Rais ajaye ni lazima awe mkristo?

Rais ajaye ni lazima awe mkristo?

Mkuu Nduka, ukienda kwenye mnada wa hadhara, kama hicho kitu unakitaka wewe, utakwewnda na timu 3. Timu moja ni ya kwako mwenyewe, timu nyingine ni ya kuwakimbiza serious contenders wote kwa kila atakayeku outbid kwa kupaisha dau kwa kuwafurusha wote wanaojaribu hadi mwisho wa siku, the highest bidder ni mtu wako, the second highest pia ni wako na wewe ndio the 3rd.

Wakati wa kulipa, the ist and the 2nd watafanya no show, ili mzigo uangukie kwako!.

Kwa wanaozijua siasa za nchi hii, JM na EL ni kambi ile ile sponsored by "the King Maker!", kuna watu niliwaeleza humu tangu mwanzo, kuna watu ni just "pace makers" na kina Yohana Mbatizaji tuu, wakiyanyoosha mapito ya "the chosen one!", hawakunielewa!, labda sasa wataelewa kwamba "that is what is the name of the game!", na kujua "the games people play!", "plays our minds away!".

Pasco
This is the name of the game!.
Pasco
 
Sasa kuna asiye fisadi, wewe tu mwenyewe wakikupa urais kitu utacho anzanacho ni ufisadi, rais ajaye awe fisadi, awe nini lakin awe tu mkristo, wenzetu watoto wa mamdo mme prove fairure ktk uongozi. Hihihihiiiiiiiiiiiiiikwiiiiiiiiiiiii!

Kwa hiyo hata akiwa fisadi kwako bora tu awe mkristo? Sawa ni maoni yako mkuu!
 
Mkuu Nduka, ukienda kwenye mnada wa hadhara, kama hicho kitu unakitaka wewe, utakwewnda na timu 3. Timu moja ni ya kwako mwenyewe, timu nyingine ni ya kuwakimbiza serious contenders wote kwa kila atakayeku outbid, mtu wako atamfurusha kwa ku bid very high hadi mwisho wa siku, the highest bidder ni mtu wako, the second highest pia ni wako na wewe ndio the 3rd.

Wakati wa kulipa, the ist and the 2nd watafanya no show, ili mzigo uangukie kwako!.

Kwa wanaozijua siasa za nchi hii, JM na EL ni kambi ile ile sponsored by "the King Maker!", kuna watu niliwaeleza humu tangu mwanzo, kuna watu ni just "pace makers" na kina Yohana Mbatizaji tuu, wakiyanyoosha mapito ya "the chosen one!", hawakunielewa!, labda sasa wataelewa kwamba "that is what is the name of the game!", na kujua "the games people play!", "plays our minds away!".

Pasco
You're VERY RIGHT... Siku nilipopata fununu za JM kuutaka u-Rais nikaanza kwanza kufikiria ni mchezo gani hasa anaoufikiria kuucheza na EL. Nikajaribu kujiuliza ikiwa inataka kufanana na mchezo ambao Ghalib Bilal alipata kuucheza kwa kushirikiana na Ibrahim Raza... mpaka sasa natafakari, sijapata picha... au labda JM anatangulizwa kuandaa kikosi... hata mkimfyeka, Jemadari mwenyewe yupo nyuma hivyo wafuasi wamfuate Jemedari... sijapata jibu, sijapata jibu... jibu pekee nililo nalo ni makubaliano ya EL kuwa President na JM kuwa Prime Minister... Hata JM nae anafahamu kabisa kwamba for the time being, u-PM unamtosha sana unless airejee na kutishwa na historia ya JK na EL... RA mwenyewe ametulia tu wakati watu mnahangaika....
 
Pasco ndugu yangu umehama kambi ya Lowassa?
Bora ushabikie Wassira kuliko huyo Makamba.
Mkuu Nduka, ukienda kwenye mnada wa hadhara, kama hicho kitu unakitaka wewe, utakwewnda na timu 3. Timu moja ni ya kwako mwenyewe, timu nyingine ni ya kuwakimbiza serious contenders wote kwa kila atakayeku outbid kwa kupaisha dau kwa kuwafurusha wote wanaojaribu hadi mwisho wa siku, the highest bidder ni mtu wako, the second highest pia ni wako na wewe ndio the 3rd.

Wakati wa kulipa, the ist and the 2nd watafanya no show, ili mzigo uangukie kwako!.

Kwa wanaozijua siasa za nchi hii, JM na EL ni kambi ile ile sponsored by "the King Maker!", kuna watu niliwaeleza humu tangu mwanzo, kuna watu ni just "pace makers" na kina Yohana Mbatizaji tuu, wakiyanyoosha mapito ya "the chosen one!", hawakunielewa!, labda sasa wataelewa kwamba "that is what is the name of the game!", na kujua "the games people play!", "plays our minds away!".

Pasco
This is the game people play!.
Pasco
 
Mkuu umeandika maneno ya maana sana, lakini unfortunately, hali halisi haiko hivyo!

