Wana CCM wanasubiria Rais Samia aondoke madarakani wamseme kwa mabaya

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,547
41,060
CCM kwa bahati mbaya sana imejaa watu wanafiki. Watu ambao kwao kilicho muhimu ni kuwa na madaraka. Ndiyo maana huwezi kumsikia kiongozi wa CCM au Serikali akiikosoa CCM au Serikali au Rais, wakati Serikali hiyo au Rais huyo akiwa madarakani. Rais akiwa madarakani, wakati wote ni kumsifu kwa kila sifa kama vile hakuna Rais mzuri popote Duniani wa kufikia kiwango cha Rais wa Tanzania. Akiondoka madarakani ndiyo sasa ubaya na mapungufu yake yataanza kusemwa na wale wale waliokuwa wakimsifia.

Hayati Magufuli akiwa Waziri wa Ujenzi, kila mara alimsifia Kikwete. Kikwete alipoondoka madarakani, mara kadhaa indirectly au directly alimsema Kimwete na uongozi wake kuwa ulijaa ufisadi na upendeleo wa ajabu. Hayati hakuwahi kuyanena hayo, Kikwete akiwa madarakani. Lakini wapo watu wakweli wa nafsi waliusema utawala wa Kikwete ulivyokuwa umebobea kwenye ufisadi, Kikwete akiwa madarakani, ila walipuuzwa na wanaCCM.

Hayati Magufuli alipokuwa madarakani, kila kiongozi wa chama na Serikali alimpa sifa Hayati Magufuli za kila aina kiasi cha kutaka kuwaaminisha watu kuwa Magufuli ndiye alikuwa Rais bora kabisa Duniani. Baada ya kufariki, ubaya wa aina mbalimbali wa uongozi wa Magufuli, unasemwa mpaka leo, kuanzia kwenye udikteta, kudhulumu mali za watu, kuwabambikia watu kesi, kuwanyang'anya watu pesa zao, n.k. Sahizi utawala wa Magufuli, ambao watu wakweli waliusema akiwa hai kuwa ulikuwa ni utawala unaodhulumu haki za watu, unasemwa kwa mabaya mengi mpaka na wale waliokuwa wasaidizi wake wa karibu kabisa.

Kinachoendelea sasa, ni ujumbe murua kwa Rais Samia. Kama atakubali kupumbazwa na sifa za kinafiki za viongozi wa Serikali na CCM, ajue anaandaa kitabu cha kuja kusemwa vibaya sana na viongozi hao hao baada ya kutoka madarakani.

Atasemwa kuhusiana na mikataba ya bandari, mikataba ya kuwapa hifadhi za Taifa wageni wakati hakuna uwekezaji kwenye mbuga za wanyama na hifadhi za misitu, kwani uwekezaji ulikwishafanywa na Mungu. Waliopewa ni wavunaji na siyo wawekezaji.

Rais Samia atasemwa vibaya kwa kujifanya mwanademokrasia huku akikubali kupitisha sheria za uchaguzi na Tume huru ya uchaguzi zinazoua demokrasia na kuzuia uchaguzi huru na wa haki.

Watu husema kuwa mtu mwerevu hujifunza kutokana na yaliyowapata wenzake, iwe ni mazuri au mabaya. Je, Rais Samia atajifunza kutokana na watangulizi wake kusemwa vibaya kwa kuhakikisha tunapata sheria nzuri za uchaguzi na Tume ya uchaguzi au atakubali kupumbazwa na wanafiki wanaopanga kumsema vibaya akishatoka madarakani?

Nina hakika, kwa Rais mwerevu, anajifunza kutokana na historia, atasikiliza zaidi maoni ya wananchi kuliko maoni ya watu wanafiki ambao kula yao inategemea teuzi za Rais.
 
