Rais ajaye ni lazima awe mkristo?

Rais ajaye ni lazima awe mkristo?

Hata Kijana, kuanzia jina ni Christian name, mama ni Christian, Mke ni Christian, watoto ni Christian, na kanisani ataingia!. Uislamu wake ni kwa Baba tuu kama alivyo Baraka Hussein!. He is fit in every aspects!.
Pasco

Pasco ndugu yangu umehama kambi ya Lowassa?
Bora ushabikie Wassira kuliko huyo Makamba.
 
Mkuu dunia ya sasa maoni ya watu yanaruhusiwa kabisa almradi hauvunji sheria ya nchi!

Dunia ya sasa ya kisiasa ni ya kuvumiliana tu mkuu!La sivyo tutajingiza kwenye udikteta na kuvunja haki za binadamu!

Cha msingi ni sisi kuchambua mchele na pumba, na kubakiza mchele pumba tupa huko!

Ukiwa una mind kihivi, basi utashangazwa sisi wachagga tunavumiliaje kutukanwa kila siku na watu kulike hizo comment?

Kiukweli kwenye hii thread ni kauli mbili tatu tu za maudhi kutoka kwa baadhi ya member.Lakini ujumbe ni wa muhimu kiasi kwamba ni sawasawa tu kuwaignore.Ikiwa kuna comment umeiona kuwa offensive, basi bonyeza kitufe cha kureport abuse..

Other than that ni vyema tukajadili bila hisia, mihemko na kwa utulivu!

Uhuru lazima uwe na mipaka, ndio maana kuna maeneo watu huchora mistari ya kuonyesha mwisho wa jambo. Dunia ya sasa inaelekea kubaya sababu ya kusingizia uhuru, ndio maana ushoga, usagaji unapewa audience ya lazima, comment yangu ya kwanza inasimama.

Na wewe ni mmojawapo uliolike baadhi ya hizo comment za kipuuzi, Nimesikitishwa sana.
Kwa taarifa tu mimi ni mchaga na mkristo lakini NACHUKIA SANA UDINI NA UKABILA.
 
Haa haa kwa nini tusiwe na rais mpagani? Ila kwa mazoea ya taifa letu rais ajaye atakuwa mkristo tena mkatolikiki! Si unajua tena mfumo wetu ule ..!
 
Hata Kijana, kuanzia jina ni Christian name, mama ni Christian, Mke ni Christian, watoto ni Christian, na kanisani ataingia!. Uislamu wake ni kwa Baba tuu kama alivyo Baraka Hussein!. He is fit in every aspects!.
Pasco
Vgeugeu
 
Naona watu wanajadili kutokana na kwamba wagombea urais waliokuwa wamejiandaa sasa wanajitokeza! Makamba naona yuko kwa kasi sana na ana watetezi wengi ndani ya chama especially wale wa gia ya "rais kijana"

Si lengo la thread hii kusema kuw dini flani ndo kigezo cha urais kama vike wale wa kigezo cha ujana wanavyofanya.

Lengo halisi hapa ni kutafakari na kuchukua maamuzi ya busara zaidi.Tunafahamu taifa letu mbali na kugawanywa kwa misingi ya chuki za kikabila na kidini zilizochochewa kwasababu tu ya ulafi wa madaraka na wagombea wa chama tawala esp. Uchaguzi uliopita!

Mbali na hayo, chini ya taratibu zetu ndani ya awamu nne, hatujawahi kuwa na marais wawili mfululizo wenye imani moja!

Kwa utaratibu huo, ni wazi kuwa sasa ni muhimu tukapata kiongozi mwenye imani ya tofauti, inaweza ikawa hata mpagani!

Tusipofanya hivyo, tunaweza tukapata matatizo yatakayopelekea kudumaa kwa shughuli za kimaendeleo hususan jitihada zetu za kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini kwa kutumia nguvu kazi, maarifa pamoja na rasilimali zetu ikiwemo watu.

Pia haina maana kuwa hatuna haki ya kuendelea kuwajadili wale wenye imani sawa na rais anayemalizia muda wake, ie Membe na Makamba, bali ni muhimu kutilia mkazo umoja wetu na mshikamano wetu, vitu ambavyo vimetusaidia kudumisha amani miongoni mwetu!

