Mushi,
Mbona huufikiria ni wakati sasa Wazanzibari nao waiatowa Rais wa Tanzania ili kudumisha muungano wetu badala yake unapigia debe rais Mkristo? Hii ni kwasababu Tangu Mkapa na Kikwete ni miaka zaidi ya 20 sasa hatujaongozwa na Rais Mzanzibari (Hata huyo Mwinyi anahisiwa sio Mzanzibari Mzawa bali mzawa wa Mkuranga).
Au unaongozwa na msukumo wa udini nyuma yako?
Heshma mbele mkuu! Long time not see you mkubwa!
Mkuu tuko pamoja kabisa! Nashangaa sana wanaoipinga rasimu ya katiba mpya iliyopatikana kutoka kwa wananchi na kuwakilishwa kwenye bunge maalum la katiba na mh jaji Warioba.
Ninaweza kuzungumzia hilo, lakini ni ukweli wa wazi kuwa serikali mbili ni kizungumkuti.
Kabla ya hapo, bado tulikuwa tukielekea upande huo huo ninaouzungumzia hapa(wa kupokezana)
Kumbuka Mwinyi alipokuwa akizungumziwa kuwa ni jiwe moja kuuwa ndege wawili? Kwamba alikuwa muislam na kwa asili katokea Zanzibar?
Hadi usawa huu, hatuna utaratibu tena wa kupokezana madaraka kati ya nchi ya Zanzibar na Ile ya Tanganyika! Ndo maana baada ya Mwinyi, hakujawa na rais mwananchi wa Zanzibar aliyetokea kuwa rais wa muungano! Maana kwanza Zanzibar hawana shida kubwa kuhusiana na maamuzi wanayotaka kufanya kama nchi...Wana hadi wimbo wa wa Taifa nk.
Ni vyema tukaweza kutofautisha mambo ya muungano na hili ninalolizungumzia hapa,, ambapo wengi wetu wanaongozwa na hisia pamoja na nidhamu ya woga wa mazoea, wakidhani kuwa amani tuliyonayo ipo kwa bahati mbaya tu!?
Hilo la kipimo ama kikomo cha uongozi, ni Issue ya kikatiba kama ilivyo ile ya muungano.
Sasa umekubali kuhusiana na hayo ya kina Mwinyi, hayo yalikuwa ya kikatiba lakini bado unalalamika kuwa hakuwa mzanzibari, kesho utaacha kulalamika kwanini hakuwa muislam? Sasa hapo nani atakuwa mdini?
Twende taratibu mkuu...Ushaanza kulalamika Mwinyi hakuwa mzanzibari.Unadhani ungeacha kulalamika endapo asingekuwa muislam!?
Unafiki unatusumbuwa watanzania! Tusijadili kwa hisia, tutulizane tutumie fahamu zetu ipasavyo bila bias!