Rais Magufuli: Nitaondoka madarakani kwa mujibu wa Kanuni na Katiba ya CCM na Katiba Nchi

Beira Boy

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2016
Messages
17,353
Points
2,000

Beira Boy

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2016
17,353 2,000
Aman iwe nanyi wakuu

Rais Magufuli amedai kuwa licha ya mashinikizo mengi kutoka kila pande lakini yeye ataondoka madarakani kwa mujibu wa katiba ya CCM na nchi wala hataongeza miaka maana kazi ya Urais ni ngumu sana.

Amedai kuna watanzania wengi tu ndani ya CCM wenye kuweza kuongoza nchi hivyo yeye atapisha atakapomaliza mda wake.

LONDON BOY
----

Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema kazi ya urais ni ngumu na ataondoka madarakani baada ya muda wake wa uongozi kumalizika.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Ijumaa Desemba 13, 2019 wakati akiongoza mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM uliofanyika jijini Mwanza.

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole imesema, “licha ya hamasa kubwa waliyokuwa nayo wajumbe wa halmashauri kuu kutokana na kazi nzuri ya Serikali ya CCM, Magufuli amesisitiza kazi ya urais ni ngumu sana na yeye ataheshimu utamaduni na desturi za CCM, kanuni, katiba ya CCM na Katiba ya nchi na kwamba CCM ni kiwanda cha kuzalisha viongozi na kwa utaratibu ambao chama kimejiwekea kitampata mtu bora zaidi atakayepokea uongozi baada yake.”

Rais Magufuli aliyeingia madarakani Novemba 5 mwaka 2015 ngwe ya kwanza ya miaka mitano itamalizika mwaka 2020 na ya pili ataihitimisha mwaka 2025 iwapo atachaguliwa tena katika uchaguzi mkuu 2020.

Msimamo huo wa Rais Magufuli ameutoa ikiwa ni siku moja imepita tangu Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Mizengo Pinda kueleza matamanio yake kuona Rais Magufuli anaongezewa miaka mingine mitano baada ya kumaliza muda wake wa uongozi wa miaka 10.

Pinda aliyekuwa Waziri mkuu Mwaka 2008 hadi 2015 alitoa kauli hiyo jana Alhamisi Desemba 12, 2019 katika ufunguzi wa semina ya wajumbe wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM unaofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu (BoT) jijini Mwanza.

Aprili 3, 2019 Rais Magufuli alisema muda wake wa uongozi ukiisha ataondoka madarakani tarehe hiyohiyo kwa kuwa yeye sio rais wa maisha. Alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Newala akiwa katika siku ya pili ya ziara yake mkoani Mtwara.

“Mimi napata matumaini makubwa sana kwamba miaka hii kumi uliyopewa itatupeleka pazuri sana, ni kwa kuwa tu katiba zenyewe kidogo ziko tight lakini kama si kwa sababu hiyo Wallah ningesema mzee piga mingine tena ongeza kama mitano tu.”

“Sasa najua hata mkijaribu kumlazimisha atawakatalia tu, lakini nataka niseme kwa namna ninavyoguswa na kazi kubwa unayoifanya,” alisema Pinda.
 

ROBERTO 20

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2017
Messages
5,231
Points
2,000

ROBERTO 20

JF-Expert Member
Joined Jul 25, 2017
5,231 2,000
"Aondoke hata kesho nimeshamchoka mimi maana ni muongo kweli anachosema sicho anachomanisha"

Urais mgumu kwani nani alimpeleka kwa nguvu kuchukua form?

Urais ungekuwa mgumu si angeacha kubana wapinzani wake wakina Lissu ili na wao wapate nafasi ya kuongoza?
Lissu atawaongoza watu kama wewe.
 

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Messages
12,901
Points
2,000

britanicca

JF-Expert Member
Joined May 20, 2015
12,901 2,000
Harufu harufu harufu
Ikinuswa harufu ya viatu wajanja tunaita (Kamnyama) ujue kuna mtu anawi vema miguu na hajavaa soksi kavua Viatu

Ukisikia harufu ya Kinga zikizotumika jua uko karibu na danguro au nyumba ya kihuni ya Kulala wageni

Ukisikia harufu ya boxer chafu ujue anayeivaa haogi vizuri uenda anaishi maeneo ya Fangasi, au ana mkono wa sweta kabisa,

NANUSA harufu Fulani ya Kutawaliwa kidikteta rasmi mwaka 2026,

Tutakuwa na Makundi ya kiharakati yatakayo ongezewa Jukumu la kupigania Ukomo wa Urais baada ya Kuvurugwa

Muda mfupi Mtu aliyepinda na Mizengwe yake alisahau kwamba aliwai kuwa Na nafasi kubwa anaongea suala la Rais kuongezewa Muda kweli?

Hajui kina Jingalao, kina Kibajaji watachukuliaje Hilo suala, Kina Nkamia kuanza kumuyumbisha mgogo wa Mpwapwa kurubuni vichwa Maji wa CCM kubadili katiba

Tunajiandaa akipitisha hata siku mbili, tuna haki ya Kufanya lolote

Britannica
 

NJOLO

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2017
Messages
444
Points
500

NJOLO

JF-Expert Member
Joined Mar 6, 2017
444 500
Kwa sisi Wakristo, tungetamani Yesu Kristo Abaki Duniani hadi leo tukiendelea kuishi naye.

Aliinjilisha kwa miaka mitatu na akaondoka kwenda kwa Baba Mbinguni (hii ni imani yetu na haitakiwi kuhojiwa au kuthibitishwa).

Kutawala kwa muda mfupi na ukaondoka wakati bado watu wanakuhitaji ni jambo la busara na hekima.

Rais wetu kama alivyosema kazi ya Urais ni ngumu sana kwa sababu pengine anaongoza watu wengi ambao hawana maadili na hawatii sharia bila shuruti.

Ni vyema amalize muda wake wa kikatiba akiwa na afya njema kuliko kuendelea kufanya kazi ngumu kwa muda mrefu kitu ambacho kinaweza kumletea madhara makubwa kiafya.
 

Glenn

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2018
Messages
7,135
Points
2,000

Glenn

JF-Expert Member
Joined May 22, 2018
7,135 2,000

Forum statistics

Threads 1,379,239
Members 525,346
Posts 33,739,276
Top