Nina amani kuwa rais anayekwenda kumaliza muda wake, aliweza kupata madaraka hayo kwasababu watanzania waliudumisha utamaduni ule wa kuhakikisha hatupati watawala wenye kutoka kwenye imani moja awamu mbili mfululizo.

Unless tuwe na viongozi wenye qualifications ambazo zinawazidi wengine wote kwa kiasi kwamba kuuvunja utamaduni wa kubadilisha watawala kwa kuzingatia imani kukawa justified!

Utamaduni huu upo taka tusitake, nafahamu kuna watakaosema kiwa huo ni utaratibu wa ccm, well! Ccm ndo wanatupatia watawala, na hilo la dini za watawala wetu limekuwa ni mjadala nchini mwetu na hata humu jukwaani sote tunafahamu hilo.

Kwa maoni yangu, hypothetically, si vyema kureplace malalamishi ya mfumo wa imani moja kwa kuupachika mfumo wa imani nyengine.
Ngoja nikuache sababu wewe mbishi sana.
 
Tunataka mtu mwenye uchungu na nchi yetu
Aliye tayari kujitoa kwa maslahi ya wananchi wake atakayekaa muda mwingi na kuangalia matatizo ya nchi na kutafuta namna ya kusolve sio kila kukicha kuzurula ovyo ,na Bla Bla za kila siku
 
Hivi nyie watu mbona hamdai rais anayekuja awe Mwanamke? Au awe Muhindi au Mwarabu? Na yule anayesema waislam ni failure anatumia vigezo gani? Pengine atupe mchanganuo wake kwani as far as I know watendaji wakuu wa serikali wengi tangu enzi za nyerere ni wakristo je nani ni failure?
 
umetisha....eti mafutari....jmn!!!haya mkuu...
ndo manake lazima awe mkristo ..tumechoka kugeuza Ikulu kuwa sehemu ya kulia mafutarina kufanya mahitima january to december.. vile vile hatutaki rais anayenyoa upara
 
Rais anatakiwa kua Mtanzania, mchapa kazi, mfia nchi, mpenda maendeleo, mchukia ufisadi!! dini, rangi, jinsia, kabila haviwezi kua vigezo vya kutupatia Rais!!
 
Mkuu Nduka, ukienda kwenye mnada wa hadhara, kama hicho kitu unakitaka wewe, utakwewnda na timu 3. Timu moja ni ya kwako mwenyewe, timu nyingine ni ya kuwakimbiza serious contenders wote kwa kila atakayeku outbid, mtu wako atamfurusha kwa ku bid very high hadi mwisho wa siku, the highest bidder ni mtu wako, the second highest pia ni wako na wewe ndio the 3rd.

Wakati wa kulipa, the ist and the 2nd watafanya no show, ili mzigo uangukie kwako!.

Kwa wanaozijua siasa za nchi hii, JM na EL ni kambi ile ile sponsored by "the King Maker!", kuna watu niliwaeleza humu tangu mwanzo, kuna watu ni just "pace makers" na kina Yohana Mbatizaji tuu, wakiyanyoosha mapito ya "the chosen one!", hawakunielewa!, labda sasa wataelewa kwamba "that is what is the name of the game!", na kujua "the games people play!", "plays our minds away!".

Pasco

Pasco nimekuelewa na hata mimi naamini kikatiba January hana sifa za kugombea urais na ndio maana hata comments za kikwete kwa mtu mwenye akili timamu anajuwa hili ni chase linachezwa.

huyu dogo shida yake ni awe waziri mkuu wa mr edo.
 
Umebadili kambi?
No this is the game!.
Mkuu Nduka, ukienda kwenye mnada wa hadhara, kama hicho kitu unakitaka wewe, utakwewnda na timu 3. Timu moja ni ya kwako mwenyewe, timu nyingine ni ya kuwakimbiza serious contenders wote kwa kila atakayeku outbid kwa kupaisha dau kwa kuwafurusha wote wanaojaribu hadi mwisho wa siku, the highest bidder ni mtu wako, the second highest pia ni wako na wewe ndio the 3rd.