Labda kama unadhani tumepata marais wa dini za tofauti kila awamu kwa bahati mbaya?

Hilo hatuwezi kulikwepa mkuu!

It is an unwritten rule! Akija rais muislam awamu ijayo lazima kutakuwa na maneno!
Sioni kama kuna mtu aliyepata Urais wa ajili ya dini yake. Mwalimu alipotoka madarakani, alitaka nchi iongozwe na Mzanzibar... si kutokana na uhodari wao kwenye kuongoza bali alifahamu harakati za kisiasa za ZNZ... alihofu, akija m-Bara mwingine, ZNZ wanaweza kusumbua sana! INgekuwa lengo kuu la Mwalimu ni nchi kuongozwa na Mwislamu, basi angemwachia Rashidi Kawawa... lakini alitaka Mzanzibari.

It's very (un)fortunately kwamba, utakapoweka kigezo cha u-ZNZ, basi probability ya option husika kubeba na Uislamu ni 99%! Hata hivyo, probability hii kwa Mwalimu aliona ni kama kupiga ndege wawili kwa jiwe moja... jambo la msingi ni kwamba, hata kama ZNZ ingekuwa majority/all ni christians, bado urais 1985 ungeenda huko.

Tukija Mkapa, ingawaje by coincidence inaonekana ilikuwa ni kukamilisha ile trend, ukweli ni kwamba Mwinyi alikuwa ameivuruga sana hii nchi. Hapa Nyerere akataka apate mtu anayemuwamini... mtu anayemfahamu in and out!Kwa bahati mbaya, akadhani anamfahamu Mkapa kumbe alikuwa hamfahamu pamoja na kwamba alimfundisha mwenyewe na kufanya nae kazi!

2005 watu tunapenda sana kujitia upofu! Ulizeni NEC ya CCM 1995... KIkwete alikuwa na nguvu sana kwenye mchujo wa 1995... kama pangekuwa na fairness, JK ndie angesimama 1995 lakini kwa bahati mbaya, Mwalimu alitaka mtu anayemfahamu vizuri ili azibe mashimo yaliyoachwa na Mwinyi. Kwa wafuatiliaji wa siasa za nchi hii, wanakumbuka neno MIZENGWE liliibuka na kushika kasi Dodoma... ni kwamba Mwalimu alimfanyia mizengwe JK. Sasa basi, baada ya uchaguzi wa 1995, JK akajitahidi sana kujiepusha na kashifa zozote... na ile kupewa uwaziri wa foreign affairs kukamsaidia sana kujiepusha na domestic scandals. Hata watoto wake, akawa anasomesha shule hizi hizi za kiswahili, ili mradi tu pasije wakatokea wa kusema "watoto wake wanasoma Ulaya!" Kutokana na hilo, JK akaingia kwenye kinyang'anyiro cha 2005 akiwa na nguvu kubwa mno....Mtu pekee ambae angekuwa tishio kwa JK ni EL na SAS. Kwa bahati mbaya/mzuri, EL akaingia ubia na JK, kwahiyo tishio kuu akabaki SAS!

Hata hivyo, JK alikuwa na advantage moja ukiliganisha na SAS... kule ZNZ, bado zile siasa zao za Hizbu na ASP bado zilikuwa na nguvu... wanazi wa CCM kutoka ZNZ, wakamkwamisha SAS ingawaje watu wanasema JK alimchafua SAS.
 
Mkuu issue ya kuchagua mwanamke ama kijana ipo kwenye katiba?

Soma vyema mkuu, hakuna pahala nimesema ndo kigezo kikuu, pitia mabandiko mkuu!

Wenye kuchagua kiongozi anayewafaa ni wananchi, na hiyo ndo demokrasia! Demokrasia pia ni uwezo wa kutoa maoni bila kubughudhiwa almradi hujavunja sheria za nchi!
jmushi1,
Hata kama utakataa vipi, wewe hoja yako umesukumwa na UDINI lakini unajibaragua... danganyana wengine, lakini kama mimi huwezi kunidanganya kwavile kwa kumbukumbu zangu, nimeshaktana na wewe angalau mara mbili kwenye mijadala kama hii huku mara zote ukitaka kujifanya sio mdini... hii hoja yako hapa umesukumwa na yale yale ambayo nilishapaa kukuambia jamvi hili hili la siasa

Aidha, umekuwa ukirudia mara kwa mara kwamba "issue ya kuchagua mwanamke ama kijana ipo kwenye katiba?" Hii hoja hapa haina mashiko, haitoshelezi japo robo ya kiganja. Nchi hii, and in fact, duniani, hakuna lethal struggles basing on gender or age-group. Na ni kutokana na hilo, ndipo mamlaka huwa zinafanya upendeleo wa wazi wazi basing on gender or age group lakini kwa nchi kama zetu huwezi kufanya hivyo basing on religion coz' it's very sensitive issue. Kwahiyo leo kusema tuchague mtu kutokana na dini yake kwavile tayari tunafanya hivyo basing on gender or age group ni upotofu wa hali ya juu!!

