Waliotaka kuizunguka katiba wasilaumiwe, ilaumiwe CCM

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,246
113,631
Mahojiano aliyoyafanya mkuu wa majeshi mstaafu yametufungulia kaupenyo kwenye dirisha la kilichokuwa kinaendelea kwenye siku za mwisho za uhai wa Rais Magufuli.

Kitendo cha mkuu wa majeshi na wenzake waliokuwepo wakati Rais Magufuli anavuta pumzi yake ya mwisho na ‘sintofahamu’ iliyojitokeza juu ya nini kifanywe baada ya kufa kwa marehemu wakati katiba iliyopo inaelezea vizuri tu utaratibu wa kurithi madaraka endapo Rais aliyekuwepo madarakani anakufa au anashindwa kufanya kazi yake ni hukumu mbaya dhidi ya CCM kuhusu utamaduni wa kuvunja katiba walioutengeneza wao wenyewe.

Katiba iko wazi kuhusu utaratibu wa kurithi uongozi wa nchi.

Lakini kumbe kulitaka kutokea ujanja ujanja wa kuvunja tena katiba mkiuke taratibu zilizopo.

Tutawalaumu vipi hao watu [sina hakika sana ni akina nani] wakati marais wa Tanzania ndo vinara wa kuvunja katiba?

Wenyeviti wa CCM ndo wavunja katiba wakuu. Kuanzia Nyerere mpaka Samia….wote wavunjaji wa katiba hawa.

Ndo maana haishangazi kuona au niseme kusikia kuwa kuna watu walitaka tena kuikiuka katiba na kufanya vile watakavyo wao baada ya Magufuli kufariki.

Ambaye angekuwa mhanga wa hilo naye alipoingia madarakani akaendeleza mambo yale yale ya uvunjaji wa katiba kana kwamba hakupata somo la kuiheshimu katiba walipotaka kumtenda.

Kaingia madarakani akaendeleza mambo yaleyale ya kupiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa [ambayo ni haki ya kikatiba] na akatoa kisingizio dhaifu sijapata kuona. Eti anatengeneza uchumi kwanza.

Hilo zuio haramu halipo tena. Ina maana uchumi ulishatengemaa?

Na ni wapi kwenye katiba panapomruhusu yeye kuzipiga marufuku haki za kikatiba kwa kisingizio cha kujenga uchumi?

Marais wote wa Tanzania ni wavunjaji wa katiba. Haishangazi kusikia kuna wengine nao walitaka pia kuivunja katiba kwenye kuurithi urais!

Uvunjaji wa katiba Tanzania ni zao la CCM na wala huwa hawakemeani. Sana sana huwa wanateteana.

Hivyo, waliotaka kuivunja katiba na kumtenda makamu wa Rais Samia, wala wasilaumiwe sana.

They are products of their environment.
 
Kabla ya kuongelea mambo ya katiba. Swali alilopaswa kuulizwa Mabeyo kwanza ni kwa nini wananchi hawakujulishwa juu ya ugonjwa na wakati Rais anaumwa wanakuja kutangaziwa kifo?

Mbona kifo walitangaza, lkn wakati anaumwa hawakusema. Ingefaa wakae kimya hivyo hivyo waendelee na maziko na huo uvunjaji wa katiba, unawezaje kuambia wananchi katiba ilitaka kuvunjwa wakati huyo aliyekufa hawakuambiwa km yu mgonjwa!
 
Kabla ya kuongelea mambo ya katiba..Swali alilopaswa kuulizwa Mabeyo kwanza ni..kwa nini wananchi hawakujulishwa juu ya ugonjwa na wakati Rais anaumwa wanakuja kutangaziwa kifo?
Mbona kifo walitangaza, lkn wakati anaumwa hawakusema..ingefaa wakae kimya hivyo hivyo waendelee na maziko na huo uvunjaji wa katiba, unawezaje kuambia wananchi katiba ilitaka kuvunjwa wakati huyo aliyekufa hawakuambiwa km yu mgonjwa!
Wengine nao wako wapi waje waongee?
 
sifi leo

Ujumbe wa Leo wa Rais Sa100 TBC saa 05:20 haujasikika vizuri ulikua unakwaruzakwaruza sijui kwanini sijasikia kitu kabisa umekwaruzakwaruza tu alafu tunaambiwa huo ndio ujumbe wa Leo wa Rais alipokuwa ......
 