Wakati wa kulipa, the ist and the 2nd watafanya no show, ili mzigo uangukie kwako!.

Kwa wanaozijua siasa za nchi hii, JM na EL ni kambi ile ile sponsored by "the King Maker!", kuna watu niliwaeleza humu tangu mwanzo, kuna watu ni just "pace makers" na kina Yohana Mbatizaji tuu, wakiyanyoosha mapito ya "the chosen one!", hawakunielewa!, labda sasa wataelewa kwamba "that is what is the name of the game!", na kujua "the games people play!", "plays our minds away!".

Pasco
 
Hata waunde kambi gambi...kuuzika kwao kugumu 2015. Watanzania wako macho si kawaida.
 
Pia haina maana kuwa hatuna haki ya kuendelea kuwajadili wale wenye imani sawa na rais anayemalizia muda wake, ie Membena Makamba, bali ni muhimu kutilia mkazo umoja wetu na mshikamano wetu, vitu ambavyo vimetusaidia kudumisha amani miongoni mwetu!
Una maana Mheshimiwa Membe na JK imani yao ni moja, au?
 
Kamanda mie nipo namshukuru mola niko hai,

Unajua mkuu amani tuliyo nayo it is not amani bali woga na ni kwasababu watanzania hawajaamka kujua haki zao na jukumu la watu wanaopewa uongozi. Ukweli wa mambo ikipotea hii nidhamu ya woga na watu wakawa na courage ya kudai haki zao amani unayoiona itapotea kama siagi inayowekwa katika jua.

Turudi katika mada Swala la uzanzibari ni la msingi sana hasa wakati huu ambapo muungano upo kitanzini. Rasimu ya warioba imeamsha mwamko na hamasa ya uzalendo na utaifa wa kila upande. Upande mmoja ukitetea maslahi ya wazanzibari na kudai mamlaka yao kamili na upande wa pili wakidai uwepo wa Tanganyika na kudai kujitenga na Zanzibar. Kiufupi Taifa la Tanzania liko mashakani kupotea na kuzaliwa tena upya kwa mataifa mawili ya Tanganyika na Zanzibar.

Hoja ya Rais Mzanzibari ina mashiko zaidi kuliko mkristo kwani kwanza itasaidia kurudisha umoja wa Kitanzania ambao umedumu miaka 50 sasa. Pili sio umoja tu hata amani kwani mihemko hii ya uzanzibari na utanganyika sio yote inaishia mwisho mwema. Hivyo ni vema tukauenzi utanzania wetu na kumuenzi baba wa Taifa na jitihada alizozifanya kuleta umoja na mshikamano nchini.

Pili hoja ya Rais mkristo haina mashiko kwasababu badala ya kuleta amani itachochea mpasuko zaidi. Kwanza elewa hata kama walikuwa marais waislamu kwa kipindi cha miaka 10 lakini Serikalini na kwengineko bado wakristo ni wengi sana kulinganisha na waislamu. Kwa kuanzia asilimia 75 ya cabinet members ni wakristo ambapo waislamu ni asilimia 20 na 5 dini nyenginezo kama wapagani. Sasa ratio hii haiko sawa na hili limeleta manunguniko mengi miongoni mwa waislamu hadi kupelekea kudai kuna MFUMO KRISTO Tanzania.

Vile vile hata ukienda katika taasisi zenginezo kama mahakama na kwengineko ratio ya wakristo dhidi ya waislamu ni kubwa sana mfano mahakama tu.

Sasa pamoja kansa hii bado tunapiga debe tunataka Rais ajaye awe mkristo je tutafika?

Mwisho kabisa matatizo yetu watanzania sio dini bali ufisadi na kama tutapata Rais mwadilifu na mchapakazi awe mkristo, mwislamu na pagani huyo ndio anafaa kuwa kiongozi na sio kulazimisha awe mkristo hilo ni kupoteza mwelekeo ndugu.

Chukua like mkuu.kama hivyo kila taasis iwe equal.
 
Back
Top Bottom