Hayati Magufuli akiwa Waziri wa Ujenzi, kila mara alimfia Kikwete. Kikwete alipoondoka madarakani, mara kadhaa indirectly au directly alimsema Kimwete na uongozi wake kuwa ulijaa ufisadi na upendeleo wa ajabu. Hayati hakuwahi kuyanena hayo, Kikwete akiwa madarakani. Lakini wapo watu wakweli wa nafsi waliusema utawala wa Kikwete ulivyokuwa umebobea kwenye ufisadi, Kikwete akiwa madarakani, ila walipuuzwa na wanaCCM.

Hayati Magufuli alipokuwa madarakani, kila kiongozi wa chama na Serikali alimpa sifa Hayati Magufuli za kila aina kiasi cha kutaka kuwaaminisha watu kuwa Magufuli ndiye alikuwa Rais bora kabisa Duniani. Baada ya kufariki, ubaya wa aina mbalimbali wa uongozi wa Magufuli, unasemwa mpaka leo, kuanzia kwenye udikteta, kudhulumu mali za watu, kuwabambikia watu kesi, kuwanyang'anya watu pesa zao, n.k. Sahizi utawala wa Magufuli, ambao watu wakweli waliusema akiwa hai kuwa ulikuwa ni utawala unaodhulumu haki za watu, unasemwa kwa mabaya mengi mpaka na wale waliokuwa wasaidizi wake wa karibu kabisa.

Kinachoendelea sasa, ni ujumbe murua kwa Rais Samia. Kama atakubali kuumbazwa na sifa za kinafiki za viongozi wa Serikali na CCM, ajue anaandaa kitabu cha kuja kusemwa vibaya sana na viongozi hao hao baada ya kutoka madarakani.

Atasemwa kuhusiana na mikataba ya bandari, mikataba ya kuwapa hifadhi za Taifa wageni wakati hakuna uwekezaji kwenye mbuga za wanyama na hifadhi za misitu, kwani uwekezaji ulikwishafanywa na Mungu. Waliopewa ni wavunaji na siyo wawekezaji.

Rais Samia atasemwa vibaya kwa kujifanya mwanademokrasia huku akikubali kupitisha sheria za uchaguzi na Tume huru ya uchaguzi zinazoua demokrasia na kuzuia uchaguzi huru na wa haki.

Watu husema kuwa mtu mwerevu hujifunza kutokana na yaliyowapata wenzake, iwe ni mazuri au mabaya. Je, Rais Samia atajifunza kutokana na watamgulizi wake kusemwa vibaya kwa kuhakikisha tunapata sheria nzuri za uvhaguzi na Tume ya uchaguzi au atakubali kupumbazwa na wanafiki wanaopanga kumsema vibaya akishatika madarakani?

Nina hakika, kwa Rais mwerevu, anajifunza kutokana na historia, atasikikiza zaidi maoni ya wananchi kuliko maoni ya watu wanafiki ambao kula yao inategemea teuzi za Rais.
Watu husema kuwa mtu mwerevu hujifunza kutokana na yaliyowapata wenzake, iwe ni mazuri au mabaya. Je, Rais Samia atajifunza kutokana na watamgulizi wake kusemwa vibaya kwa kuhakikisha tunapata sheria nzuri za uvhaguzi na Tume ya uchaguzi au atakubali kupumbazwa na wanafiki wanaopanga kumsema vibaya akishatika madarakani?
 
Unafiki ni kama nembo kwa mtanzania. Kuongea ukweli mbele ya mtu hawezi ila anasubiri aondoke ili amseme
 
CCM kwa bahati mbaya sana imejaa watu wanafiki. Watu ambao kwao kilicho muhimu ni kuwa na madaraka. Ndiyo maana huwezi kumsikia kiongozi wa CCM au Serikali akiikosoa CCM au Serikali au Rais, wakati Serikali hiyo au Rais huyo akiwa madarakani. Rais akiwa madarakani, wakati wote ni kumsifu kwa kila sifa kama vile hakuna Rais mzuri popote Duniani wa kufikia kiwango cha Rais wa Tanzania. Akiondoka madarakani ndiyo sasa ubaya na mapungufu yake yataanza kusemwa na wale wale waliokuwa wakimsifia.