Wewe muwaza vyeo Nyani Ngabu !
Wakati unawaza vyeo pamoja na wasakatonge wenzako!
Sisi wengine tunajiuliza....
Swali muhimu!
Ni kwa nini walituficha ugonjwa wa mpendwa Rais wetu JPM?
Tunajiuliza ...
Dk Janabi alikuwa pale muda wote akifanya nini ilhali yeye hakuwahi kuwa Daktari wa JPM,bali alikuwa ni Daktari wa familia ya Kikwete na pia swahiba ya JK?

Tunajiuliza ...ni kwa nini walikwenda kumficha pale Mzena badala ya kumpeleka kwenye hospitali nyingine yenye hadhi ikiwezekana hata nje ya nchi?

Tunajiuliza .... kama waziri mkuu alituficha!,Makamu wa Rais alituficha!

Ni nani au kikundi gani kilikuwa kinaratibu haya mambo?
Tunajiuliza....

Kama Mkuu wa majeshi aliambiwa na JPM awali kwamba wamrudishe nyumbani akafie huko.Ni kwa nini aligoma kutimiza takwa la Marehemu?

Na kwa nini hakuwashirikisha wengine ili wachukuwe maamuzi sahihi?
Je!
Magufuli aliugua ugonjwa gani huo ambao madaktari walikaa pembeni wakimshuhudia akipigania uhai wake akiwa kama mateka?Anasema alipofariki wao wakuu wa vyombo ndio waliwajulisha viongozi kama PM, CS na baadae makamu wa rais.. Tena wote hawakuwepo eneo la tukio...

Hatuoni mahala makamo wa Rais,mwanasheria mkuu, Wala jaji mkuu au spika wakiwa na maamuzi yeyote. Kila kitu kilipangwa na jeshi.
Huyu Mabeyo ameongea....
Iko siku na wengine wataanza kuongea!
Damu ya mtu huwa haipotezwi bure....
Tunashuhudia taraatiiibu!
R.I.P Jemedari JPM!

Wameanza kuropoka huku!
 
Mimi nawaza vyeo gani?
 
Kama Mkuu wa majeshi aliambiwa na JPM awali kwamba wamrudishe nyumbani akafie huko.Ni kwa nini aligoma kutimiza takwa la Marehemu?
Yote uliyoandika uko sahihi kabisa isipokuwa kipengele hiki.

Kuna mazingira ambayo mlengwa anakuwa hana maamuzi, ni kama ilivyokuwa kwa JPM kwa wakati huo.
Hapo aliyekuwa na maamuzi ya mwisho ni DAKTARI pekee yake na sio vinginevyo.
 
Kucheza rafu za Katiba ni utamaduni wa CCM. Kufanya mambo kwa mazoea ni utaratibu wa CCM
Kukiuka kanuni na tamaduni ni taratibu za CCM.

Taratibu hizo ndizo zinawzwezesha kutuchezea Raia Rafu za Kikatiba

Kilichobadilika baada ya JPM kufariki ni uwepo wa pande mbili ambazo ilibidi zichezeane Rafu kwanza kabla ya kutuchezea sisi Raia. In the end atakayeshinda atatuchezea Rafu na lipo wazi, anatuchezea Rafu

Hakuna shaka lipo kundi lililotaka kucheza rafu ya kukiuka katiba na kuwaweka wahusika pembeni.

Msikilize CDF, ni wazi yeye aliamua ugomvi na kumpa aliyestahili kwa mujibu wa Katiba.

Kikao cha CCM cha uteuzi Marais wastaafu wote walihudhuria kuashiria kwamba waliona tatizo la Wahuni

Mstaafu mmoja alisikika akimwambia mmoja wa ' Wahuni'', '' Bwana wewe si umeondoka huku kwenye chama na upo serikalini, huku kwenye vikao vya chama unafuta nini, tulishatenga chama na serikali, ondoka''.
Huyo ndiye alikuwa kiongozi wa Wahuni

Aliyeingia akawafyeka Wahuni wote, lakini hajaacha utamaduni na mila za CCM za kuisigina Katiba.
 
Back
Top Bottom