Rais Magufuli ataja sababu kusitisha ujenzi bandari ya Bagamoyo kwa Mkopo wa Dola Bilioni 10

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
618
1,000
1123438

RAIS John Magufuli amesema sababu kubwa ya kusitishwa kwa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ni masharti magumu yaliyomo katika mkataba wa utekelezaji wa kazi hiyo.

Jiwe la msingi la ujenzi wa bandari hiyo liliwekwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwaka 2015 na ulitarajiwa kugharimu dola za Marekani bilioni 10. Bandari hiyo endapo ingejengwa ingekuwa kubwa zaidi Afrika Mashariki ikiwa na ukubwa wa ekari 3,000 na viwanda 190 vingejengwa.

Akizungumza jana kwenye mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) uliowashirikisha wafanyabishara kutoka wilaya 139 nchini, Rais Magufuli aliweka wazi sababu za kusitishwa kwa ujenzi wa bandari hiyo. Rais Magufuli alisema “kwenye mkataba wa ujenzi wa bandari hiyo kulikuwa na vipengele vya ovyo”. Rais Magufuli alisema mojawapo ya masharti ni kutojengwa wala kuendelezwa kwa bandari yoyote kuanzia eneo la Tanga hadi Mtwara.

"Yaani kwenye eneo lote kuanzia Tanga hadi Mtwara kusijengwe bandari yoyote. Bandari ya Kilwa tusiiendeleze, Bandari ya Mtwara ambayo itawezesha mikoa ya kusini kupokea mafuta badala yake Dar es Salaam kisha yarudi huko, hatutakiwi kuiendeleza, Barabara kutoka Mtwara hadi Bamba Bay ambayo itatuwezesha kusafirisha mizigo hadi Msumbiji tusiijenge," alisema Rais Magufuli

Pia alisema wawekezaji hao wangeweza kumiliki ardhi kwa hati ya miaka 99 pamoja na kutoruhusiwa kuuliza nani anamiliki eneo hilo. Rais Magufuli alisema sharti lingine ni gharama zitakazotumiwa na mwekezaji huyo katika ujenzi wa bandari hiyo kutakiwa kurejeshwa.

Soma pia:
Bandari ya Bagamoyo: Je, sababu alizotoa Rais Magufuli ni za kweli?. Je, haya mazungumzo ni ya nini tena kama wameachana na mradi huo? - JamiiForums
 
mwanawao

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
2,402
2,000
Shamba la bibi, kuna mambo lazima tukubali Rais wetu anajitahidi sana kuyaweka vizuri na tumpe heko. Katika kulinda uridhi wetu kwa kweli nampa heko, anajitahidi sana.

Mikataba ya hovyo kama hii ni wizi wa mchana kabisa. Hamna maslahi kwetu kama watanzania. Hii mikataba kama ya mangungo ifutiliwe mbali.

Natamani aingilie mikataba ya gasi pia, kule nako sijui kama tupo salama.

Kama watakubaliana na mkataba ambao ni win win wajenge ila mkataba ambao hatufaidi chochote, hatuhoji chochote yaani tumeuza uridhi wetu kwa miaka 99 bila chochote watu wanachuma tu, tena bado turejeshe gharama na hatuna uwezo wa kufanya chochote mbadala, hapana kwa kweli..khaaa

Heko Rais, tuliendie urithi wetu tutakukumbuka kwa hilo.
 
Kahise

JF-Expert Member
Jul 25, 2008
349
500

Mikatabba ya Kiwanja cha ndege cha Chato, ya Stiegler's Gorge, ya ununuzi wa ndege pia viwekwe hadharani, ili Watanzania wafanye comparisons!
 
Kiyawi

JF-Expert Member
Nov 30, 2011
1,857
2,000
Shamba la bibi, kuna mambo lazima tukubali Rais wetu anajitahidi sana kuyaweka vizuri na tumpe heko. Katika kulinda uridhi wetu kwa kweli nampa heko, anajitahidi sana.

Mikataba ya hovyo kama hii ni wizi wa mchana kabisa. Hamna maslahi kwetu kama watanzania. Hii mikataba kama ya mangungo ifutiliwe mbali.

Natamani aingilie mikataba ya gasi pia, kule nako sijui kama tupo salama.

Kama watakubaliana na mkataba ambao ni win win wajenge ila mkataba ambao hatufaidi chochote, hatuhoji chochote yaani tumeuza uridhi wetu kwa miaka 99 bila chochote watu wanachuma tu, tena bado turejeshe gharama na hatuna uwezo wa kufanya chochote mbadala, hapana kwa kweli..khaaa

Heko Rais, tuliendie urithi wetu tutakukumbuka kwa hilo.

Hiyi ilikuwa kazi kuu ya serikali ya awamu ya nne na watendaji wake wakuu!! Halafu unaona watu wanakenua!!

Hata mababu zetu ambao hawakuwa wamepata elimu ya hata kindergarten ya Kimangaribi(Western education) hawakuwa na akili finyo kama za wasomi wa vyuo vikuu wenye Masters na PhDs!!!! Kudos Rais Dr Magufuli.
 
Chiwa

JF-Expert Member
Apr 17, 2008
3,076
2,000
safari bado ndefu lakini tukumbuke safari moja huanzisha nyingine!
 
