Rais Magufuli ataja sababu kusitisha ujenzi bandari ya Bagamoyo kwa Mkopo wa Dola Bilioni 10

Sasa hayo mazungumzo yalikuwa yanaendeshwa na nani kama sio serikali ya huyo unayesema maamuzi yalipitishwa baada ya kufa?

Na kumbe Magufuli alisemaje kwenye hiyo video niliyokuwekea?

The problem, hujawahi kutoa hoja yoyote kuhusu ubaya wa huu mradi!! Kila siku, the same old story... mara kuna upigaji, mara vile!! Mara Kikwete, mara Zitto... jadili faida na hasara za mradi!

Hakuna asiyefahamu kwamba nchi hii kuna upigaji!! Hoja hapa ni faida na hasara za mradi, na namna gani mradi unaweza kufanywa kwa maslahi ya nchi.

Hicho ndicho unachotakiwa kujadili! Na ndicho mara zote nimekuwa nikijadili!!!

Au unataka kusema upigaji utakuwa kwenye Bandari ya Bagamoyo tu, na kwingine kote hakuna upigaji?! Au ndo yale yale ya kutuaminisha mwizi mkubwa nchi hii ni Acaccia na makinikia yake, wakati kampuni zote za madini ni wale wale tu??!

Hiyo obsession yako na akina Zitto, nakuachia mwenyewe!!
Sina obsession ila najua jamaa ni wapigaji tu. Zitto ni mnafiki na mbinafsi kuliko.
 
Back
Top Bottom