Binafsi, ingawaje mimi ni Mwislamu, lakini wala sioni Mwislam anaefaa miongoni mwa hawa wanaotajwa tajwa. Si kwa sababu Rais wa sasa ni Mwislamu bali hawa tunaowafahamu hawatoshi(with exception of SAS ambae hata hivyo nae umri umeenda sana). Lakini wewe unataka kiongozi Mkristo si kwa sababu hakuna Mwislamu anayetosha bali kwavile Rais wa sasa ni Mwislamu basi anayekuja awe mkristo... HUO NI UDINI USIO NA MAANA mbao hautakusaidia wewe wala familia yako... sana sana utafaidika na stupid social satisfaction...
 
Kwa wale wanaodai ni zamu ya zanzibar kutoa raisi, mlishachelewa zamu yenu ilikuwa baada ya mkapa, mlikuwa wapi hamkupiga kelele kipindi kile? Imeshakula kwenu hiyo....
 
ina maana mkuu pasco umeshamjua raisi mtarajiwa:A S 11:
 
Msituhamishie kwenye dini na raisi ajae ,hapa kuna jambo hapa ,wacheni limalizike hili halafu tuangalie kwengine ,yaani nyie mnatupumbaza sana ,mlitupeleka kwenye gesi kumbe mmeshaliwa zamani, mkatuhamishia kwenye denguo kumbe hilo gonjwa linatesa tokea zamani halikupewa nafasi kwenye media tu ,haya hivi sasa kumenuka homa ya bonde la ufa na hapa mnashuka na hili la mgombea ,aloo yote hayo ya nini ?

Katiba mpya kwanza hayo ya mgombea na msungura baadae ,Tunahitaji kuona CCM mnarudi kwenye meza na akili zenu timamu mambo ya kujifanya MAZUZU na kuja na rasimu zenu mifukoni.

NB*
Huu ni wakati mfumo wa vyama vingi huo utamaduni wa raisi ajae awe muislamu au mkiristo umeshapitwa na wakati ,maana kama mnataka hivyo ni lazima Tume hiyo huru ya Uchaguzi itakayokuja ni lazima itoe tangazo au ILANI kuwa safari hii kila Chama kilete Mgombea URAISI Mkiristo na si vinginevyo.

Nionavyo mgombea yeyote yule anafaa awe wa dini yeyote pengine wa dini tofauti na yako akakujali na kukuletea maendeleo kuliko yule wa dini moja na wewe kama inavyoonekana.
 
Kwa wale wanaodai ni zamu ya zanzibar kutoa raisi, mlishachelewa zamu yenu ilikuwa baada ya mkapa, mlikuwa wapi hamkupiga kelele kipindi kile? Imeshakula kwenu hiyo....

Tatizo WaTAnganyika ni wabaguzi WaZanzibari hatutegemei kupata Raisi wa JMT na kwa vile Tumekaliwa na kutawaliwa na Mkoloni wetu Tanganyika ndio kabisa ,subirini tuwe huru ,yaani siku tukipokea Uhuru kutoka Tanganyika tu tutafanya sherehe za aina yake na tutaitangazia dunia na kuandika kwenye vitabu ,nchi ya mwisho kupata uhuru.
 
Umebadili kambi?

Hahahaa..........jumping ship? The old one is sinking faster than Titanic!

Rats_jump_ship.jpg


Aint the first.....

KATUNI%252528493%252529_thumb%25255B3%25255D.jpg
 
Uhuru lazima uwe na mipaka, ndio maana kuna maeneo watu huchora mistari ya kuonyesha mwisho wa jambo. Dunia ya sasa inaelekea kubaya sababu ya kusingizia uhuru, ndio maana ushoga, usagaji unapewa audience ya lazima, comment yangu ya kwanza inasimama.

Na wewe ni mmojawapo uliolike baadhi ya hizo comment za kipuuzi, Nimesikitishwa sana.
Kwa taarifa tu mimi ni mchaga na mkristo lakini NACHUKIA SANA UDINI NA UKABILA.
Wise of you
 
Wenye tabia ya kumchugua rais kwa kuangalia dini yake ni CCM.Kwa hiyo zamu inayofuata ni ya rais mkristo kuiongoza CCM.Tanzania itaongozwa na rais yeyote mwenye uwezo wa kuiletea nchi maendeleo pasipokujali imani yake.
 
Wenye tabia ya kumchugua rais kwa kuangalia dini yake ni CCM.Kwa hiyo zamu inayofuata ni ya rais mkristo kuiongoza CCM.Tanzania itaongozwa na rais yeyote mwenye uwezo wa kuiletea nchi maendeleo pasipokujali imani yake.

Na sio mkristu tu ni lazime awe Mkatoliki
 
Kama tunatizama dini kwa nini basi tusiende kutafuta maraisi mapandre au mashekhe sifa zake ndio zitampa uraisi
 
Haitakuja kutokea tena hii inchi iongozwe na mwislam
 
Nimefurahi sana, maana Urais unazungumzwa sana. ila cha msingi Rais ajae ajue watannganyika si wadanganyika tena!! Hilo tu
 
Back
Top Bottom