Mungo Park

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
1,691
2,000
Kwa hili la bagamoyo Port nahisi bado tulipaswa kulipa kipaumbele cha kipekee.
Tumeangalia Zaidi upande wetu lakini tumeshindwa kuangalia upande wa wanaotoa fedha za kuijenga.
Kwa hali ya kawaida dola bilioni 10 siyo kitu cha mchezo mchezo.
Tulipaswa kuangalia pia yafuatayao:
  • Biashara za kando zitakazo anzishwa(adjacent businesses).
  • Viwanda vitakavyoanzishwa.
  • Nafasi za ajira kwa watu wetu.
  • Kupanuka kwa mji hadi kuwa jiji kwa Bagamoyo.
Kuhusu vipengele vya mkataba nafikiri kulikuwa na nafasi ya kujadiliana na kufikia muafaka kwani nia yao nafikiri ilikuwa kulinda mtaji wao na kupata faida walioitarajia.
Tulitakiwa kujua pia namna ya Bandari nyingine kama Rotterdam,Hong Kong n.k. zinavyoendeshwa.
Tutambue kuwa nchi yetu ni kubwa na tunahitaji maendeleo ya haraka ya watu wetu.
 
mludego

JF-Expert Member
Mar 16, 2013
1,583
2,000
Duuh Zitto amesharudi tena chadema? Mradi ni mzuri ila mkataba ndio mbaya
Niliwashangaa sana Chadema kutetea huu mradi, isijekuwa wabunge wa hiki chama walirubuniwa. Nina mashaka sana na Zito kwa sasa. Maana aliutetea sana huu mradi.
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
9,391
2,000
Pale tunaposhangilia Kutokuwa na bandari badala ya kuwa na Bandari!

Serikali ya awamu ya Tano inanikumbusha msemo maarufu wa Waziri Njonjo wa Kenya aliyeipiga vijembe serikali ya Nyerere baada ya Nyerere kutoa kauli ya kuiikejeli Kenya kwa kusema "Kenya is a man eat man society", Njonjo akasema “Tanzania is a man eat nothing society"!
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
40,709
2,000
Tulishazisema hizo sababu hapa na Rais amethibitisha.

Ni Tanzania tu ambapo kiongozi aliyekuwa kimya mpaka mkataba wa kinyonyaji ukapita anakuja kusema huo mkataba ulikuwa mbovu! Wakati huo huo hata yeye huo Mkataba hataki kuonyesha nini kiko ndani ya huo mkataba alipokubali upite, kisha akaukataa. Kichekesho ni pale rais huyo huyo anapogomea katiba mpya ili mambo yaendeshwe kwa uwazi zaidi na watu wanashangilia na kusema ni kiongozi sahihi!
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
23,252
2,000
Sera ya uwezezaji ya CCM inasemaje kuhusu mambo haya? maana hayakuota kama uyoga..ni lazima yalianzia kwenye chama ambacho ndicho kimepewa ridhaa ya kuongoza Serikali...

CCM tunaomba majibu ya kina tafadhali juu ya mkanganyiko huu -- inapofikia Rais wa nchi anasema "Hajawahi kuona Project ya kijinga kama hii" kwa kweli ni kauli nzito sana.

CCM tupeni majibu......
 
stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
11,994
2,000
Shamba la bibi, kuna mambo lazima tukubali Rais wetu anajitahidi sana kuyaweka vizuri na tumpe heko. Katika kulinda uridhi wetu kwa kweli nampa heko, anajitahidi sana.

Mikataba ya hovyo kama hii ni wizi wa mchana kabisa. Hamna maslahi kwetu kama watanzania. Hii mikataba kama ya mangungo ifutiliwe mbali.

Natamani aingilie mikataba ya gasi pia, kule nako sijui kama tupo salama.

Kama watakubaliana na mkataba ambao ni win win wajenge ila mkataba ambao hatufaidi chochote, hatuhoji chochote yaani tumeuza uridhi wetu kwa miaka 99 bila chochote watu wanachuma tu, tena bado turejeshe gharama na hatuna uwezo wa kufanya chochote mbadala, hapana kwa kweli..khaaa

Heko Rais, tuliendie urithi wetu tutakukumbuka kwa hilo.
"Natamani aingilie mikataba ya gasi pia, kule nako sijui kama tupo salama"Hata mimi natamani aingilie huku ingawa najua huku pia lazima kuna michezo imechezwa na hakuko salama...
 
Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
2,141
2,000
Niliwashangaa sana Chadema kutetea huu mradi, isijekuwa wabunge wa hiki chama walirubuniwa. Nina mashaka sana na Zito kwa sasa. Maana aliutetea sana huu mradi.
Ila hujiulizi nani alikuwa waziri wako wa ujenzi wakati president kikwete anaweka jiwe hili la msingi,why hawaku rise hizi issue?,uoga wao na njaa ya matumbo yao wakawa kimya kulinda vibarua vyao na sasa wanataka kujifanya ni mashujaa,politics za kinafiki zitatuumiza sana nchi hii ,na tukitukanwa kwa kuitwa pithole country tunachukia wakati ndio ukweli wenyewe.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom