja na serikali yetu. Mama ana dhamira njema na Taifa letu na ndio maana amekuwa akifanya kazi usiku na mchana kwa ajili yetu watanzania. Tuendelee kumuombea afya njema na nguvu za kuendelea kututumikia watanzania..

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Mbona viongozi uchwara na machawa wao huwa ni empty set hivi?.

Yaani unaua, una tesa, una teka, halafu una kazana kusema nawasamehe mf.
 
Back
Top Bottom