Lugano5

R I P
Jul 15, 2010
4,520
755
TAMISEMI yatangaza ajira 21000 afya na elimu 2023

======

Screenshot 2023-04-12 at 09-59-02 OFISI YA RAIS TAMISEMI (@ortamisemi) Instagram.png

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia ajira mpya 13,130 za kada ya Ualimu watakaofundisha katika Shule za Msingi na Sekondari.

Aidha, idadi ya watumishi watakoajiliwa katika kada za Afya ni 8,070 ambao watafanya kazi katika Hospitali za Halmashauri, Vituo vya Afya na Zahanati za Serikali.

Takwimu za Tume ya Utumishi wa Walimu zinaonesha Tanzania ina Walimu 87,992 wa Sekondari na 173,591 wa Shule za Msingi huku mahitaji halisi yakiwa ni Walimu 237,502 wanaotakiwa kufundisha kwa uwiano wa Mwalimu 1 awe na Wafunzi 45.

Waombaji ni wahitimu wa nafasi hizo kuanzia mwaka 2015 hadi 2022 ambao watakuwa na sifa stahiki na wasiozidi umri wa miaka 45 lakini wanaofanya kazi za kujitolewa wameitwa kuomba nafasi hizo bila kusema kama watapewa kipaumbele.

“Rais ametoa kibali cha kuajiri watumishi hao nasi tunaanza mchakato huo mara moja kuanzia leo, wanaoajiriwa ni kuanzia ngazi ya cheti hadi Shahada kulingana na kada anayoiomba mhusika,” amesema Kairuki.

Hata hivyo ameonya waombaji watakaodanganya sifa zao katika maombi ikiwemo wenye ulemavu ambao wametengewa nafasi na watakaogushi umri kwani Serikali inachukua watumishi wasiozidi miaka 45.

Amesema waombaji wote wataomba kupitia mtandao wa Tamisemi na waliokuwa wameomba siku nyingi wametakiwa kuhuisha taarifa huku akitoa katazo la waombaji ambao watatuma maombi yao kwa njia ya barua au posta kwamba hayatapokelewa.
1681303818176.png

1681303841058.png

1681303861392.png

1681303896439.png

1681303923835.png

1681303957380.png

1681303978456.png

1681304002190.png

1681304026536.png

1681304051096.png

TAMISEMI
 
Back
Top Bottom