Hayati Magufuli akiwa Waziri wa Ujenzi, kila mara alimsifia Kikwete. Kikwete alipoondoka madarakani, mara kadhaa indirectly au directly alimsema Kimwete na uongozi wake kuwa ulijaa ufisadi na upendeleo wa ajabu. Hayati hakuwahi kuyanena hayo, Kikwete akiwa madarakani. Lakini wapo watu wakweli wa nafsi waliusema utawala wa Kikwete ulivyokuwa umebobea kwenye ufisadi, Kikwete akiwa madarakani, ila walipuuzwa na wanaCCM.

Hayati Magufuli alipokuwa madarakani, kila kiongozi wa chama na Serikali alimpa sifa Hayati Magufuli za kila aina kiasi cha kutaka kuwaaminisha watu kuwa Magufuli ndiye alikuwa Rais bora kabisa Duniani. Baada ya kufariki, ubaya wa aina mbalimbali wa uongozi wa Magufuli, unasemwa mpaka leo, kuanzia kwenye udikteta, kudhulumu mali za watu, kuwabambikia watu kesi, kuwanyang'anya watu pesa zao, n.k. Sahizi utawala wa Magufuli, ambao watu wakweli waliusema akiwa hai kuwa ulikuwa ni utawala unaodhulumu haki za watu, unasemwa kwa mabaya mengi mpaka na wale waliokuwa wasaidizi wake wa karibu kabisa.

Kinachoendelea sasa, ni ujumbe murua kwa Rais Samia. Kama atakubali kupumbazwa na sifa za kinafiki za viongozi wa Serikali na CCM, ajue anaandaa kitabu cha kuja kusemwa vibaya sana na viongozi hao hao baada ya kutoka madarakani.

Atasemwa kuhusiana na mikataba ya bandari, mikataba ya kuwapa hifadhi za Taifa wageni wakati hakuna uwekezaji kwenye mbuga za wanyama na hifadhi za misitu, kwani uwekezaji ulikwishafanywa na Mungu. Waliopewa ni wavunaji na siyo wawekezaji.

Rais Samia atasemwa vibaya kwa kujifanya mwanademokrasia huku akikubali kupitisha sheria za uchaguzi na Tume huru ya uchaguzi zinazoua demokrasia na kuzuia uchaguzi huru na wa haki.

Watu husema kuwa mtu mwerevu hujifunza kutokana na yaliyowapata wenzake, iwe ni mazuri au mabaya. Je, Rais Samia atajifunza kutokana na watangulizi wake kusemwa vibaya kwa kuhakikisha tunapata sheria nzuri za uchaguzi na Tume ya uchaguzi au atakubali kupumbazwa na wanafiki wanaopanga kumsema vibaya akishatoka madarakani?

Nina hakika, kwa Rais mwerevu, anajifunza kutokana na historia, atasikiliza zaidi maoni ya wananchi kuliko maoni ya watu wanafiki ambao kula yao inategemea teuzi za Rais.
Upo sawa kabisa ,watakao anza ni hawa , machawa
 
Unafiki ni kama nembo kwa mtanzania. Kuongea ukweli mbele ya mtu hawezi ila anasubiri aondoke ili amseme

Ndiyo maana kiongozi mwenye akili unatakiwa kupuuza na kuwakemea machawa kwa sifa zao za kinafiki. Unatakiwa angalao usikilize maoni ya wale ambao matumbo yao hayategemei wala kutafita teuzi zako.
 
Na huo ndio ukweli.Atasemwa sana atakapotoka madarakani.

Ugawaji hovyo wa rasilimali za nchi kupitia ile mikataba 30 aliyosaini alipoenda kwenye maonesho kule Dubai, lazima itawekwa wazi, na hawa hawa wanaomsifia watalaani kama vile wakati inasainiwa hawakuwahi hata kusikia.
 
Back
Top Bottom